Kesi namba 458 (Jamhuri vs JamiiForums) yaahirishwa. Hakimu abadilishwa, Jamhuri yaomba kupitia upya faili la shauri

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
Kesi namba 458 ya Jamhuri vs Maxence Melo na mwenzake Micke William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha .TZ imeendelea leo Machi 13, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Kesi hii iliyokuwa chini Hakimu Victoria Nongwa imehamishiwa kwa Hakimu Huruma Shaidi baada ya Hakimu Nongwa kuhamishwa kutoka Mahakama ya Kisutu na kwenda Idara Mpya ya Usimamizi wa Mtiririko wa Kesi.

Shauri hili limeahirishwa mpaka Aprili 05, 2018 baada ya Wakili wa upande wa Jamhuri, Clara Charwe kudai hakuwa na ufahamu mzuri wa faili la shauri lenyewe(huyu ni mgeni kwenye hii kesi). Wakili Clara aliomba akumbushwe rekodi za mahakama juu ya shauri hili.

Awali, shauri hili lilikuwa chini ya Mawakili Salum Mohammed ambaye alimkabidhi Wakili Mutalemwa Kishenyi naye akamwachia Wakili Batilda Mushi na leo hii ametokea Wakili Clara Charwe.

Ikumbukwe mara ya Mwisho wakati wa ahirisho la shauri hili chini ya Hakimu Nongwa alisema lilikuwa ni ahirisho la mwisho na kuwataka Jamhuri kumaliza kuleta mashahidi wao ili hatua nyingine zifuate. Pia aliwaambia Upande wa Jamhuri kuwa inawezekana wanataka Washtakiwa waendelee kuwa na kesi mahakamani kwa kuwa kila mara wanaaihirisha kesi kwa kisingizio cha kukosa mashahidi na hata wakiwa na mashahidi wanaairisha kwa kisingizio cha kuwa ‘busy’ na kesi nyingi zinazoingiliana. (Soma: KISUTU: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidhi ya JamiiForums ya kutotumia Kikoa cha .TZ, yaahirishwa kwa mara ya mwisho )

Pia soma kujua mfululizo wa Kesi za JamiiForums.com => Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums
 
Kwa hiyo wanarushiana mpira?? Yani wamebadilisha mawakili watatu kesi moja??

Washukuru mungu Lissu hayupo!!
 
Naona hawa matutusa wameanza kupoteana kiaina. Mungu wetu, mwenye haki yu pamoja nasi. Whatever figisufigisu these TWITS will create against JF, they will completely fall through.
 
Back
Top Bottom