Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 60
- 1,237
Updates kesi ya bandari.
Majaji wanaingia muda huu saa 14:45
Kalani anataja namba ya kesi.
KESI YA KIKATIBA NA.5/2023
Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.
MAWAKILI WA SERIKALI; kwa kifupi SA.
1. Adv. Muluambo
2. Edson
3. Alice Mkulu
4. Stanley Kalokola
5. Edwin
MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI:
1. Mpale Mpoki
2. Boniface MWABUKUSI
3. Philip Mwakilima
4. Livino Ngalimitumba
WAKILI MULUAMBO SA;
Waheshimiwa Majaji, tulipokutana tarehe 20/7/2023 tulikubaliana mambo yafuatayo;
1. Kwamba Shauri hili lingekuja leo kwaajili ya Kusikilizwa
2. Kwamba usikilizwaji wa shauri hili ungefanyika kwa kuanza na mapingamizi ya awali na mfululizo kuendelea na shauri mama mpaka tutakapomaliza.
Waheshimiwa Majaji, leo hii tumepata fursa tena ya kuangalia hoja na majibu ya pande zote mbili na kwa kuzingatia kwamba hili ni shauri la Kikatiba na kwa kuzingatia kwamba ni vema Umma wa Watanzania ukapata majibu kuhusiana na shauri hili ambalo liko Mahakamani.
Hivyo, tumefikia uamuzi baada ya kukubaliana na Waleta maombi kwamba ili shauri hili lisikilizwe kwa uharaka, sisi upande wa Serikali tuondoe Mapingamizi yote ya Awali ambayo tulileta mahakamani.
Lengo la uamuzi huu ni kupisha Usikilizwaji wa Shauri mama.
Na pia tulikubaliana na pande zote kwamba hakuna upande utakaoomba gharama.
WAKILI WA SERIKALI anaendelea...
Waheshimiwa Majaji, kati ya mambo yanayobishaniwa (issues) sita; kuna yale ambayo tunakubaliana na yale ambayo hatukubaliani pande zote mbili. Mambo haya tutakuja kuyataja mbeleni.
Hivyo kwakuwa kuna maombi ya kuondoa Mapingamizi yetu, ikiwa wenzetu hawatakuwa na maombi yetu basi tungeomba Mahakama itoe Amri kwamba Mapingamizi yote yameondolewa na kisha Mahakama itoe amri itakayoona inafaa ili kuendelea na hatua nyingine.
Naomba Kuwasilisha!
MAJAJI watatu;
1. Hon. Ndunguru
2. Hon. Ismail
3. Hon. Kagomba
Wote wameinama wanaandika.
WASAIDIZI WA MAJAJI pia watatu;
1. Verus (Hakimu)
2. Mtafya (Hakimu)
3. Mapunda (Karani)
Nao wanaandika mambo yao.
WAKILI WA SERIKALI MULUAMBO anaendelea;
Order XIV Rule 3 ya CPC kwamba kabla ya Kusikilizwa kwa mashauri ya aina hii, yale mambo ambayo tunataka Mahakama iyatolee uamuzi yanapaswa kuandaliwa. Yaani 'issues need to be framed.' Na hilo hufanywa na pande zote pamoja na Mahakama.
Kwa kutii maelekezo ya Sheria, pande zote mbili zimefanya hivyo.
Yapo mambo ambayo tumekubaliana pande zote na yapo ambayo yana ubishi hatujakubaliana tutaacha Mahakama itoe maelekezo.
Wakili wa serikali anaendelea;
Waheshimiwa Majaji, yapo mambo matano ambayo pande zote tumekubaliana ila lipo jambo moja ambalo hatujakubaliana na tumeliwasilisha mbele ya Mahakama.
Kwa ruhusa yenu, tunaomba sasa tuwasilishe mambo hayo mbele ya Mahakama ili yaweze kurekodiwa na kuwa sehemu ya mwenendo wa shauri hili, iwapo wenzetu upande wa pili watakuwa tayari kwa hilo.
Naomba kuwasilisha.
Sasa anasimama wakili wa walalamikaji senior ADV. MPALE MPOKI:
Adv. Mpoki; Waheshimiwa Majaji, naomba sasa niwasomee issues;
1. Whether the signing/tabling nad ratification of the IGA was in contravention of Section 11(1)(2) of the Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act No.5 of 2017, read together with Section 5(1),6(2)(a),(b),(d) &(i) of the Natural Wealth (Review and Renegotiation of Unconscionable Terms) Act No.6 of 2017.
2. Whether the public was duly notified and afforded reasonable time to participate and give their opinion according to the laws during the ratification process of the IGA between Tanzania and the Emirate of Dubai.
3. Whether Article 2, 4(2),5(1),6(2),7(2),8(1)(a),(b),(c),3(2),10(1),20(2)(a),(e), (i),(ii), 18, 21,23 (1,3,4) 26,27 of the IGA contravene Article 1,8,28(1),3 of the Constitution of the United Republic of Tanzania
4. Whether Article 2, 23 of the IGA contravene Section 25 of the Law of Contract Act of Tanzania
5. Whether the IGA between Tanzania and Emirate of Dubai followed the legal procedures on selection methods of procurement process prescribed under Section 64 of the Public Procurement Act of Tanzania
Anaendelea senior Adv. Mpare.
WAKILI MPALE anaendelea...
5. Whether the Parties to the IGA had capacity to contract on the same.
Waheshimiwa Majaji, hii ni issue ambayo haijakubaliwa na pande zote. Upande mmoja umeweka, na wengine hawajakubaliana.
Hivyo, katika hii moja tunaomba kuacha mbele ya Mahakama ili itupe mwongozo.
WAKILI wa serikali aitwaye KALOKOLA :
Wakili wa serikali; Waheshimiwa Majaji, kimsingi Issues zilizokubaliwa tumeangalia Hoja zao za Malalamiko ambayo wameleta mahakamani.
Lakini hoja kuhusu uwezo kwamba iwapo Walioingia kwenye mkataba walikuwa na uwezo kisheria, haikuwa katika sehemu ya Malalamiko yao.
Sisi kwetu tumeona wametushtukiza kujibu hoja ambazo nyaraka za madai hazikuibua na sisi hatukuijibu katika majibu yetu.
Huo ndio msingi wa kwanini tunabishania. Anamaliza wakili wa serikali.
Anasimama wakili MPALE MPOKI kujibu
Adv. Mpoki; Sisi katika Affidavit yetu ambapo Paragraph 9 tumelisema hilo wazi.
Majibu yao ya tarehe 13/7/223 Paragraph 8 na 9 wamejibu kukataa allegations zetu za Paragraph 9. Hiki ni kiapo cha Afisa wa serikali aitwaye MOHAMED SALUM.
Hili siyo kama shauri la madai ya kawaida ambapo maelezo unayapata kwenye Plaint.
Sisi hii ni Originating Summons pamoja na Affidavit. Na wao wamejibu Malalamiko yetu.
Ni hayo Waheshimiwa.
Anasimama tena WAKILI wa serikali aitwaye KALOKOLA :
Wakili wa serikali: Waheshimiwa Majaji, kimsingi Issues zilizokubaliwa tumeangalia Hoja zao za Malalamiko ambayo wameleta mahakamani.

Kwanza ni msimamo wetu kwamba hoja inayobishaniwa majibu yanatolewa kwenye kiapo.
.
Kiapo ni ushahidi. Hoja zinazobishaniwa hutolewa kwenye Nyaraka za madai na sio kiapo.
******
Mahakama inafanya mahojiano ya maridhia (consensus) na pande zote nje ya mwenendo (offrecord) juu ya kuandaa Issues.
MAHAKAMA imerejea kwenye mwenendo wake baada ya mabishano ya Issue kati ya pande mbili.
JAJI KAGOMBA anatoa maelekezo;
Mahakama inakubali kwamba viini vitakavyohitaji kuamuliwa na Mahakama ni vile vinne ambavyo pande zote zilikubaliana. Na sisi tumeongeza viini viwili na kuwa jumla 6.
Issue ya mwisho whether the IGA is a contract itakuwa sasa ni namba 4.
Anasimama wakili wa wananchi MPALE MPOKI.
Adv: Mpoki; Waheshimiwa Majaji, kabla hatujaendelea natazama muda naona sasa ni saa 10 Jioni. Tukianza sasa hatutaweza kuendelea sawia. Na pia Issue moja iliyokua framed upya ili tuitendee haki, itakuwa vyema tupate adjournment ili kesho tuje tukiwa na fresh Mind and Spirit.
I humbly submit
WAKILI wa serikali aitwaye EDSON anajibu;
Wakili wa serikali; Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, Sisi tuna mtazamo tofauti kidogo na wenzetu.
Kesi hii imekuwa ya wananchi na ndio maana ukumbi umejaa. Kila kilichoendelea asubuhi (wananchi) walitaarifiwa kwamba shauri litaendelea saa 8 mchana. Kwahiyo kuwepo kwao hapa kuna maanisha kwamba kesi yao itaendelea.
Kama muda ulivyoendelea kwao na kwetu pia hivyo umeenda. Kwahiyo maombi yetu ni kwamba, licha ya kuwa issue moja imeongezeka (Na.4) na Waleta Maombi ndio wanaijua kesi yao hatutegemei kwamba itakuwa wanahitaji kwenda kujiandaa upya.
Ni maombi yetu kwamba tunaweza kuanda na issue zinazotangulia na tutakapoishia muda wowote tutasimama kwaajili ya kuendelea kesho.
Sisi upande wa Wadaiwa tupo tayari kuendelea.
********
Mahakama inatoa amri kwamba kesi hii itaendelea kesho 26th Julai 2023 saa tatu kamili Asubuhi.