SoC02 Kesho ya Afrika ipo katika mtandao

Stories of Change - 2022 Competition
Sep 13, 2021
11
204
4D43651F-A146-43CE-BBC8-8BB7FB396628.jpeg

Africa, ni moja ya bara lenye rasilimali nyingi, licha ya kuwa na rasilimali nyingi Africa bado inatambulika kama bara lenye uchumi wa tatu. Moja ya sababu kubwa inayoifanya Africa ishindwe kukuwa kiuchumi ni kukosa muunganiko wa soko.

Ukitizama mataifa yenye uchumi mkubwa duniani yote yanasifa ya kuwa na soko kubwa la watumiaji. Ukitizama China na Marekani zote zina soko linalozidi watu billioni moja, hata India inayokuwa kwa kasi kubwa kiuchumi inasoko linalozidi watumiaji bilioni moja. Kuwa na soko kubwa la ndani linasaidia serikali, biashara na viwanda kuweza kuimarika na kupata faida kubwa hata kabla ya kufikiria uwekezaji wa nje. Makampuni ya China na Marekani yanaweza kupata mafanikio makubwa ndani ya masoko yao ukilinganisha na makampuni ya Africa.

Kwa mfano, Biashara ya Tanzania ikiweza kupenya na kufikia asilimia 20% ya idadi ya watu wa Tanzania, itakuwa na watumiaji takribani milioni 15, lakini kampuni ya China ikiweza kupenya na kufikia asilimia 20% ya idadi ya watu wa China itakuwa na watumiaji takribani millioni 200.

Hii ni changamoto inayodumaza uchumi wa mataifa ya Africa. Hatuna soko pana, licha ya Africa kuwa na idadi ya watu wasiopungua billioni 1.3 kwa takwimu za 2020.

Moja ya sababu inayofanya Africa kutokuwa na muunganiko wa soko ni mipaka ya nchi zetu. Africa ina nchi huru 57, na kila nchi ina uongozi, katiba, sera na sarafu yake binafsi. Kampuni ya Tanzania inapoenda Kenya kufungua biashara tayari ni uwekezaji wa kigeni nchini Kenya. Huu mtazamo na mipaka baina yetu sisi wa Africa ndo inayoturudisha nyuma ingawa mataifa ya kigeni yanaona fursa ya Africa kama soko moja. Taswira yetu inahitaji kubadilika na kuunganisha masoko yetu kama tunataka kujitoa katika uchumi wa tatu duniani.

Swali linakuja ni namna gani tunaweza kuunganisha soko letu la Africa.

Ili Africa iweze kunufaika na idadi kubwa ya watu kwenye bara letu, inabidi tuunganishe soko letu, na hii itawezekana kupitia fursa ya tecknologia ya mtandao maarufu kama internet. Mtandao hauna mipaka kama ilivyo kwa nchi zetu, mtandao tayari unatuunganisha na ndugu na jamaa zetu waliopo ndani na hata nje ya Africa. Mfano mzuri kupitia application ya whatsapp, tunaweza kuwasiliana bila kujali mipaka ya nchi zetu.

Mtihani ulio mbele yetu ni namna gani tunaweza kuitumia fursa hii ambayo tayari imeonyesha uwezo wa kutuunganisha na kutufikia watu wote, na kuweza kuitumia kuunganisha masoko yetu, tuweze kupata maendeleo kiuchumi.

Africa tunahitaji kutengeneza mfumo wa kuaminika wa soko la kimtandao ( E-commerce Platform), pamoja na mfumo bora wakufanya malipo mtandaoni. Hii mifumo miwili itakuwa chachu ya mafanikio ya biashara mtandaoni.

Mfumo wa masoko, utamwezesha mtumiaji kuwa na biashara mtandaoni ambayo wateja kutoka mataifa yote hamsini na saba ya Africa wanaweza kuifikia kiurahisi na kufanya manunuzi kupitia simu janja. Fikra yangu kubwa ni kwa mfanyabiashara wa kawaida wa Tanzania kuweza kuuza bidhaa zake Africa nzima katika kiganja cha mkono wake, hii ndo fursa ya karne ya 21, na sababu inayofanya ni thubutu kusema kesho ya Africa ipo katika mtandao.

Kwa mfumo wa kibiashara tunaotumia sasa hivi, itamgharimu mfanyabiashara au kampuni mamilioni ya fedha ilikuweza kuuza bidhaa zake kwenye nchi nyingine ya Africa.

Lakini tukiweza kufanikisha soko la kimtandao na mfumo wa malipo utakaofanya kazi kwa ufanisi tunaweza kukwepa gharama kubwa za uwekezaji katika kufikia masoko mapya. Na kutumia hizo rasilimali kuhakikisha tunatengeneza miundombinu sahihi ambayo itasaidia soko la mtandao kukuwa kwa urahisi Africa, maana changamoto kubwa itakayo tukabili ni swala la miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa urahisi na uharaka. Ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa technologia ya reli za kisasa ambazo zinazaweza kuunganisha mataifa yote ya Africa, nina imani kama serikali zetu, jumuiya zetu za maendeleo (SADC,EAC), pamoja na wadau wa biashara Africa tukiunganisha nguvu na mawazo changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.

Sekta nyingi sana zitanufaika kutokana na fursa hii. Ukiachilia mbali ukuaji wa uchumi wa nchi za Africa ambao utanufaika na ongezeko la soko la watumiaji.

Sekta ya usafirishaji na uchukuzi itanufaika kutokana na biashara ya soko la mtandao kwenda bega kwa bega na usafirishaji kwa sababu watumiaji hawaonani ana kwa ana. Mfumo ukifanya kazi kwa ufanisi na kufanikiwa kuunganisha nchi zote za africa makampuni ya usafirishaji yatakuwa kwa kasi pia miundombinu ya Africa itaendelezwa ili kuweza kurahisisha biashara.

Sekta ya viwanda vya ndani, itanufaika pia, makampuni ya Africa yataweza kutanua masoko yao na kufikia watu wengi zaidi. Nchi ya China ni ushahidi tosha kupitia soko lao la Alibaba viwanda vya uzalishaji vimeweza kuimarika na kuuza bidhaa duniani kote. Pia ushindani na ubora wa bidhaa utakuwa maradufu.

Vijana watapata ajira mpya kupitia kukua kwa sekta hii ya teknologia, kuanzia kuajiriwa na kujiajiri kwenye sekta ya usafirishaji, pia kujiajiri kwenye sekta ya upigaji picha wa bidhaa, branding ya maduka ya mtandao na kadhalika. Itakuwa rahisi pia kwa vijana kuingia na kujiajiri katika soko la Africa, utahitaji kuwa na biashara pamoja na simu janja na utaweza kunufaika na muunganiko wa soko mtandaoni.

Biashara ya mtandaoni (e-commerce) sio wazo jipya, ni fursa ambayo imeweza kuthibitisha manufaa yake katika mataifa makubwa duniani. Kutokana na takwimu za forbes za mwaka 2021, Marekani ilifanya mauzo ya dola billioni 870 za kimarekani katika masoko ya kimtandao.

Pia mwaka 2020 kampuni ya Alibaba na JD.com ambayo ni masoko ya mtandao nchini china. Yalivunja rekodi za mauzo yaliyofikia dola billioni 115 za kimarekani katika kipindi cha siku 11 kutoka novemba 1 mpaka novemba 12 katika tukio la watu walio single linalo adhimisha nchini china , ambapo pia watumiaji 800 millioni walishiriki katika manunuzi hayo mtandaoni.

Hii inatuonyesha uwezo na nguvu ambayo masoko ya mtandao yanaweza kuisaidia Africa kiuchumi endapo tutayafanya kwa ufanisi kwa maana sekta hii bado ni changa katika bara letu la Africa. Kunukuu maneno ya hayati Mwl Julius Nyerere katika hutuba yake ya mwaka 1995, serikali zinabidi kujitolea katika maendeleo ya taifa na kuzilea sekta binafsi mpaka zitakapo weza kupambana kiuchumi. Na hivi ndo tunavyotakiwa kuikuza sekta hii kwa kuungana nguvu sekta binafsi na serikali za africa kwa ujumla, kama tunahitaji itupe mafanikio waliyopata mataifa mengine.

Kumbukumbu:
Alibaba, JD zaweka rekodi mpya zamauzo mtandaoni zilizofika dola billioni $115 za kimarekani. Mhariri ni Arjun Kharpal Nov 12 2020 (CNBC)

Manunuzi mtandaoni ya kuwa 50% mpaka 870 Billion. Mhariri by Jason Goldberg Feb18 2022, Jarida la forbes.
 
9C067D7C-F937-4D69-A037-BC0903617640.jpeg
Nimepata bahati ya kukaa China miaka mitano , nimejionea kwa namna gani biashara ya mtandao imeweza kubadilisha uchumi, kukuza sekta mbali mbali za uzalishaji na kuongeza ajira kwa watu tofauto.

Siku moja katika jiji la Shandong Jinan, nilishuhudia supermarket ikipunguza na kufunga matawi yake kwa sababu ilikuwa inafikia watu wengi na kufanya mauzo mengi mtandaoni kuliko kwenye matawi rasmi.

Siku hii ndio ilipo zaa ndoto yangu na kuamini kwamba kama Afrika itataka kupata mafanikio makubwa basi haina budi kuwekeza nguvu katika tecknologia ya internet.

Mataifa ya ughaibuni yametupita kwa vitu vingi lakini internet imeweza kutupa fursa ya kupambana na kukua kiuchumi. Ingawa kwa Africa bado hatujatumia hii fursa ipasavyo lakini manufaa yake hayafichiki katika jamii zetu.
 
View attachment 2309061
Africa, ni moja ya bara lenye rasilimali nyingi, licha ya kuwa na rasilimali nyingi Africa bado inatambulika kama bara lenye uchumi wa tatu. Moja ya sababu kubwa inayoifanya Africa ishindwe kukuwa kiuchumi ni kukosa muunganiko wa soko...
Changamoto hiyo e-commerce itauza product zetu maana yake apo tutakutana na competition nje( amazon nk) kwa hiyo viwanda vinabidi vijipange sana na kujitangaza kwa nguvu maana uelewa wa tecnology bado kutokana na data za TCRA 27% tu ya watu Tz bado nchi nyingine kwa hiyo hayo mapato kwa US na China bado
 
Hakuna Competition hapo, kama soko lipo simply natural selection will take place, High IQ shall win, Natural Resources favor Africans, intelligence?
 
Changamoto hiyo e-commerce itauza product zetu maana yake apo tutakutana na competition nje( amazon nk) kwa hiyo viwanda vinabidi vijipange sana na kujitangaza kwa nguvu maana uelewa wa tecnology bado kutokana na data za TCRA 27% tu ya watu Tz bado nchi nyingine kwa hiyo hayo mapato kwa US na China bado
Lengo kubwa ni kwa platform kuwa kwa ajili ya Africa na viwanda vyake.
 
View attachment 2309061
Africa, ni moja ya bara lenye rasilimali nyingi, licha ya kuwa na rasilimali nyingi Africa bado inatambulika kama bara lenye uchumi wa tatu. Moja ya sababu kubwa inayoifanya Africa ishindwe kukuwa kiuchumi ni kukosa muunganiko wa soko.

Ukitizama mataifa yenye uchumi mkubwa duniani yote yanasifa ya kuwa na soko kubwa la watumiaji. Ukitizama China na Marekani zote zina soko linalozidi watu billioni moja, hata India inayokuwa kwa kasi kubwa kiuchumi inasoko linalozidi watumiaji bilioni moja. Kuwa na soko kubwa la ndani linasaidia serikali, biashara na viwanda kuweza kuimarika na kupata faida kubwa hata kabla ya kufikiria uwekezaji wa nje. Makampuni ya China na Marekani yanaweza kupata mafanikio makubwa ndani ya masoko yao ukilinganisha na makampuni ya Africa.

Kwa mfano, Biashara ya Tanzania ikiweza kupenya na kufikia asilimia 20% ya idadi ya watu wa Tanzania, itakuwa na watumiaji takribani milioni 15, lakini kampuni ya China ikiweza kupenya na kufikia asilimia 20% ya idadi ya watu wa China itakuwa na watumiaji takribani millioni 200.

Hii ni changamoto inayodumaza uchumi wa mataifa ya Africa. Hatuna soko pana, licha ya Africa kuwa na idadi ya watu wasiopungua billioni 1.3 kwa takwimu za 2020.

Moja ya sababu inayofanya Africa kutokuwa na muunganiko wa soko ni mipaka ya nchi zetu. Africa ina nchi huru 57, na kila nchi ina uongozi, katiba, sera na sarafu yake binafsi. Kampuni ya Tanzania inapoenda Kenya kufungua biashara tayari ni uwekezaji wa kigeni nchini Kenya. Huu mtazamo na mipaka baina yetu sisi wa Africa ndo inayoturudisha nyuma ingawa mataifa ya kigeni yanaona fursa ya Africa kama soko moja. Taswira yetu inahitaji kubadilika na kuunganisha masoko yetu kama tunataka kujitoa katika uchumi wa tatu duniani.

Swali linakuja ni namna gani tunaweza kuunganisha soko letu la Africa.

Ili Africa iweze kunufaika na idadi kubwa ya watu kwenye bara letu, inabidi tuunganishe soko letu, na hii itawezekana kupitia fursa ya tecknologia ya mtandao maarufu kama internet. Mtandao hauna mipaka kama ilivyo kwa nchi zetu, mtandao tayari unatuunganisha na ndugu na jamaa zetu waliopo ndani na hata nje ya Africa. Mfano mzuri kupitia application ya whatsapp, tunaweza kuwasiliana bila kujali mipaka ya nchi zetu.

Mtihani ulio mbele yetu ni namna gani tunaweza kuitumia fursa hii ambayo tayari imeonyesha uwezo wa kutuunganisha na kutufikia watu wote, na kuweza kuitumia kuunganisha masoko yetu, tuweze kupata maendeleo kiuchumi.

Africa tunahitaji kutengeneza mfumo wa kuaminika wa soko la kimtandao ( E-commerce Platform), pamoja na mfumo bora wakufanya malipo mtandaoni. Hii mifumo miwili itakuwa chachu ya mafanikio ya biashara mtandaoni.

Mfumo wa masoko, utamwezesha mtumiaji kuwa na biashara mtandaoni ambayo wateja kutoka mataifa yote hamsini na saba ya Africa wanaweza kuifikia kiurahisi na kufanya manunuzi kupitia simu janja. Fikra yangu kubwa ni kwa mfanyabiashara wa kawaida wa Tanzania kuweza kuuza bidhaa zake Africa nzima katika kiganja cha mkono wake, hii ndo fursa ya karne ya 21, na sababu inayofanya ni thubutu kusema kesho ya Africa ipo katika mtandao.

Kwa mfumo wa kibiashara tunaotumia sasa hivi, itamgharimu mfanyabiashara au kampuni mamilioni ya fedha ilikuweza kuuza bidhaa zake kwenye nchi nyingine ya Africa.

Lakini tukiweza kufanikisha soko la kimtandao na mfumo wa malipo utakaofanya kazi kwa ufanisi tunaweza kukwepa gharama kubwa za uwekezaji katika kufikia masoko mapya. Na kutumia hizo rasilimali kuhakikisha tunatengeneza miundombinu sahihi ambayo itasaidia soko la mtandao kukuwa kwa urahisi Africa, maana changamoto kubwa itakayo tukabili ni swala la miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa urahisi na uharaka. Ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa technologia ya reli za kisasa ambazo zinazaweza kuunganisha mataifa yote ya Africa, nina imani kama serikali zetu, jumuiya zetu za maendeleo (SADC,EAC), pamoja na wadau wa biashara Africa tukiunganisha nguvu na mawazo changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.

Sekta nyingi sana zitanufaika kutokana na fursa hii. Ukiachilia mbali ukuaji wa uchumi wa nchi za Africa ambao utanufaika na ongezeko la soko la watumiaji.

Sekta ya usafirishaji na uchukuzi itanufaika kutokana na biashara ya soko la mtandao kwenda bega kwa bega na usafirishaji kwa sababu watumiaji hawaonani ana kwa ana. Mfumo ukifanya kazi kwa ufanisi na kufanikiwa kuunganisha nchi zote za africa makampuni ya usafirishaji yatakuwa kwa kasi pia miundombinu ya Africa itaendelezwa ili kuweza kurahisisha biashara.

Sekta ya viwanda vya ndani, itanufaika pia, makampuni ya Africa yataweza kutanua masoko yao na kufikia watu wengi zaidi. Nchi ya China ni ushahidi tosha kupitia soko lao la Alibaba viwanda vya uzalishaji vimeweza kuimarika na kuuza bidhaa duniani kote. Pia ushindani na ubora wa bidhaa utakuwa maradufu.

Vijana watapata ajira mpya kupitia kukua kwa sekta hii ya teknologia, kuanzia kuajiriwa na kujiajiri kwenye sekta ya usafirishaji, pia kujiajiri kwenye sekta ya upigaji picha wa bidhaa, branding ya maduka ya mtandao na kadhalika. Itakuwa rahisi pia kwa vijana kuingia na kujiajiri katika soko la Africa, utahitaji kuwa na biashara pamoja na simu janja na utaweza kunufaika na muunganiko wa soko mtandaoni.

Biashara ya mtandaoni (e-commerce) sio wazo jipya, ni fursa ambayo imeweza kuthibitisha manufaa yake katika mataifa makubwa duniani. Kutokana na takwimu za forbes za mwaka 2021, Marekani ilifanya mauzo ya dola billioni 870 za kimarekani katika masoko ya kimtandao.

Pia mwaka 2020 kampuni ya Alibaba na JD.com ambayo ni masoko ya mtandao nchini china. Yalivunja rekodi za mauzo yaliyofikia dola billioni 115 za kimarekani katika kipindi cha siku 11 kutoka novemba 1 mpaka novemba 12 katika tukio la watu walio single linalo adhimisha nchini china , ambapo pia watumiaji 800 millioni walishiriki katika manunuzi hayo mtandaoni.

Hii inatuonyesha uwezo na nguvu ambayo masoko ya mtandao yanaweza kuisaidia Africa kiuchumi endapo tutayafanya kwa ufanisi kwa maana sekta hii bado ni changa katika bara letu la Africa. Kunukuu maneno ya hayati Mwl Julius Nyerere katika hutuba yake ya mwaka 1995, serikali zinabidi kujitolea katika maendeleo ya taifa na kuzilea sekta binafsi mpaka zitakapo weza kupambana kiuchumi. Na hivi ndo tunavyotakiwa kuikuza sekta hii kwa kuungana nguvu sekta binafsi na serikali za africa kwa ujumla, kama tunahitaji itupe mafanikio waliyopata mataifa mengine.

Kumbukumbu:
Alibaba, JD zaweka rekodi mpya zamauzo mtandaoni zilizofika dola billioni $115 za kimarekani. Mhariri ni Arjun Kharpal Nov 12 2020 (CNBC)

Manunuzi mtandaoni ya kuwa 50% mpaka 870 Billion. Mhariri by Jason Goldberg Feb18 2022, Jarida la forbes.
Kama Africa tuna Mambo mengi Sana mazuri ya kujivunia na kuyatangaza duniani, tunakwama kwenye kuanza, Mimi naamini hili Jambo likianzishwa tutafika mbali Sana...Safari ya hatua 1000 huanza na hatua 1...tujipange, tuanze, tujiamini tutafanikiwa...hongera Sana Kwa idea nzuri
 
Nzuri sana👍🏾
 
Habari, kwa wageni wote jinsi ya kunipigia kura gusa kimshale hapa chini ya post chenye arama "^" chini ya chapisho.

Kama ukipata shida kwenye kupiga Kura Tafadhali nijulishe kwenye comment kwa maelekezo zaidi.

Tafadhali lakini pia usisahau Ku-like chapisho na kuacha maoni yako kuhusiana na chapisho hili
Sebastian sioni hicho kimshale
 
Tayr
 
Wazo Bora Sana,. Ili afrika tujinasue kwenye utumwa wa kiuchumi na kisiasa,lazima mipaka hii ilyowekwa na wakoloniniondolewe na isiwe kikwazo kwa ustawi wa maendeleo ya ya waafrika
 
Back
Top Bottom