Uchaguzi 2020 Kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,762
4,516
Wewe Mtanzania kesho ndio siku maalumu uliyongojea miaka 5.

Hakuna siku nyingine uliyopewa zaidi ya kesho ya kuchagua kuumizwa tena 5 au kutoumizwa tena.

Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu. Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.

Kama ulikosa ajira, mafao, mkopo, elimu, filisiwa, dhulumiwa, someshwa namba, na madhalimu yote ya kila namna haya mpira upo Kati goli lipo wazi ulenge au ulengeshwe tena 5 yrs za mateso, jasho na damu uamuzi ni wako.
 
Hayo matatizo yote yanaenda kutatuliwa na J.P. Magufuli pekee.

Hawa wenyewe hawana sera ya maendeleo na baadhi ya sera zao matusi tu. Tutawapumzisha waendelee na:
1. Ujenzi wa ofisi zao(kuondoa aibu ya kumiliki ofisi kama mabanda ya nguruwe).

2. Wajifunze namna ya kutumia ruzuku.

3. Pia wajipange katika uchaguzi ujao na kutafuta viongozi bora. Huku wakiacha maswala ya kulia lia kwa kila jambo.
 
Nawatakia mafanikio Wapenda Mabadiliko wote. Niliahidi kuwa tena Mpiga Kura Mtiifu mara tu huyu "Mzee" atakapo ondoka madarakani.

Kauli zake za vitisho, na pia yale maigizo yaliyotokea wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na wale Wabunge/Madiwani njaa, ulinikatisha kabisa tamaa ya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020!
 

"Kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi"


Hapana, sio kulipiza kisasi, Bali ni siku yako ya kutimiza haki yako ya kikatiba ya kumchagua kiongozi unayemtaka.
----
1603787757184.png
 
Hayo matatizo yote yanaenda kutatuliwa na J.P. Magufuli pekee...
Mna ofisi hata moja tu ya chama chenu mliyojenga kwa hizo hela za ruzuku? Kama ni hizo zilizopo, karibia zote zilijengwa na Nyerere na Mwinyi kwa kodi za Watanzania wote enzi za mfumo wa chama kimoja.

Ukija kwenye huo ukumbi wa Dodoma, mlijengewa na Wachina! Na mpaka sasa hatujui mliwalipa meno yetu ya tembo, au la! Halafu unapata kabisa ujasiri wa kuwanyooshea kidole wengine. Unafahamu hicho chama chako kingeshajifia kitambo bila msaada kutoka Polisi na NEC?
 
Kesho lazima Amsterdam na vibaraka wake wapigwe nje ndani.
Amsterdam kiboko ya madikteta ya afrika Anafile kesi direct the Hague sio wa mchezo mchezo shughuli yake pevu muulize Putin.Amedili na madikteta Sugu sembuse uchwara?
 
5 yrs ameshindwa nyongeza za mishahara tu kipi ndo ataweza ongezea maisha Bora kila mtz?
Ambacho ujui ni kitu kimoja. Kila miaka au serikali inapriority ya mambo fulani. Tumekamilisha kutengeneza mazingira kwa nchi kuwa ya viwanda na uwekezaji wa hali ya juu.

Haya mazingira ndiyo yanaenda kuzalisha ajira kwa watanzania na maisha bora kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom