Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 12,998
- 6,659
Tokea amechaguliwa 2010 sijawahi kumuona Huku Mbagala kuja kusikiliza Kero za wapiga kura wake Kama wanavyofanya wakina Mdee na Mnyika kwenye majimbo Yao yeye kutwa ni kufungua Album za miziki ya kwaya tuu.
Vilevile asifikirie ujenzi wa daraja la kigamboni atautumia kujinufaisha kisiasa kwamba amehusika kufanikisha ujenzi wake kwa michango yake bungeni tunajua hausiki hata chembe.
Huku mbagala, kongowe Pamoja na Toangoma wananchi wanaapa kutompa mbunge mvivu Kama Dr F. Ndugulile kura tena bora wangempa Komu wangepata uwakilishi mzuri Kama ilivyo ubungo na kawe.
2015 huyu mbunge wetu mvivu atakuwa kwenye wakati mgumu sana
MAJIBU YA MBUNGE:

Precise Pangolin,
Nashukuru kwa mtazamo wako. Kwa mwezi huu wa Septemba nimekuwa Mbagala siku zifuatazo:
2/9 - Mwaliko Ibada Mbagala KKKT. Mchana nilitembelea miundombinu ya barabara na madaraja inayohitaji maboresho.
6/9 - Nilikutanana kusikiliza kero za wananchi katika Ofisi yangu iliyopo Mbagala Kizuiani.
13/9 - Nilishiriki katika ukaguzi wa barabara ya Kilwa pamoja na Waziri Magufuli katika eneo la Kizuiani.
21/9 - Nilitembelea miundombinu na miradi ya maendeleo katika maeneo ya Mangaya na Moringe. Siku hiyo nilitembelea kata ya Kiburugwa maeneo ya Kingugi, kwa Dumbarume na kufanya mkutano wa hadhara Kingugi.
Kata ya Mbagala ina mitaa mitano, ni mtaa upi unaouongelea wewe? Kuhusu Toangoma nilikuwa na mkutano na wadau wa maendeleo wa sekta ya elimu juzi siku ya Jumamosi 22/9.
Nilaumiwe kwa mengine lakini si kwa ziara za kata na kuongea na wananchi.