Kero za wananchi Jimbo la Kigamboni na majibu ya mbunge...

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
13,001
6,659
Tokea amechaguliwa 2010 sijawahi kumuona Huku Mbagala kuja kusikiliza Kero za wapiga kura wake Kama wanavyofanya wakina Mdee na Mnyika kwenye majimbo Yao yeye kutwa ni kufungua Album za miziki ya kwaya tuu.

Vilevile asifikirie ujenzi wa daraja la kigamboni atautumia kujinufaisha kisiasa kwamba amehusika kufanikisha ujenzi wake kwa michango yake bungeni tunajua hausiki hata chembe.

Huku mbagala, kongowe Pamoja na Toangoma wananchi wanaapa kutompa mbunge mvivu Kama Dr F. Ndugulile kura tena bora wangempa Komu wangepata uwakilishi mzuri Kama ilivyo ubungo na kawe.

2015 huyu mbunge wetu mvivu atakuwa kwenye wakati mgumu sana

MAJIBU YA MBUNGE:

Precise Pangolin,

Nashukuru kwa mtazamo wako. Kwa mwezi huu wa Septemba nimekuwa Mbagala siku zifuatazo:

2/9 - Mwaliko Ibada Mbagala KKKT. Mchana nilitembelea miundombinu ya barabara na madaraja inayohitaji maboresho.
6/9 - Nilikutanana kusikiliza kero za wananchi katika Ofisi yangu iliyopo Mbagala Kizuiani.
13/9 - Nilishiriki katika ukaguzi wa barabara ya Kilwa pamoja na Waziri Magufuli katika eneo la Kizuiani.
21/9 - Nilitembelea miundombinu na miradi ya maendeleo katika maeneo ya Mangaya na Moringe. Siku hiyo nilitembelea kata ya Kiburugwa maeneo ya Kingugi, kwa Dumbarume na kufanya mkutano wa hadhara Kingugi.

Kata ya Mbagala ina mitaa mitano, ni mtaa upi unaouongelea wewe? Kuhusu Toangoma nilikuwa na mkutano na wadau wa maendeleo wa sekta ya elimu juzi siku ya Jumamosi 22/9.

Nilaumiwe kwa mengine lakini si kwa ziara za kata na kuongea na wananchi.
 
Si kweli hata kidogo........ NI mbunge wangu pia, nadhani kuna lako jambo maana CCM mkikosa wa kuwalipua na kuwaibia mnaishia kutafunana wenyewe

We can support different political ideologies but we need to be realistic when it comes to development
 
Mkuu Huku mbagala hatujawahi kumuona tokea 2010 tunajuta lakini 2015 asifikishe daluga Huku
 
andamananeni mumtoe sasa hv 2015 ni mbali atasababisha damage kubwa zaidi kama mpo serious lakini!
 
Si kweli hata kidogo........ NI mbunge wangu pia, nadhani kuna lako jambo maana CCM mkikosa wa kuwalipua na kuwaibia mnaishia kutafunana wenyewe

We can support different political ideologies but we need to be realistic when it comes to development

kama kuna mambo ameyafanya huko mbagala siumtajie mwana jombo mwenzako ?? acha bla bla blah
 
Mkuu Huku mbagala hatujawahi kumuona tokea 2010 tunajuta lakini 2015 asifikishe daluga Huku

kaka mbagala kubwa sana, uwe specific, ni sawa na kusema alifika kisota lakini mtaa wangu hakuja, au kaenda gezaulole lakini ras kutani hakufika

just be specific mkuu, maana kwenye wall yake na ile ya kigamboni i want kuna updates zote za kazi zake... there are a few members e.g. 235 mule nk

jana tu amepost kwamba alikua charambe kwenye shughuli ya kijamii, kiburugwa nk.
 
Kwani huo mzigo umefungashwa kwa super glue juu ya vichwa/mabega yenu??? Si muutue??? Kumbekeni wenzenu wameshatua mizigo yao na wako raha mstarehe. Nia nyingine, ushusheni huo mzigo muupakue upungue uzito halafu muubebe tena, itakuwa ni nafuu. Huo ni ushauri wangu wa bure!!!
 
Uzuri wa wabongo akija na tshirts na pilau isiyo na nyama mnasahau yote na kumpigia kura tena. Shamba la bibi, hadi mtakapoamua!
 
Uzuri wa wabongo akija na tshirts na pilau isiyo na nyama mnasahau yote na kumpigia kura tena. Shamba la bibi, hadi mtakapoamua!
TRUE THAT KAMANDA

waweza kuta alikua mpambe nambari wani sasa katoswa kwenye vikao vya alawansi anakuja kashika kichwa

Kila kitu kiko mikononi mwa wnannchi, kusuka au kunyoa

watu wanalalama weeeeeeee, ikija voting, wanaegemea kulekule
 
Hakuna mwanasiasa aliyeleta maendeleo nchi hii wote ni wale wale tu pasua kichwa na kupenda umaarufu usiokuwa na maana
 
kaka mbagala kubwa sana, uwe specific, ni sawa na kusema alifika kisota lakini mtaa wangu hakuja, au kaenda gezaulole lakini ras kutani hakufika

just be specific mkuu, maana kwenye wall yake na ile ya kigamboni i want kuna updates zote za kazi zake... there are a few members e.g. 235 mule nk

jana tu amepost kwamba alikua charambe kwenye shughuli ya kijamii, kiburugwa nk.
Jana alikuwa anafungua album ya nyimbo za dini Kama mgeni rasmi huyo tapeli mkuu tena ilikuwa ni gezaulole. Sehemu Kama kisota na kibada lazima aje kwasababu wanaishi watu wenye hela ndefu
 
Kwani huo mzigo umefungashwa kwa super glue juu ya vichwa/mabega yenu??? Si muutue??? Kumbekeni wenzenu wameshatua mizigo yao na wako raha mstarehe. Nia nyingine, ushusheni huo mzigo muupakue upungue uzito halafu muubebe tena, itakuwa ni nafuu. Huo ni ushauri wangu wa bure!!!
@Mama Mdogo ushauri nimeupata 2015 atanikoma
 
Lawama za namna hii haziwezi kumsaidia Mnunge yeyote. Kama suala ni kushirikiana na wananachi katika kuyatambua na kuyatatua matatizo Dr Ndungulile ameshiriki. Ni vyema kuwasifu uliowataja kwa sababu tofauti na hii ya "kumponda" Ndungulile kwa mambo yasiyo na msingi wa ukweli.
 
Mkuu subiri 2015 ili umuwajibishe,najua wewe ujamchagua ila wenzio wamewaponza kwa kudanganywa na khanga na tishert za kijani.

Pole sanaaaa, lazima awajibishwe 2015
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom