Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdul Aziz M. Abood anaendelea na ziara yake ya Kikazi kwenye Kata ya Mafiga na Kata ya Mbuyuni

Oct 8, 2023
37
17
30/11/2023

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Dkt. Abdul Aziz M. Abood anaendelea na ziara yake ya Kikazi kwenye Kata ya MAFIGA na Kata ya MBUYUNI.

Huu ni mwendelezo wa ziara yake inayopia mtaa kwa mtaa lengo la ziara hii ni kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Kila Kata na mitaa alikoenda Mhe Mbunge amewaeleza wananchi juu ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali na ya Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan aidha Mhe Mbunge amewaeleza wananchi kuwa Serikali ya Mama SAMIA ni Serikali sikivu ameongeza kuwa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana wananchi wake hapendi kusikia wanapata shida yoyote.

KATA YA MAFIGA akiwa Kata hii Mhe Mbunge amesikiliza kero za wananchi na kuzitatua baadhi ya kero zao papo kwa papo pia baadhi ya kero zilizoitaji majibu ya kina pamoja na ufatiliaji amezichukua changamoto hizo na kuwaahidi wananchi kuwa atazipatia majibu kwa haraka sana. Vilevile Mhe Mbunge ameahidi kuchangia kiasi cha Tsh (4,000,000 Million Nne) kwaajili ya kusapoti ujenzi wa vyoo vya wanafunzi kwenye Shule ya Msingi MISUFINI B ambayo ipo Kata ya MAFIGA.

KATA YA MBUYUNI
akiwa kwenye Kata hii Mhe Mbunge ilivyo kawaida ya ziara zake zote kipaumbele ni Wananchi wake wazungumze mambo yote ambayo ni kero kwao ili aweze kuyapokea na kuwapatia majibu ya kero zao. Mhe Mbunge amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya MBUYUNI na kuwapatia majibu ya papo kwa papo kwa asilimia kubwa ya kero zao. Vilevile Mhe Mbunge akiwa Kata hii ameahidi kuchangia TOFALI 2,000, SARUJI MIFUKO 30 NA NONDO PC 20 hii ni kwaajili ya kusapoti ujenzi unaoendelea Shule ya MBUYUNI MORDEN SECONDARY iliyopo kwenye Kata hii ya MBUYUNI
IMG-20231130-WA0375.jpg
 
Morogoro Dhiki Ya Maji Anawaeleza Nini Wananchi
AAlitakiwa 2025 Atupwe Nje Akaendeshe Bus
 
Morogoro Dhiki Ya Maji Anawaeleza Nini Wananchi
AAlitakiwa 2025 Atupwe Nje Akaendeshe Bus
Basi zake zinasidiaga misibani, daladala zikigoma abood anatoa, anasidia chakula kwenye misiba, utatuambia nini watu wa morogoro?
 
Basi zake zinasidiaga misibani, daladala zikigoma abood anatoa, anasidia chakula kwenye misiba, utatuambia nini watu wa morogoro?
Wee utakuwa ndo waleee! Hiyo misaada inasaidia nini kielimu, kiuchumi? Eti misaada kwenye misiba!
 
30/11/2023

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Dkt. Abdul Aziz M. Abood anaendelea na ziara yake ya Kikazi kwenye Kata ya MAFIGA na Kata ya MBUYUNI.

Huu ni mwendelezo wa ziara yake inayopia mtaa kwa mtaa lengo la ziara hii ni kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia I MORDEN SECONDARY iliyopo kwenye Kata hii ya MBUYUNIView attachment 2829853
Najaribu kuunganisha akili yangu, lakini bado haiungi. Kwa hiyo mkulu huwa anadesa? Kwamba mtu ambaye hana Romanians ndio akapita baharini na mkubwa naye fresh...hebu ngoja niendelee kuangalia Huba na jua Kali ....na jua litakuwa Kali sana sana...
 
30/11/2023

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Dkt. Abdul Aziz M. Abood anaendelea na ziara yake ya Kikazi kwenye Kata ya
Eti amesikiza kero za wananchi na kuzitatua!! Una uhakika!?
Yaani wanajua muda wa kuomba kura unawadia ili waendelee kukamua ngombe!.
Mbona asingelienda mwaka jana?
Wananchi tuendelee kuokotwa na maisha yaendelee kutupiga kwa sababu ya huu uoumbavu
 
Morogoro Dhiki Ya Maji Anawaeleza Nini Wananchi
AAlitakiwa 2025 Atupwe Nje Akaendeshe Bus
Hujaona clip amewaambia wana Moro kwamba atawanunulia chupa afu3 za mafuta ya mwamposya, na mwamposya ahamie Moro mazima. Nchi hii utaamaje Sasa?
 
Hujaona clip amewaambia wana Moro kwamba atawanunulia chupa afu3 za mafuta ya mwamposya, na mwamposya ahamie Moro mazima. Nchi hii utaamaje Sasa?
😄😅😁🤣😀😃😁🤣😀😀🤣Ila Ccm Jamani Shida
 
Back
Top Bottom