Kero ya Umeme, barabara yasimamisha msafara wa Chongolo. Atoa maagizo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo umesimamishwa na wananchi wa Msia, Kata ya Milepa, Jimbo la Kwela mkoani Katavi ili kufikisha kero yao ya umeme na barabara.

Wananchi hao wamesimamisha msafara huo leo Jumanne, Oktoba 10, 2023 wakati Chongolo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa chama hicho, Issa Ussi Gavu ukiendelea na ziara jimboni humo kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho 2020/25, kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Kutokana na kero hizo, Chongolo ametoa maagizobalimbali kwa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).
 
Back
Top Bottom