KERO Kero ya ubovu wa barabara ya Majohe Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ebbyramadhani

Senior Member
Jan 5, 2017
101
109
Habari za weekend wakuu, Tusaidiane kufikisha Hii taarifa ya adha inayowakumba wakazi wa Majohe kwa muda mrefu sana kuhusiana na ubovu wa barabara kuanzia shule ya sekondary Halisi mpaka kituo cha kwa mjeshi.

Barabara hii ni mbovu mno kupelekea vyombo mbali mbali vya usafiri ikiwemo usafiri wa umma kushindwa kupita hivyo kufanya magari kukatisha ruti njiani kukwepa eneo hilo ambalo ni korofi sana.

Wananchi wanalazimika kutembea kutoka Halisi mpaka Majohe kwa Mpemba ambapo ndo dalada ilipaswa kufika hapo kama kawaida ya mwanzoni kabla ya adha hii.

Kutoka Halisi mpaka kwa mpemba kuna km takriban zisizopungua 3.
Ubovu wa eneo hili unatokana barabara kutokuwa na mitaro na madaraja kwaajili ya kuvusha maji yanayotoka mitaani Hivyo kupelekea mvua zinaponyesha eneo hili linaharibika mara kwa mara.

Jitihada kubwa zinahitajika kusaidia wananchi wa Majohe kuweza kutatuliwa kero hii.

IMG_1072.jpeg
 
Attachments

  • IMG_1076.jpeg
    IMG_1076.jpeg
    6.5 MB · Views: 5
  • IMG_1075.jpeg
    IMG_1075.jpeg
    6 MB · Views: 4
  • IMG_1068.jpeg
    IMG_1068.jpeg
    3.2 MB · Views: 5
  • IMG_1069.jpeg
    IMG_1069.jpeg
    5.3 MB · Views: 4
Kijana wewe ni mrundi nini? Mbona eneo la kuweka R umeweka L na eneo la kuweka L umeweka R?

Namna hii ulichoandika kitaeleweka kweli? Maana kuna maneno mengine ukibadilisha tu herufi moja unaharibu maana nzima ya kile ulichoandika.

Btw poleni na matatizo ya barabara huko Majohe. Nakushauri uje uhamie huku Mbweni, kuna nyumba yangu ina vyumba vya kupangisha kwa gharama nafuu. Chumba kimoja napangisha kwa laki mbili tu mkuu.
 
Nimeandika nikiwa burundi mkuu
 
Hakuna sehemu yoyote aliyochanganya R na L.
Acheni ubaguzi wa kijinga. Na wewe ni mjinga, sifuri kabisa.

Mtu anaandika hoja ya msingi, unaleta ukarumekenge hapa.
 
Nilipita njia hiyo juzi kwa bodaboda...kwa vichochoro alivyopita baada ya kuliacha njia juu nilidhani nimetekwa!!! Barabara haipo kabisa hapo...ni eneo lililoachwa kwa ajili ya barabara!
 
Hiyo barabara nimepeleka abiria na bajaji yangu niliapa sitarudi huko na kweli sijawahi kurudi tena ni una dunda dunda hadi unafika
 
Nilipita njia hiyo juzi kwa bodaboda...kwa vichochoro alivyopita baada ya kuliacha njia juu nilidhani nimetekwa!!! Barabara haipo kabisa hapo...ni eneo lililoachwa kwa ajili ya barabara!
Alhamdulillah kwa wenye usafir na kipato cha kukodi boda
Kuna watu wanatembea mzee
 
Back
Top Bottom