Kero ya Muungano iliyotatuliwa ndani ya mwaka mmoja

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Nikiwa natazama TBC kipindi mwaka mmoja wa awamu ya sita. Moja kati ya mafanikio ni kupatiwa suluhisho kwa kero za Muungano na kero hiyo ni " Ajira za Zanzibar kwenye taasisi na wizara za muungano" Hii kero ndani ya mwaka mmoja imeshapatiwa suluhisho.

Hii kero imepatiwa suluhisho ndani ya muda mfupi mno. Hatujasikia tume ikiundwa wala ikiwasilisha mapendekezo yake.

Nani hasa huwa wanakaa na kuamua haya?

Hivi kero za Muungano ni upande wa Zanzibar tu?
 
Mimi nafahamu Wazanzibar kadhaa wapo TANAPA,AUWSA..... sasa sijui huu ujinga utamalizika lini !.

Hii kero kaitatua upande wa Zanzibar lakini kazalisha kero upande wa Tanganyika hizo hesabu sijui formula gani imetumika.
 
T

Tanganyika haina msemaji. Watoto wa viongozi hawana shida ya ajira. Huwezi kuwakuta uwanja wa taifa wakigombea nafasi 10.
 
Nikiwa natazama TBC kipindi mwaka mmoja wa awamu ya sita. Moja kati ya mafanikio ni kupatiwa suluhisho kwa kero za Muungano na kero hiyo ni " Ajira za Zanzibar kwenye taasisi na wizara za muungano" Hii kero ndani ya mwaka mmoja imeshapatiwa suluhisho. Hii kero imepatiwa suluhisho ndani ya muda mfupi mno. Hatujasikia tume ikiundwa wala ikiwasilisha mapendekezo yake. Nani hasa huwa wanakaa na kuamua haya?
Hivi kero za Muungano ni upande wa Zanzibar tu?
Huko kuna kitengo maalumu kwa Kazi hiyo,kama una kinyongo jifie
 
Nikiwa natazama TBC kipindi mwaka mmoja wa awamu ya sita. Moja kati ya mafanikio ni kupatiwa suluhisho kwa kero za Muungano na kero hiyo ni " Ajira za Zanzibar kwenye taasisi na wizara za muungano" Hii kero ndani ya mwaka mmoja imeshapatiwa suluhisho. Hii kero imepatiwa suluhisho ndani ya muda mfupi mno. Hatujasikia tume ikiundwa wala ikiwasilisha mapendekezo yake. Nani hasa huwa wanakaa na kuamua haya?
Hivi kero za Muungano ni upande wa Zanzibar tu?
Kwani nchi ya Tanganyika inatajwa katika katiba kama sehemu ya JMT? Je! Ni nani hasa kwa hivi sasa anaweza kuzungumzia maslahi ya Tanganyika ama Watanganyika!?

Wenzetu licha ya kuitwa Tanzania Visiwani walibaki na hadhi ya utambulisho wa nchi yao ya Zanzibar, huku wakibaki na Rais wao, bendera yao, wimbo wao wa taifa na vitu vingine muhimu vyenye kulitambulishwa. Tulipokubali kupoteza hadhi ya kutambulika kama Tanganyika ndani ya JMT, basi tukubali kuwa hakuna kero za kitu kinachoitwa Tanganyika pekee.

Tanganyika imebakia na kumbukumbu yake ya kupata uhuru, ijapokuwa hata katika maadhimisho ya siku hii, jina hili linakwepa hata kutajwa. Rais wa JMT SSH ni Mzanzibari, na Rais Mwinyi Jr naye hali kadhalika.

Sasa ni kipi ambacho kinashindikana pale fursa hii ya kipekee inapotokea kutatua kwa muda mfupi kero za wananchi wa Zanzibar!
 
Nilishangaa sana hata TBC siku ya Uhuru Tanganyika wanaandika " SHEREHE ZA UHURU"

Wanakwepa neno Tanganyika.
 
Back
Top Bottom