KERO Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa hatujalipwa fedha za kujikimu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, tukiwa miongoni mwa waajiriwa wapya wa mwaka 2026 (kuanzia mwezi Januari) katika kada mbalimbali zikiwemo ualimu, afya, ustawi wa jamii, kilimo na maendeleo.

Changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni kutolipwa fedha za kujikimu hadi sasa. Jambo linalotushtua zaidi ni kukosekana kwa majibu ya kueleweka kutoka kwa uongozi wa halmashauri, ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi na wakuu wa idara husika.

Kila tunapofuatilia madai yetu, tunaambiwa kuwa huenda tusilipwe ndani ya mwaka huu, na wengine tunaelezwa kuwa malipo yanaweza kuchelewa hadi hata miaka miwili, ilhali tunaendelea kufanya kazi na kupokea mshahara wa kawaida.

Hali hii inatuweka katika mazingira magumu sana ya maisha, hasa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. Wengi wetu tunafanya kazi katika maeneo ya vijijini, ambapo hata kufuatilia madai haya kunahitaji gharama kubwa za usafiri kwenda mjini, kiasi cha kutumia fedha nyingi bila mafanikio yoyote.

Tunaomba mamlaka husika, ikiwemo uongozi wa juu wa Serikali, kulifuatilia kwa karibu suala hili ili kuhakikisha watumishi wapya wanapata haki zao za msingi kwa wakati, na kuondoa changamoto hii inayotuathiri kiuchumi na kisaikolojia.
 
Kada ya UALIMU=CCM ,ni ileile...kufeni njaa kabisa...
 
Tunaomba mamlaka husika, ikiwemo uongozi wa juu wa Serikali, kulifuatilia kwa karibu suala hili ili kuhakikisha watumishi wapya wanapata haki zao za msingi kwa wakati, na kuondoa changamoto hii inayotuathiri kiuchumi na kisaikolojia.
Endeleeni kupoteza muda, haki haiombwi inadaiwa. Siku hizi kesi za kazi pale CMA zinafunguliwa online, eutatuzi.cma.go.tz,
 
Sisi ni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, tukiwa miongoni mwa waajiriwa wapya wa mwaka 2026 (kuanzia mwezi Januari) katika kada mbalimbali zikiwemo ualimu, afya, ustawi wa jamii, kilimo na maendeleo.

Changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni kutolipwa fedha za kujikimu hadi sasa. Jambo linalotushtua zaidi ni kukosekana kwa majibu ya kueleweka kutoka kwa uongozi wa halmashauri, ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi na wakuu wa idara husika.

Kila tunapofuatilia madai yetu, tunaambiwa kuwa huenda tusilipwe ndani ya mwaka huu, na wengine tunaelezwa kuwa malipo yanaweza kuchelewa hadi hata miaka miwili, ilhali tunaendelea kufanya kazi na kupokea mshahara wa kawaida.

Hali hii inatuweka katika mazingira magumu sana ya maisha, hasa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. Wengi wetu tunafanya kazi katika maeneo ya vijijini, ambapo hata kufuatilia madai haya kunahitaji gharama kubwa za usafiri kwenda mjini, kiasi cha kutumia fedha nyingi bila mafanikio yoyote.

Tunaomba mamlaka husika, ikiwemo uongozi wa juu wa Serikali, kulifuatilia kwa karibu suala hili ili kuhakikisha watumishi wapya wanapata haki zao za msingi kwa wakati, na kuondoa changamoto hii inayotuathiri kiuchumi na kisaikolojia.
Hapo kwanza ncheke. Huku jamii forum kumepigwa pin ulivyokuja huku unajua wewe. Unazani hii taarifa itawafikia walengwa. Ushauri tafuta njia mpya ya ku lobby tumia account za watu maarufu watumie pm hata watano mmoja wapo ataipost tu
 
Back
Top Bottom