Kero: Wasafirishaji wa mizigo kupakilia mizigo kwenye makazi ya watu Kariakoo

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
11,038
5,259
Msingi wa shida zote ni serikali za mitaa, na hizi karibu zote zilipita bila kupingwa,

Sasa hapa Kariakoo misheni kota yaani utafikiri uko sijui kwenye viwanda vya kutengezea malori, yaani mitaa yote kuanzia Ndanda hadi Muheza, Narun'gombe, Magira, Masasi na Aggrey street hapajulikani ni jiji, mji, kijiji au porini?!

Katikati ya nyumba za kuishi na fremu za biashara kuna wasafirishaji wanapanga mizigo ya kusafirisha hadi kuziba barabara na matumizi mengine ya hizo barabara.

Na hili limeripotiwa serikali ya mtaa wa misheni kota ofisi yao ikiwepo pale Tandamti kwenye container bila hatua zozote kuchukuliwa.

Na hata jiji habari zipo na diwani anajua na mbunge pia mheshimiwa analijua na kuliona hili ila wapo kimyaaaaa.

Sasa nauliza wale waliopeleka magari yao jangwani ni wajinga? Kwanini kiburi cha hawa wanaolazimisha kubebea mizigo kwenye makazi ya watu? Jiji halina mipango miji? Au ndio mali ya wakubwa?

Najua magu ungewepo ungeshuhulikia hili ila pia wewe ndio uliwaleta hawa wasimamizi wabovu wa serikali
#ondoamalorikariakoo
 
Mida hii imepita gari hapa inawatangazia bodaboda kuondoka Kariakoo. Huu ni uonevu wa hali ya juu sana na Mungu anawaona mujue.

Yaani bodaboda zilete foleni na sio malori?

#ondoamalorikariakoo
 
Yaani mamlaka angaieni hili ni shida kupita maelezo wakaazi wanataabika, wapita njia wanataabika, kisa malori tu! Imekuwa kama hakuna serikali?

Basi waruhusuni wote warudi kuliko kuwa double standard
 
Mida hii imepita gari hapa inawatangazia bodaboda kuondoka Kariakoo. Huu ni uonevu wa hali ya juu sana na Mungu anawaona mujue.

Yaani bodaboda zilete foleni na sio malori?

#ondoamalorikariakoo
Heeh, sasa boda zinatokaje kariakoo?
 
Heeh, sasa boda zinatokaje kariakoo?

Kwamba hakuna kijiwe kariakoo, Vijiwe vyote viwe nje ukihitaji huduma upige simu aje,
ila malori ruhsa kuziba barabara yaani hata sijui wenye malori wanatoa kiasi gani kwani ile gari yenye namba sm... 1.3... Inapita na kukusanya mchana kweupe,
yaani hauo maeneo niliyoainisha yote kuanzia saa mbili asubuhi hakupitiki mpaka saa tano usiku ni kama vile ni yard ya malori
 
interesting kwa kweli
 
Ukiongelea suala la mipango miji,

Kwasasa,
kariakoo hapakutakiwa Tena kua makazi ya watu, Lile Ni soko. Tena la kimataifa.

Wazaramo mnatuangusha Sana
 
Kua soko sio shida,
Shida ni malori yanavyochafua kariakoo
Labda kama Unakusudia soko la malori,
Ila kama ni soko la bidhaa mbali mbali hilo lipo na linafanyika tangu enzi na enzi ila sasa malori yameharibu kariakoo

Barabara mpya mpya zinajengwa na serikali lakini zinageuka parking za magari, njia inabaki kuwa moja ni shida kwa kweli
 
Ukiongelea suala la mipango miji,

Kwasasa,
kariakoo hapakutakiwa Tena kua makazi ya watu, Lile Ni soko. Tena la kimataifa.

Wazaramo mnatuangusha Sana
Kua soko si shida ,
Shida ni malori,
Tangu enzi na enzi kariakoo ni soko na watu wanaishi huko humo na mambo yanakwenda,
Malori yanaziba na kuharibu barabara jaribu kuelewa point
 
Msingi wa shida zote ni serikali za mitaa, na hizi karibu zote zilipita bila kupingwa,

Sasa hapa Kariakoo misheni kota yaani utafikiri uko sijui kwenye viwanda vya kutengezea malori, yaani mitaa yote kuanzia Ndanda hadi Muheza, Narun'gombe, Magira, Masasi na Aggrey street hapajulikani ni jiji, mji, kijiji au porini?!

Katikati ya nyumba za kuishi na fremu za biashara kuna wasafirishaji wanapanga mizigo ya kusafirisha hadi kuziba barabara na matumizi mengine ya hizo barabara.

Na hili limeripotiwa serikali ya mtaa wa misheni kota ofisi yao ikiwepo pale Tandamti kwenye container bila hatua zozote kuchukuliwa.

Na hata jiji habari zipo na diwani anajua na mbunge pia mheshimiwa analijua na kuliona hili ila wapo kimyaaaaa.

Sasa nauliza wale waliopeleka magari yao jangwani ni wajinga? Kwanini kiburi cha hawa wanaolazimisha kubebea mizigo kwenye makazi ya watu? Jiji halina mipango miji? Au ndio mali ya wakubwa?

Najua magu ungewepo ungeshuhulikia hili ila pia wewe ndio uliwaleta hawa wasimamizi wabovu wa serikali
#ondoamalorikariakoo
Kwahiyo wakati wa Magu alikuwepo unamaanisha?!
 
Back
Top Bottom