sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,038
Binafsi niweke wazi kabisa kwamba napenda kuishi kijamii na wala sinaga tatizo na misiba ila hali ya mbeya imezidi sana
Sasa kwa huku Mbeya hali ya misiba imekuwa tofauti sana, watu hawajali kushiriki kwako msibani hawakwambii hata msiba ulipo mpaka uwauilze na hata hawajali ukaribu wako na mfiwa, kinachopewa kipaumbele ni mchango wako pesa, na huna budi inabidi uchange tu kukwepa lawama kwamba hauna ushirikiano kwenye jamii.
Kisingizio huwa ni pale wanakwambia inakubidi uchangie lasivyo siku ukipata msiba watakususia..Huu ni upuuzi mkubwa, hivi mtu ninayemchangia ambaye hata sijaenda kwenye mazishi yake na hatujuani kweli ndio nitegemee awe tegemeo kuu kwenye msiba wangu, hapana! Watu naowategemea kwenye msiba wangu ni wale ambao hata wao wakipata misiba huwa inailazimu kupangua ratiba yangu ili niende kuhudhuria msibani, nazungumzia wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wa karibu, na hata kama ni mtu wa sokoni basi akiwa ni mtu wangubwa karibu ama rafiki wala sihitaji kupitishiwa daftari, ntaenda kuhudhuria msiba au ntampelekea hela mkono kwa mkono au kwa mpesa nikiwa mbali.
Huku maofisini kuna unafuu maana waajiriwa wamechanganyika, Shughuli ipo mitaa yenye wazawa wengi wa Mbeya, maderva wa bajaji, kwenye frem za maduka, n.k
Nina frem yangu pale soko kuu la Mwanjelwa nimemweka binti yani kwa wiki ni mara 4, niliwahi pia kushinda hapo na kweli nikajiridhisha, wanakuja watu wa sokoni pale pale (ni wazawa wa Mbeya) kama watatu moja kashika picha, mwengine peni na daftari mwengine anawasindikiza, inabidi uchangie tu.
Na bora ingekuwa ni mtu aliyefariki ni mwenye frem, yani unakuta mtu aliyefariki ni ndugu yake mwenye frem na kama mnavyojua wenzetu Wanyakyusa ni kawaida kuwa na ndugu hata 150.
Kuna baadhi ya misiba nimeshuhudia watu wanaingia hadi barabarani wanaomba michango huku msiba unaendelea, hasa misina ya Makunguru, Ilolo, Isanga, n.k.
Pia kwa upande wa bajaji naonaga sana hii, pale pale Mwanjelwa kuna viongozi wao kila siku lazima kuwe na mchango wa msiba.
Hii ni kero sasa.
Hitumisho:michango ifanywe kwa wahusika wenyewe sio kila mtu ahusike kwenye msiba usiomuhusu...