Misiba ina gharama kubwa kuliko ankara za tiba

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Msibametrics.

Siku hizi jamii inahamasika kwa wingi na kasi kubwa kuchangia misiba kuliko kuchangia matibabu (ugonjwa).

Hii ni kwa sababu misiba ni fursa ya kibiashara na watu wanasaka fursa.

Fursa za kwenye msiba:-
1. Upishi.
2. Maji.
3. Umeme (wiring).
4. Viti, meza, turubai, maliwato ya kuhamishika.
5. Nishati ya kuni/mkaa.
6. Kukodi vyombo vya chakula.
7. Muziki.
8. MC na DJ.
9. Jeneza.
10. Magari na ndege.
11. Casket Lowering Belt (Mkanda wa kushusha jeneza kaburini).
12. Camera.
13. Catering staffs.
14. Wachimba na wajenga kaburi.
15. Wajenga nyumba (msonge) wa marehemu.
16. Watumishi wa kulipwa (Paid Pastors (Freelancers)).
17. Waliaji wa kukodi.
18. Mifugo na nafaka.
19. Vinywaji.
20. Guest house, boarding and lodging.
21. Mapambo.
22. Mashada na maua.
23. Gharama za Mochuari.
24. Tozo za RITA.
25. Gharama za Mashahidi wa Mirathi.
26. Printers wa fulana (T-shirts).
27. Studio ya ku-develop picha kubwa.
28. Washona (wauzaji) sare za dera.
29. Gari la Polisi lenye king'ora kusafisha njia.
30. Vijana wa itifaki ya misiba wanaovalia suti nyeusi kubeba jeneza.
31. Matangazo ya vifo redioni.
32. Wapigaji (Mafisadi wa rambirambi).
33. Mnaniachaje watu wa mjini najuwa sasa mnaondoka kurejea mjini.

Fursa za Ugonjwa:-
1. Daktari.
2. Muuguzi.
3. Fundi Maabara.
4. Mfamasia.
Full stop.

Msiba una fursa 33 za kutengeneza faida.

Msiba una fursa zaidi ya 50 za ajira za msibani tu.

Ugonjwa una fursa 4 tu za ajira na za kutengeneza faida.

NB.
Watoa rambirambi lazima wawe wengi kuliko wachangia ankara za matibabu.

Muhtasari/Summary.

Msiba una fursa 33 za kutengeneza ela na ajira zaidi ya 50 za papo kwa hapo na za kudumu kwenye vikundi vya kuhudumia misiba.

Ugonjwa una fursa 4 tu za kutengeneza ela na ajira mpya 0.

Watu wanapenda kwenye fursa nyingi kuliko kwenye fursa chache.

Hivyo inabidi wachangia misiba (rambirambi) wawe wengi kuliko wachangia matibabu.

Ugonjwa una Bima msiba hauna. Yale maandishi yanayopambwa kwa maua freshi herufi 1 tu ni Tshs.50,000 bei ya punguzo.

Wachangia misiba wana uhakika wa kujirudishia michango yao na faida kubwa juu lakini wachangia matibabu hawawezi kurudisha hata senti 0 (kiendacho kwa tabibu na nesi hakirudi).

Hivyo watu wanakwepa kuchangia matibabu ya mgonjwa ili kwamba asipone ili wapate zile fursa 33 za msiba ambazo zina ela ndefu ambazo hazina auditing (ukaguzi) wala kuvunja Kamati.

Asomaye na afahamu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

Tujadili.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha,
Juzi tu nilipita sehemu nikakuta msiba una bajeti ya 7m
Japo mimi sio muslim ila kwenye suala la maziko nawakubali sana hawa wenzetu!
Unakufa unazikwa fasta kama kuna michango iwafae walobaki mana kuna maisha baada ya msiba!
Ile style ni nzuri sana,
Halafu kutokuwa na jeneza nayo inasave cost sanaaa,
Siku hizi majeneza ya 700+ ndio watu wanazikia, + gharama za misosi na vitu ka hivyo,
Msiba cost siku hiI ni 3M -5M, ina depend na gharama za usafiri, eg mtu kafia mwanza na inabidi azikwe Iringa, au kafia Dar akazikwe Bukoba
 
Msiba na gharama una influence kubwa ya hadhi ya marehem au hadhi ya familia yake. Hata kwa Waislam, kwenye msiba wa tajiri gharama zipo juu kuliko masikini, ingawa bado msiba wa tajiri wa Kiislam utakuwa na gharama nafuu kuliko msiba wa tajiri wa Kikristo.

Lakini kusema ukweli, msiba wa Kikristo ni biashara.
Kuna mwanangu anakodisha viti, hata siku ile ya supu ya Yanga alihusika.....ntamfuata anipe ABCD ya biashara hii. Unaweza kukuta kila week una laki kadhaa za kukodisha tu turubai na viti.
 
Umenikumbusha,
Juzi tu nilipita sehemu nikakuta msiba una bajeti ya 7m
Japo mimi sio muslim ila kwenye suala la maziko nawakubali sana hawa wenzetu!
Unakufa unazikwa fasta kama kuna michango iwafae walobaki mana kuna maisha baada ya msiba!
Ipo siku hizi misiba yenye bajeti sawa au hata zaidi ya harusi.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Everything hapa duniani is all about trading, hata wazazi wako kukuzaa ama wewe kuzaa unafanya trading. Ngoja uliiowazaa wasimit your expectations aka profit in terms socially, materialistically and emotionally utajuta kuzaa ama kuzaliwa.

Kuwa mvuta bangi na mpiga debe mzazi hatakuwa anakutambulisha Kama wewe Ni mwanae
 
Ile style ni nzuri sana,
Halafu kutokuwa na jeneza nayo inasave cost sanaaa,
Siku hizi majeneza ya 700+ ndio watu wanazikia, + gharama za misosi na vitu ka hivyo,
Msiba cost siku hiI ni 3M -5M, ina depend na gharama za usafiri, eg mtu kafia mwanza na inabidi azikwe Iringa, au kafia Dar akazikwe Bukoba
Kila wafiwa wa imani zinazotumia jeneza wanataka kaburi kama la Magufuli la ku-slide grave-top (mfuniko wa kaburi) Baghosha!

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Everything hapa duniani is all about trading,hata wazazi wako kukuzaa ama wewe kuzaa unafanya trading.ngoja uliiowazaa wasimit your expectations aka profit in terms socially, materialistically and emotionally utajuta kuzaa ama kuzaliwa.kuwa mvuta bangi na mpiga debe mzazi hhatakuwa anakutambulisha Kama wewe Ni mwanae
Na ukiwa mvuta bangi ya Nyamwaga au Muriba ambaye unaleta chochote cha kufanya familia izunguke meza mara 2 kutwa pia bado atakukana kwa kigezo cha uvuta bangi ya Genkuru Keribo?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha,
Juzi tu nilipita sehemu nikakuta msiba una bajeti ya 7m
Japo mimi sio muslim ila kwenye suala la maziko nawakubali sana hawa wenzetu!
Unakufa unazikwa fasta kama kuna michango iwafae walobaki mana kuna maisha baada ya msiba!
Mkuu swala la msiba watu wengi wanafanya kuiga hata kama hawajiwezi mimi najishughulisha na moja ya kazi za misibani unakuta familia inakuja inataka vifaa kadhaa kama msiba wa fulani ukiwatajia bei wanaruka kama chura sasa unawashauri tendo la kusitiri mwili lisifanye mkafarakana kama hamna uwezo ila watu hawasikii kuna changamoto sana muda mwingine inabidi utoe sadaka tu na uombe Mungu vifaa virudi salama maana unaweza dai na usilipwe bora utoe kwa moyo. Ipo misiba bajeti yake ni 13 mpka 16m na watu hawahangaiki ila kuna wenzangu na mimi bajeti ya 3m inawatoa jasho mpka wanagombana ndugu kwa ndugu
 
uchumi lazima ukue hamna namna, ukiamua kuzikwa na bajeti ya laki ni wewe tu, ila kama wewe ni mtu wa watu lazima wakuzike vizuri, wanamshukuru Mungu kwa kuwa uliishi, pia wanapata nafasi ya kukumbuka kuwa ipo siku nao watapotea
Mura, kwahiyo misiba ya Kiislamu haina economic incentives? Haikuzi uchumi?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu swala la msiba watu wengi wanafanya kuiga hata kama hawajiwezi mimi najishughulisha na moja ya kazi za misibani unakuta familia inakuja inataka vifaa kadhaa kama msiba wa fulani ukiwatajia bei wanaruka kama chura sasa unawashauri tendo la kusitiri mwili lisifanye mkafarakana kama hamna uwezo ila watu hawasikii kuna changamoto sana muda mwingine inabidi utoe sadaka tu na uombe Mungu vifaa virudi salama maana unaweza dai na usilipwe bora utoe kwa moyo. Ipo misiba bajeti yake ni 13 mpka 16m na watu hawahangaiki ila kuna wenzangu na mimi bajeti ya 3m inawatoa jasho mpka wanagombana ndugu kwa ndugu
Umetema nyongo mkuu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mbona hizo fursa za msiba nyingi ulizoorodhesha hazina Umuhimu wala ulazima kufanyika kwenye siku ya msiba.

Lengo la msiba ni kuzika. Mengine ni hiari na wala sio lazima kufanyika.

Tukirudi kwenye tiba ni lazima Daktari, nesi, famasia wawajibike pia gharama ni lazima zifanyike. Otherwise labda mgonjwa atokee kwenye familia masikini
 
Back
Top Bottom