Pole sana mkuu. Watangazaji wa redio wa siku hizi hawana maadili. Watangazaji walikuwa zamani enzi za RTD. Zamani usingeweza kumsikia mtangazji anacheka, kukohoa au kuongea ujinga ujinga akiwa studo. Siku hizi watangazaji wanaochekacheka ndio wanaonekana wajanja. Dunia imepinduka kichwa chini, miguu juu!
Habari wanaJF?
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Kwa mujibu wa utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni, usikilizaji wa redio na utazamaji wa TV umepungua sana miongoni mwa wafuatiliaji wa habari. Hili halijatokea kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu ya kupungua usahihi wa taarifa na ubora wa watangazaji. Sote ni mashahidi jinsi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Voice of Kenya (VoK) zilivyokuwa na watangazaji nguli ambao huchoki kuwasikiliza.
Watangazaji wengi wa redio na TV zinazochipukia kama uyoga hapa nchini wanakera mno kwa utangazaji...