Mkurugenzi wa vipindi Radio One, soma hapa na uchukue hatua mara moja ili msiendelee kupoteza soko la wasikilizaji.

Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
656
483
Tangu mwaka huu uanze naona kama ma-DJ au watangazaji au waandaa vipindi radio one wameamua kutufanya sisi washabiki wao kama mazuzu. Kumekuwa na "mixing" kama nne ambazo kila siku zinatumika kutoa burudani kiasi mpaka sasa zimekuwa ni kero kwa wasikilizaji. Mara nyingi kuaanzia saa 2:15 hadi saa 3 kamili usiku (siku za jumatatu hadi ijumaa), au saa 3 usiku mpaka saa 4 usiku jumanne na jumatano au usiku wa saa 7 mpaka saa 11 alfajiri ndipo moja ya "mixing" hizi hutumika kwaajiri ya kuburudisha. Muda wa "mixing" moja ni kati ya dakika 45 mpaka dakika 90 (saa moja na nusu), hivyo anayekuwa zamu huweka mixing mojawapo na kuacha hiyo mpaka mwisho wa kipindi. Imefika mahali mpaka nyimbo zimekinai maana ni kwa miezi sita mfululizo ni nyimbo hizohizo. Tafadhari mkurugenzi wa vipindi radio one fuatilia hili na utusaidie kurejesha raha ya kusikiliza radio yetu pendwa. Mixing zenyewe ni kama ifuatavyo

Mixing A: Zouk/rhumba -mara nyingi huchezwa jumanne, nyimbo zake ni
1. Cocola - tshela mwana
2. My love Elizabeth - kanda bongoman
3. Marina - sam mangwana
4. Bane - oliver ngoma
5. Muzina - tabuley
6. Karibu yangu - tshela mwana
7. Double double - nyiboma
8. Nakusema sema - madilu system
9. ....onaaa ok are you ready now ?(sijaujua)
10. Heshima kwanza

Mixing B: Bolingo - mara nyingi huchezwa Jumatano, nyimbo zake ni
1. Kalayi boieng - wenge musica bcbg
2. Julia - quarter latin & koffi olomide
3. Chorus ya mbongo - mayaula mayoni
4. Chorus kofi olomide - musa musa ee ahaa
5. Chorus ya wimbo wa Voyage mboso wenge musica bcbg
6. Chorus from dede album zaiko langa langa
7. Chorus ya dandi victoria elyson
8. Chorus kofi olomide demokrasia
9. Chorus ya filandu wenge musica bcbg
10. Maya nyiboma
11.Chorus wimbo wa dede zaiko langa langa
12. Chorus sijaijua
13. Chorus fredynelson extra musica

Mixing C: Bongo fleva,mara nyingi huchezwa Alhamisi, nyimbo zake
1. Niite basi - Joselin
2. Dunia inamambo - Afande sele & Watu poli
3. Naja - Squizer ft Juma nature
4. Yule - A Y
5. Mapozi - Mr Blue
6. Nje ndani - Gangwe mob
7. Kama - Mike T
8. - Jebby
9. Nitoke vipi - Bwana misosi ft hard mad
10. Nimechezea bahati - Man x ft dully sykes
11. Maria - Abby skillz ft blue & ali kiba
12. Huyu na yule - Fid Q
13. Mtazamo - Afande sele ft prof j & solo

Live sebene (mara nyingi usiku saa 7 - 9)
1. Chorus from - Koffi olomide
2. Chorus zenith show 1999 - wenge maison mere & werason
3.
 
Back
Top Bottom