1. Tanesco and water authority.
i. Service charge mnatukata kwasababu gani wakati tunanunua luku kwa njia ya m-pesa/tigo-p/airtel-m. ii. Kwanini mita za luku mnatukata kila mwezi wakati sisi tunahitaji kununua umeme wala si kununua mashine zenu za luku?. Mm huwa naona kero sana ninapokatwa pesa bila mpangilio/ mnakula jasho langu bila kulifanyia kazi
2. Sumatra na ujinga wao barabarani.
a). Wananchi wanachajiwa nauli kubwa kupindukia ktk safari fupi kwenye barabara ya rami, mfano; ukitoka mwanza to bunda nauli unachajiwa elfu 8, mwanza to tarime nauli unatozwa elfu 10, mwanza to musoma unatozwa elfu 8-10, (hii ni kwa mabasi yote yaani daraja la kawaida na yale mengine). Wabandikieni nauli mbele ya magari abiria wenu, mfano pale dodoma nmeona kuna basi zinabandikwa nauli abiria anakuwa anajua anachoenda kukilipa ktk safari yake.
b). traffic anapokagua gari anakuta kuna kosa la gari kukosa mikanda ya kwenye siti n.k, inatokea traffic anaiandikia gari husika faini akiisha maliza anairuhusu gari kuendelea na safari, likitokea tatizo kwenye gari nani atalaumiwa?. huwa inanishangaza sana, traffic wa Tanzania hawawatakii mema wananchi bali hutetea pesa tu. Ina kera sana; mm huwa naona ni bora abiria wakapewa usafiri mwingine na sio kuruhusu kuendelea na safari wakiwa kwenye gari ile ile yenye kasoro.
Pongezi: Watendaji wa serikalini naona wengi wenu mmeanza kuwa na hamu ya kutekeleza majukumu yenu mnapokuwa kazini. nampongeza mheshimiwa aliyeko juu, halmashauri X kila mtu yuko bize na hawaruhusiwi kuzurula nje ya ofisi pasipo sababu, naona kila mtu anaulizia kazi ya kufanya