Kero Kubwa za Watanzania - Changia

Kero Kubwa za Watanzania - Changia

(Naomba mods wa stick uzi huu kwa ustawi wa taifa letu)

Naamini timu nzima ya #WachapaKazi wa Magufuli wapo tayari kuchukua kero zetu #Watanzania na kuzifanyia kazi bila kusita.

Hivyo basi, tuweke kero za msingi hapa.

Mimi naanza na hizi;

1. Mpasuko unaosababishwa na tofauti za kiitikadi.
- Tuweke Utanzania mbele kuliko itikadi.

2. Ufisadi wa kutisha
- viporo vyote vya ufisadi vifanyiwe kazi na mfumo uimarishwe.

3. Bei Kubwa ya Umeme
- Mikataba ya umeme ipitiwe.

4. Miundombinu
- Sehemu kubwa ya Tanzania bado haina miundombinu ya barabara, maji, umeme nk.

5. Mazingira
- Mazingira yetu yanaathiriwa sana na kelele za muziki wa ma bar na vilabu, uchafu, ujenzi holela nk.

6. Mfumo wa Uchumi
- Uchumi wetu umeshikiliwa na unanufaisha tabaka fulani la wachache na wageni kutokana na serikali kutosimamia vyema fursa zinazojitokeza.

7. Madawa ya kulevya
- Madawa ya kulevya yanaua nguvu kazi ya taifa letu.

8. (Endelea ........ )
mabaa na kumbi za starehe kwenye makazi ya watu.
 
Kero kubwa na pale Baadhi ya Matangazo ya ajira kuweka vigezo vya waombaji kuwa ni lazima wawe wamesajiriwa na bodi za taaluma zao . Kuweka sifa ya aina hiyo kwa mwombaji ndiyo KULAZIMISHWA KWENYEWE HUKO (INDIRECT). Mwombaji Inamlazimu ajisajiri na bodi ili angalau aweze kukidhi sifa hiyo mojawapo. Ajira zenyewe ni ngumu kuzipata mtu anakaa nyumbani miaka zaidi ya 3 hajapata kazi , halafu leo hii tangazo la kazi linamlazimisha eti lazima awe amesajiliwa na bodi.

Kusajiliwa na bodi ni jambo zuri sana ,lakin nadhani ingekuwa vizuri sana wangewasisitizia zaidi waliopata kazi au waajiriwa au walioamua kujiajiri kwa kufungua kampuni (mfano consultant wa taaluma fulani) wajiunge na hizo bodi kwa sababu tayari wao wapo kwenye mfumo na hata uwezo wa kiuchumi wa kulipia ada za kila mwaka za huo usajili wanao.
Mtu hana kipato cha uhakika halafu unamwongezea gharama kwa kumlazimisha ajisajili na kulipia ada ya kila mwaka hii nayo ni kero. Ananufaika vipi na huu usajiri nje ya ajira ikiwa hata hizo semina hata hapewi mwaliko wake. Hizo semina ananufaika nazo akiwa chuoni tu, akimaliza chuo basi hizo semina wala hatumiwi mwaliko wake.

WAHUSIKA LIANGALIENI HILI MSIFURAHIE TU KUKUSANYA ADA ZA WASAJILIWA. NIA YENU NZURI SANA, KUJIUNGA NA BODI NI KUZURI KUNAONGEZA THAMANI YA TAALUMA ILA MNGEWEKA MKAZO ZAIDI KWA WAAJIRIWA AU IWE MARA TU BAADA YA KUAJIRIWA.
 
(Naomba mods wa stick uzi huu kwa ustawi wa taifa letu)

Naamini timu nzima ya #WachapaKazi wa Magufuli wapo tayari kuchukua kero zetu #Watanzania na kuzifanyia kazi bila kusita.

Hivyo basi, tuweke kero za msingi hapa.

Mimi naanza na hizi;

1. Mpasuko unaosababishwa na tofauti za kiitikadi.
- Tuweke Utanzania mbele kuliko itikadi.

2. Ufisadi wa kutisha
- viporo vyote vya ufisadi vifanyiwe kazi na mfumo uimarishwe.

3. Bei Kubwa ya Umeme
- Mikataba ya umeme ipitiwe.

4. Miundombinu
- Sehemu kubwa ya Tanzania bado haina miundombinu ya barabara, maji, umeme nk.

5. Mazingira
- Mazingira yetu yanaathiriwa sana na kelele za muziki wa ma bar na vilabu, uchafu, ujenzi holela nk.

6. Mfumo wa Uchumi
- Uchumi wetu umeshikiliwa na unanufaisha tabaka fulani la wachache na wageni kutokana na serikali kutosimamia vyema fursa zinazojitokeza.

7. Madawa ya kulevya
- Madawa ya kulevya yanaua nguvu kazi ya taifa letu.

8. (Endelea ........ )

9. Madeni, Serikali yanayodaiwa na Kampuni za Wazawa, Serikali inatakiwa kulipa madeni ya ndani, Sijui hizi Kampuni za Wazawa watalipaje Mishahara ya Wafanyakazi wake na Uendeshaji wa Kampuni zao.
10. Urasimu Tender zinazotangazwa za Serikali. Kampuni za Wazawa zipewe Kipaumbele, Utakuta Kampuni inayoshinda Tender ni nyingine na inayopewa Tender au inayotangazwa mshindi ni nyingine.
11. Urasimu kwenye Ofisi na Taasisi za Serikali.
 
HUDUMA KWA WATANZANIA KWENYE BALOZI ZETU ZA NJE YA NCHI NI TATIZO

Mfano ni ubalozi wa Uingereza: Customer service ni tatizo kuanzia mtu anayepokea simu pale reception, eneo la kuomba vibali vya kusafiria / kurenew passport n.k.

Nilibahatika kuwasiliana na watanzania wachache kuhusu zoezi la kuomba passort mpya ubalozi wa Uingereza, wengi wanashauri ni bora uchukue likizo ufanye maombi Tanzania kuliko kutuma maombi yako ubalozini. Sababu kubwa hakuna ushirikiano mzuri na wafanyakazi wa pale, pili passport zinachukua muda mrefu kutolewa.
 
Finger print za passport pale airport pia ni kero kubwa sana na usumbufu.

Wenzetu nchi zilizo endelea mbona hawachukuliwi fingers print kwenye passport zao or immigration control?
 
Kodi ya mapato inayotozwa kwenye mishahara ya watumishi wa umma (PAYE) ni kubwa mno. Wenyewe (watawala) utawasikia, "watumishi wanatozwa kodi ya 11%. Huu ni uongo kwani ukipiga mahesabu utagundua kwamba kiasi cha kodi ni zaidi ya 16%. Kwa mfano, mtumishi anayelipwa 'basic salary' kiasi cha Tshs. 940, 000, anatozwa kodi ya Tshs. 145,340. Hebu kokotoa hiyo kodi uone kama ni 11% au ni zaidi ya hapo. Lakini hata wangetoza hiyo 11% bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa mtumishi wa umma ambaye mshahara wake ni wa 'kijungujiko'
 
Bei gani wametangaza.?
700, 1200 hili lisimu langu limegoma Kuleta kapicha kwenye mchangamanuo....
wa hizi nauli japo Nadhan bado Hawajjapitisha ndo proposal mh. imani umezalilisha psychological.. loh
 
Lingine swala la wahamiaji haramu. Tunako elekea vijana watakosa kazi kabisa. Haiwezekan mwekezaji anakuja alafu anaajiri watu wote toka nje ya nchi. Wakati anaomba kuwekeza anakuja na sela nyingi tukijua kuwa ni mtu mwema. Kumbe ametumwa kwao aje awatafutie rai wengine toka huko atokako nafasi za kazi. Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa. Leo hii huwezi kufanya kazi nchi za wenzetu kama si rai. Najua watajitetea sana kuwa ni ma expart. Lakin wachunguzen sana maana washajulia Tanzania kuwa ni shamba la bibi
 
mabaa na kumbi za starehe kwenye makazi ya watu.
sio bar tu na makanisa Ya Ajabu ajabu Wanakuwa watu 2 wameweka yale maspika ya disco wanawasha kwa sauti mpaka mwisho aghrrrrr nampenda Mungu lakini kuna wakati W a Mungu na wakati unabidi Tufanye kazi
 
Nadhani kukosa mtaji wa wazo zuri la niashara ambalo linaweza tengeneza ajira kwako na kwa wengine wengi ni kero kubwa sana kulilo kukosa ajira, iwepo mifumo ya kujenga mawazo kuwa biashara
 
Back
Top Bottom