Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,178
Naamini timu nzima ya #WachapaKazi wa Magufuli wapo tayari kuchukua kero zetu #Watanzania na kuzifanyia kazi bila kusita.
Hivyo basi, tuweke kero za msingi hapa.
Mimi naanza na hizi;
1. Mpasuko unaosababishwa na tofauti za kiitikadi.
- Mbali ya wananchi, kuna viongozi wakubwa kabisa ambao hawajitambui. Mpaka leo bado wapo tayari kuona taifa linadidimia ili vyama vyao vistawi. Wapo tayari kutetea ufisadi wakidhani wanalinda chama. Wapo tayari kuminya uhuru wa maoni na kupata habari wakidhani wanalinda chama. Wapo tayari kukwamisha miradi ya maendeleo sehemu zenye itikadi tofauti wakidhani wanalinda chama. Wameweka maslahi ya chama kabla ya maslahi ya taifa.
- Ni wakati wa kuweka Utanzania mbele kuliko itikadi, tumeachwa !.
2. Ufisadi wa kutisha
- viporo vyote vya ufisadi vifanyiwe kazi na mfumo uimarishwe.
3. Bei Kubwa ya Umeme
- Mikataba ya umeme ipitiwe.
4. Miundombinu
- Sehemu kubwa ya Tanzania bado haina miundombinu ya barabara, maji, umeme nk.
5. Mazingira
- Mazingira yetu yanaathiriwa sana na kelele za muziki wa ma bar na vilabu, uchafu, ujenzi holela nk. Kuna jamii zinateswa sana na hii kero ya kelele ambapo inafika mahali hawawezi kufanya shughuli za uzalishaji, elimu nk. Wanashinda mahakamani na kwenye maofisi ya serikali kutafuta ufumbuzi miaka nenda rudi.
- Wizara husika ikomeshe kelele za muziki kwenye makazi ya watu.
6. Mfumo wa Uchumi
- Uchumi wetu umeshikiliwa na unanufaisha tabaka fulani la wachache na wageni kutokana na serikali kutosimamia vyema fursa zinazojitokeza.
7. Madawa ya kulevya
- Madawa ya kulevya yanaua nguvu kazi ya taifa letu.
8. (Endelea ........ )

Last edited by a moderator: