Kabaridi
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 2,023
- 534
Mkuu hii minyanga'au imetuzidi kwa kupiga domo tu hakuna lingine. Laiti tukiwaweza kwenye kusimamia uchumi wetu kwa umakini in near future hawa manyang'au watakuwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki wakipigana wenyewe kwa wenyewe. Kitu wasichokijua ni kuwa tunataka usawa na kuheshimiana kwenye hiyo EAC wao wanataka wawe ndio viranja wetu wajichukulie rasilimali zetu watakavyo. Itawezekana wapi?
Tayari muna watu wa mataifa mengi wanaoishi Tz, wanaofanya biashara na wamenunua ardhi kutoka serikali ya Tz. Hata kama wageni wamenunua chini ya mpango wa Kulizi wa miaka 5 au 99, serikali inafaidika kutokana na ununuzi huo. kwa hivyo sioni haja ya kuzua matusi. Ikiwa munataka usawa katika EAC mutapata, pengine kwa usawa wa ugavi wa viti kwa wajumbe wanaowakilisha mataifa yote ya jumuia ya Afrika Mashariki. Lakini ikifikia uongozi wa EAC, lazima kuwe na uongozi mmoja. Kuna pia katiba ya EAC, tofauti sana, kwa mfano na katiba za nchi ambao ukitekelezwa vizuri, waTZ mutaridhika.