Kenyatta amtumia Lowassa kuwapasha Watanzania

Kenyatta amtumia Lowassa kuwapasha Watanzania

Nilikuwa nafuatilia mazishi ya waziri wa zamani wa serikali ya Jamhuri ya KENYA ndg.WILLIAM OLE NTIMAMA.Kwa bahati mbaya sana pamoja na kurushwa na vyombo vya habari ikiwemo LIVE coverage TV lugha iliyokuwa imetumika kwa zaidi ni lugha ya kimasai mbele ya Rais wa NCHI Mh.KENYATA.

Tafsiri niliyoipata ni kwamba kuna watu wakipewa mamlaka ndani ya nchi ni hatari sana kugawa nchi kwa misingi mbali mbalimbali ikiwemo ukabila,mf mrahisi akapewa nafasi MWAKILISHI kutoka Tanzania naye kajichanganya humo kwa kuzungumza lugha hiyo isiyo ya kibantu na kumwambia- Rais hupaswi kujua nini nimewaambia,hiyo ni siri ya ndani japokuwa kuna watu watakuja kutafsiria mh.Rais baadaye lakini siyo jambo jema kwa mustakabali wa nchi na watu wake.

Mambo ya kitaifa yanapaswa kufanyika kitaifa au kimataifa kwa faida ya jumuiya nzima,kwa kweli nampa pole RAIS UHURU KENYATA kwa yaliyotokea na mimi mwenyewe kwani maeneo mengine sikuweza kuelewa kabisa isitoshe nilikuwa nafuatilia kupitia ntv.

Sasa najiuliza kwa baadhi ya wagombea waliopigiwa kura uchaguzi uliopita lakini leo tunaona mienendo yao ama kweli tungeingia kwenye tanuru la moto.

Sikupendezwa kabisa watanzani mambo kama haya tuyakatae yabaki kwenye vikao vya kimila tu wala si vinginevyo.MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.


Upo sahihi kiongozi walitakiwa tu waweke vionjo kwenye salamu au awepo mkalimani kama kuna watu hawaelewi kiswahili au kiingereza
 
Maneno kama hayo angeonge Magufuli angeitwa dikteta
 
KENYATA NILIMUELEWA, LAKINI JAMANI LOWASSA SIJUI ALISEMA NINI, SIJUI KAMA KUNA YEYOTE ALIMUELEWA. YAANI NI KITUKO
Bogasi kama wewe uwezi elewa matamshi ya lowassa... we subili tufyatueni,sijaribiwi,majizi,vilaza ndo uwezo wako wa kufikiri ulipo na fikra zilipoelekea..
 
Bogasi kama wewe uwezi elewa matamshi ya lowassa... we subili tufyatueni,sijaribiwi,majizi,****** ndo uwezo wako wa kufikiri ulipo na fikra zilipoelekea..
Acheni kutumia maneno makali kwenye mijadala ya msingi,maneno ambayo hayana mantiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Maana yake ni kwamba ninyi wa Tzzz mnashirikiana na wapinzani wa Kenya kumfanya aone kiti chake ni cha moto,,lakini Mungu si athimani bado yupo kitini.
Tueleze ni watanzania wapi wanaoshirikiana na wapinzani wa Kenya? toa ushahidi, sio hisia tu. Nakumbuka kuna kipindi Mseven alikuwa anampiga Besigye hadi anakimbilia Kenya kule, kupumzika na muda mwingine matibabu, kwa nini mseven hakuituhumu serikali ya Kenya kuwa inashirikiana mpinzani wake? Kenya punguzeni hisia, fanyeni siasa nchini kwenu bila kuhusisha Tanzania, mnaweza itaja Tanzania kwenye kampeni zenu kama kulifaa kuwa Tanzania wenzetu wamefanya kitu hiki na kile kama ambavyo Tanzania huitaja Kenya katika Nyanja mbalimbali kwa kutaka kujifunza.
 
Sisi tuko mbele ya wakenya...hayo mambo ya uhuru wa kuongea tulishayaishi miaka mingi toka enzi za kina JK..sasa tuko katika zama tofauti

Kama si upuuzi huu na kukosa elimu na fahiwa ni nini? Mko mbele katika nini hasa?
 
Nd

Nadhani hamjaelewa kwa nini uhuru alisema hivyo...wakati wa hotuba za walio wengi hasa laila na wenzao walikuwa wanamshabulia sana uhuru sasa lowasa alipopewa nafasi ya kuongea akamwambia uhuru naona mheshimiwa umekalia kitu ch moto. Hii lowasa aliisema kutokan na jinsi kina laila walivyomshaburia uhuru kwenye hotuba zao.

Hivyo uhuru kwa kuwa alikuwa wa mwisho kuhutubia baada ya kina laila na lowasa ndo maana akawa anamjibu lowasa aliyemwambia umekalia kiti cha moto na laila aliyesema jubilee ina mikono miwili.

Kuna mwingine amesema hiki ndo kipindi cha mwisho kwa uhuru...hii si kweli uhuru amechaguliwa 2013 kwa mara ya kwanza hivyo anaweza gombea tena 2017.

Ningekusamehe kama ingekuwa ni katika kusema tu lakini kuandika pia? Yaani hadi leo jina la RAILA ni Laila kwako? Baya zaidi, Laila ni jina la msichana!
 
Raila hawezi kuwa rais Kenya, yeye aje ajipe faraja kukaa ikulu ya TZ kwa rafiki yake na kutembea na ving'ora vya rafiki yake huku TZ. Kenyata yuko makini hana domo hajui kulalama ni mtu wa stratege na sasa wanavyounganisha vyama ndio wanammaliza kabisa Odinga, ubabe wake kwa wakenya hauwezi kufaulu, rafiki yake ubabe wa chama chake umemsaidia kuingia ikulu kuendeleza ubabe wake na watu washamjua ila mwenyewe kashajishtukia now kaanza kuwasogelea aliokuwa anawakimbia.
 
tuko mbele yao kwa fitna, woga na ujinga. lakini wako mbele yetu tena sana kwenye viwanda, elimu, demokrasia nk, Sisi tumebaki kukimbiza mwenge na kuwaambia wananchi tuna amani na hatuna ukabila.
NDO UKWELI JAPO UNAUMA
 
Back
Top Bottom