Hongera
kadoda 11 kwa kuanzisha huu uzi ambao naamini utaisha bila povu
Binafsi hii ID ni kama mpya haina mda mrefu! Lakini nimeanza kuifuatilia rasmi JF mwishoni mwa mwaka 2011! Kipindi hiki nilikuwa nje ya nchi hivyo sikutaka kujisajiri kama mwanachama, nilibaki kusoma tu kama guest!
Mara nyingi nilikiwa napitia jukwaa la siasa kujua kinachojiri huku nyumbani, huku mijadala ya kule MMU ikinikera kweli kweli hadi nikawa naona lile jukwaa halina haja
Nirudi kwenye mada, Kwenye hili jukwaa nilikuwa napita nikiwa nimetulia kabisaaaa!
Kuna watu walikuwa wananivutia kwa uchangiaji wao wa mawazo, hasa jinsi walivyokuwa wanakaa kidete kupambana na wakenya!
Upande wa tz!
1; Geza ulole!
Huyu jamaa ningekuwa namfaham in person basi ningeshampa tuzo binafsi kwa mda wake ambao alikuwa anautumia kupangua hoja! Nakumbuka kuna mkenya alikuwa anaitwa Lawmahima (Sikumbuki vizuri ID yake maana siku hizi simuoni!) Hawa jamaa walikuwa wanapelekana mpaka basi!
2; Askari Kanzu!
Huyu naye alipambana sana na kuwa inspiration kwangu! Siku hizi simuoni mara kwa mara nahisi kakabidhiwa jukum zito!
3;Joka kuu!
Nilipenda sana uchambuzi wa huyu bwana kwenye masuala anuai!
Kuongezea kwenye orodha hiyo yupo Kimweri, wapo wengi wengine nawatunza kwa sababu maalum!
Upande wa jirani zetu!
1;
Iconoclastes!
Nampenda huyu jamaa maana ni mwepesi wa kukubali jambo unlike wakenya wengi! Ngeri yake pia hasa akipata kapovu kwa mbali huwa ananikumbusha mambo ya ngugi wa thiong'o
2; @Samuel999
Ni mchambuzi mzuri wa mambo na hana povu sana!
3;
MK254, huyu nahisi anaongoza kutokuwa na povu miongoni mwa wakenya,