Kenyaforum: Who is your best conversationalist?.

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,736
kwa mda mrefu,mijadala mbalimbali imekuwa ikijadiliwa katika subsection ya kenyaforum na kupelekea kuvutia wachangiaji na
viewers wengi.

kenyaforum imejipatia wachangia mada wazuri wa kudumu na wasio wa kudumu,baadhi yao wameacha alama zinazofanya wawe mfano wa kuigwa.

napenda leo tuweke tofauti zetu za kinchi na utaifa kando,tuambiane ni member yupi anayekuvutia katika mijadala unaposoma maandiko yake.

binafsi wanaonivutia ni hawa hapa:
Geza Ulole,MK254 na Edward Wanjala.

Geza Ulole.
huyu mkuu ndio mtu aliyenivutia niweke kambi ya kudumu hapa kenyaforum.

nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2011 nilipojiunga tu na jf.nilibaini kuwa geza alikuwa ni mmoja ya watz wachache waliothubutu kupambana kwa hoja na wakenya kwa wakati huo.

alikuwa anajitahidi sana kupangua hoja za wakenya zilizokuwa zimeegemea katika ku-stereotype watanzania na mitazamo mbalimbali hasi.

ghafla nikawa inspired naye na kumfanya kuwa role mode wangu.
to me he is my all time icon in kenyaforum.

MK254
brother MK254 ni mmoja kati ya wakenya wachache hapa kenyaforum anayemudu kuandika comments zake kwa kiswahili kinachoeleweka na watu wengi.
kwa hakika ananivutia sana na ninampa pongezi kwa hilo.

yupo tofauti na baadhi ya wakenya wengi ambao hawamudu kuandika paragraph nne au tano kwa lugha ya kiswahili na zikaeleweka na watu wengi.

kuna wakati aliwahi kukiri kwamba kuishi kwake tanzania kulimsaidia sana kuboresha kiswahili chake.

Edward Wanjala
huyu jamaa ni mkenya na hana mda mrefu hapa jamiiforum,kajiunga mwaka 2016.

licha ya kutokuwa mkongwe wa jf, kuna vitu ambavyo huwa ananivutia na kumfanya kuwa one of my best conversationalist in kenyaforum.

wanjala ana hekima ambayo inakushawishi uendelee kujadiliana naye au usome maandiko yake.

yupo tofauti na wakenya wengi tulionao jf.wengi weo mjadala unapokuwa umepamba moto hususani inapotajwa kenya,huishia kupatwa na jazba na kuanza kutukana.

wanjala yupo tofauti katika hilo.huwa ninamtania kwa kumuita "mtu mwenye njaa" na wala hakasiriki.

sasa nakabidhi topic kwenu member wenzangu,kuwa huru kutuambia ni member yupi anayekuvutia katika mijadala hapa kenyaforum.taja member yoyote anayekuvutia awe mtanzania au mkenya.

pia nakaribisha comments toka kwa member wa majukwaa mengine maarufu kama siasa na MMU.tunajua baadhi yenu huwa mnapita kimya kimya huku kenyaforum kufatilia mijadala mbalimbali inayoendelea.

NB:
kenyans and tanzanians this is a no beef thread,so put aside the hate for one minute,try to be objective and unbiased.tell us who is your best conversationalist in kenyaforum?
 
uzi mzuri ila,wakenya wengi tunapenda picha, hivyo acha nianze kwa kuwafisha mecho wadau humu ndani..huyu binti anatoa huduma ya usalama ndani ya sgr baby
FB_IMG_1496566567088.jpg
 
Kuna jamaa huwa namkosa sana, anaitwa JokaKuu siku hizi huwa namwona amekomaa na nyuzi za kibongo, amesusa Kenyan forums kabisa. Yule jamaa alikua na uelewa wa juu kwenye kila aina ya mada halafu hana chembe chembe za kibaguzi, ni mzalendo tu kwa nchi yenu.

Mwanzoni nilikua napata jazba kila nikiona majibu yaliyojaa kejeli kutoka kwa Wabongo, na nilikua najibu tusi kwa tusi, lakini huyu jamaa alinifanya nianze kuwa na mtazamo chanya na kuwa na imani kwa baadhi ya Watanzania, kwamba kuna baadhi yenu mna uwezo wa kujadili hoja kwa kuzingatia mantiki na hekima.

Upande wa Kenya kuna Sammuel999 na Kafrican hawa jamaa sijui taaluma zao lakini wakianza kujadili hoja inabidi ujipange maana watatiririka na kudhihirisha ufahamu wao wa hali ya juu. Kuna wengine pia kutokea nchi zote mbili huwa wako sawa sana, na bila kuwasahau yule Mnigeria na jamaa wa kutokea Afrika Kusini ambao walitoweka kwa kuchoshwa na mada za Kiswahili.
 
thread nzuri..pia ningepeda tumalize hili swala la kuingiliana watz na wakenya.....mtu akileta mada hapa JF tujadili kwa amani si tu kujaribu kuchafuliana jina na kutusiana...Asante. Personally nampenda kaka Tuusan
Broo mimi nawapenda wakenya siku zote, nikianza kuwataja itakua napoteza muda! !hua natada na tambo zenu mkiwa mnapamba jambo flan mlilofanikisha apo kwenu looh nyie watu raha sana...

Credit ziende kwa wataalam wa kuchambua mambo ya kiuchumi hua najivunia maneno mapya kibao humu,pia napata misamiati mingi especially muda wa watu kutema mapovu yao mubashara, kingereza ya jirani ni murua sana especialy pale mtu akiwaanatoa msisitizo flan kwa apa south
Kijana wangu nakupa shukrani za dhati kabisa kwa kuniona kama mwana!! Tupo pamoja mkuu!!
 
Kuna jamaa huwa namkosa sana, anaitwa JokaKuu siku hizi huwa namwona amekomaa na nyuzi za kibongo, amesusa Kenyan forums kabisa. Yule jamaa alikua na uelewa wa juu kwenye kila aina ya mada halafu hana chembe chembe za kibaguzi, ni mzalendo tu kwa nchi yenu.

Mwanzoni nilikua napata jazba kila nikiona majibu yaliyojaa kejeli kutoka kwa Wabongo, na nilikua najibu tusi kwa tusi, lakini huyu jamaa alinifanya nianze kuwa na mtazamo chanya na kuwa na imani kwa baadhi ya Watanzania, kwamba kuna baadhi yenu mna uwezo wa kujadili hoja kwa kuzingatia mantiki na hekima.

Upande wa Kenya kuna Sammuel999 na Kafrican hawa jamaa sijui taaluma zao lakini wakianza kujadili hoja inabidi ujipange maana watatiririka na kudhihirisha ufahamu wao wa hali ya juu. Kuna wengine pia kutokea nchi zote mbili huwa wako sawa sana, na bila kuwasahau yule Mnigeria na jamaa wa kutokea Afrika Kusini ambao walitoweka kwa kuchoshwa na mada za Kiswahili.
kitu nakupenda jirani hunaga ugomvi na mtu . your so lovely
 
ulinicomfort sana nilipoibiwa chupi zangu na wakenya
 
Samuel sijamfatiria sana ila Kafrican yupo vizuri.jamaa ni great thinker original.

ningekuwa nina namba ya simu ya uhuru kenyatta ningemshauri amjumuishe huyu jamaa katika timu ya washauri wa masuala ya kiuchumi serikalini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom