joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Bila kujali vyama, kabila au sehemu wanazotoka, wabunge wakenya wamekubaliana kwamba serikali ya Kenya imefilisika kiasi cha kuomba kuruhusiwa kuomba mikopo itakayowezesha kulipa Madeni ya nyuma na kujenga miradi mikubwa.
Wakati Tanzania ikijitahidi kujenga miradi yake mingi kwa pesa zake za ndani, ili kupunguza kukopa mikopo yenye riba kubwa, kwa jirani hali ni mbaya sana ya kiuchumi kiasi kwamba muda si mrefu nchi italazimika kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi, ikiwemo rais na mawaziri wake.
Ningewaomba majirani wamtume rais wao ili aje kumuangukia " uncle Magu" ili awakopeshe japo $1B, kwasababu pesa ipo nyingi tu, tunanunua midege na kujenga madaraja na barabara vile tunavyojisikia