Rais William Ruto asema nchi haitakopa kulipa mshahara wa wafanyakazi wa umma

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,105
3,619
Rais wa Kenya William Ruto amesema nchi hiyo haitakopa ili kuwalipa wafanyakazi wa umma hata kama vyama vya wafanyakazi vilitishia kugoma kutokana na kutolipwa mishahara ya Machi.

Ruto alilaumu ucheleweshaji wa deni kubwa la umma nchini, kutokana na baadhi ya mikopo kufikia hatua ya kulipwa mwezi huu.

Alisema mishahara hiyo italipwa kutokana na ushuru unaokusanywa na mamlaka ya mapato.

Angalau mashirika mawili ya wafanyikazi yametoa notisi ya kugoma wiki hii ikiwa hawatalipwa pesa zao.

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu, mshauri mkuu wa marais wa masuala ya kiuchumi alisema mishahara hiyo italipwa hadi mwisho wa mwezi lakini akashauri serikali kupunguza ufujaji wa fedha za umma.

Deni la umma la Kenya sasa linafikia asilimia sitini na tano ya mapato.

Nchi inahitaji zaidi ya $420M kila mwezi kulipa mishahara na pensheni kwa watumishi wa umma.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Benki ya Dunia na IMF kutoa onyo tofauti kwamba Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inazama katika mgogoro mpya wa madeni, huku nchi nyingi zikiwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na deni.

Chanzo: BBC Swahili. April 11, 2023.

Angalizo:

Ni hatari kumbe wafanyakazi wa Kenya hawajalipwa mshahara wa mwezi Machi!!!!

Ukiona mwenzako ananyolewa, na wewe tia maji kwenye kichwa.

Tanzania yetu ni imara sidhani kama tutafika huko, ila hiki kipande kinaleta wasi wasi:

"Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Benki ya Dunia na IMF kutoa onyo tofauti kwamba Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inazama katika mgogoro mpya wa madeni, huku nchi nyingi zikiwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na deni."
 
Nchi zetu hizi uongo mwingi sana, ukiona mwenzako anayolewa, zako tia maji
 
Back
Top Bottom