DOKEZO Kutolipwa madeni ya mishahara ya nyuma kwa watumishi Kampala University (Tanzania)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Chuo kikuu cha Kampala nchini Tanzania (KIUT) kimekuwa na utaratibu au mazoea ya kukwepa kulipa wafanyakazi walioacha kazi au kuondoka chuoni hapo mishahara ambayo haikulipwa kipindi walipokuwa wakifanya kazi chuoni.

Hata hivyo wafanyakazi wanaoendelea na kazi wengi bado wanadai mishahara ambayo hawajalipwa kipindi cha nyuma toka 2020 ikiwepo ya wakati wa COVID-19 ambapo chuo kiliamua kuwalipa wafanya kazi nusu mshahara kwa muda wa miezi mitatu.

Wafanyakazi hawa Hata wakifuatilia wanatoa ahadi za uongo bila kutekeleza ahadi zao, wakiwa na lengo la mfanyakazi kufuatilia kwa muda mrefu na hatimae kuchoka na kuacha kufuatilia hivyo wao wanabaki na faida ya pesa za hao wafanyakazi.

Hii imekuwa ni utamaduni wao wa kila mfanyakazi anayeondoka kwao kutowalipa mishahara wanazodai.

Hata wakipelekewa bank statements zinazoonesha madai hayo hawafanyii kazi na kuishia kutoa ahadi kwa muda mrefu ili mfanyakazi huyo apotezee.

Kiuhalisia hiyo tabia sio sahihi na inawanyima haki wafanyakazi hao kwani walifanya kazi hata bila kulipwa hivyo ni wajibu wa mwajiri huyo kuwalipa.

Mamlaka inayohusika itoe msaada ili wafanyakazi hao wapewe haki zao

Sambamba na hilo chuo kina wakata wafanyakazi makato ya BIMA na NSSF bila kupeleka kwa mamlaka husika hali hii inawapelekea wafanyakazi kushindwa kumudu garama za afya pindi wanapoumwa na ukizingatia wanabahatisha kulipwa mshahara, wafanyakazi wengi NSSF zao zinasoma ZERO ilihali tayari wamehudumu kazini hapo kwa miaka mingi

Tunaomba mtupazie Sauti ili dhulma hii ijulikane
 
Back
Top Bottom