Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Hizi budget huandikwa kitaalam sana,huwa hazipo kumsaidia mnyonge,Mara nyingi zipo kwa ajili ya kuangalia chanzo cha mapato ya Serikali,budget za Serikali haziko ktk kumkomboa mnyonge,watu watazidi Kuwa masikini zaidi,wenye nazo watazidi Kuwa nazo,nimesoma budget ya mwendokas sioni tofaut ya budget zilizopita.Mnyonge kaachwa mbali sana ila inazidi kumkamua tu.Baba Jesca kama lengo lake ni kuwasaidia wanyonge basi amekwama.
 
Tusipokuwa makini tutawapoteza watalii. Siku hizi hadi vinyago vinatozwa kodi pale airport.
 
mimi ningekuwa magufuli,ningepunguza hata hiyo taxi wanachajiwa iwapo watakuja kulipia kila kitu ndani ya nchi yetu.Kama wakifanya kila kitu nje ya nchi kupitia wakala rasmi na wale sio rasmi nathani ndio hapo kodi inaweza kuwa juu.Magufuli naomba sana usituharibie nchi.
Mawazo mazuri sana haya
 
Kenya imetangaza bajeti yake huku wakiendelea kutokuweka VAT kwenye sekta ya utalii ili kuvutia watalii na kukuza sekta hiyo

Tanzania tunalenga watalii matajiri wenye pesa zao wakati kenya wanalenga watalii maskini ambao hata ukiongeza dola moja kwenye visa wanalia kama watoto wadogo.Watalii inaolenga kenya ni wale wanafunzi,walalahoi ambao hawali wala kulala mahoteli ya kitalii wanaokula kwa mama nitilie nk

Wote ni mashahidi kuwa watalii walalahoi walikuwa wengi miaka ya nyuma sio sasa ila ukienda kenya wako kibao utakutana nao wanakula mahindi ya kuchoma njiani na hulala kitanda kimoja hosteli wanalala hata wanne na wengine hukaa homestay nyumba za watu.Tanzania haiwalengi wala kuwavutia watalii wa aina hiyo ndio maana hata Visa TANZANIA ILIGOMA KUWA NA VISA YA UTALII MOJA KWA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI.

Usifananishe Tanzania na Kenya.WAKITAKA KUVUTIA watalii maskini wafute hata gharama za visa kuingia kenya wakitaka.Tanzania hatulengi hao.
 
Tatizo walotupangia bajeti hii wameangali pesa abayo iko kwenye mzunguko pamoja na wafanya biashara waliopo lakini wakasahau kuwa zaidi ya 60% ya wafanyabiashara wamekuzwa na mfumo uliotangulia wa kukwepa kodi na udanganyifu pia pesa nyingi tunazoishia kuziona possibly ni za masalia ya wizi na rushwa.
Hapo naelekea kukubaliana na ZZK kuwa itakuwa ngumu kukusanya 60% ya pesa walizoplani maana tutegemee exit kubwa ya wafanyabiashara wadanganyifu huku tukiombea ujio wa kizazi kipya cha wafanyabiashara wazalendo ambacho nacho kinahitaji muda kujijenga!
 
Wenzao hawaweki VAT ili kuvutia watalii. Ila sisi tunaweka kwasababu hatuwahitaji. Watalii wakipungua ndo tutaanza kulaumiana.
kutokana na kua na vivutio bora kuliko majirani zetu sisi tunalenga watalii tajiri sio wale wanaokuja na vibegi mgongoni kuvuta bangi pwani.
 
Kenya ni wakina nani hadi tuwaige?. Sie tunaendelea na mikakati ya ujenzi wa bomba la mafuta....
Je, unajua athari zake kiushindani kwenye sekta ya utalii? Bila shaka hujui. Hapa ndipo serikali inapaswa kuwa makini sana maana hata sasa Kenya wako juu sana kwenye sekta ya utalii na Tanzania inapaswa kuhakikisha kuwa inavutia watalii wengi kuja kutalii. Kama kuongeza VAT katika eneo hili ni jambo jema na litaongeza pato katika sector hii basi na iwe hivyo.
 
Tanzania tunalenga watalii matajiri wenye pesa zao wakati kenya wanalenga watalii maskini ambao hata ukiongeza dola moja kwenye visa wanalia kama watoto wadogo.Watalii inaolenga kenya ni wale wanafunzi,walalahoi ambao hawali wala kulala mahoteli ya kitalii wanaokula kwa mama nitilie nk

Wote ni mashahidi kuwa watalii walalahoi walikuwa wengi miaka ya nyuma sio sasa ila ukienda kenya wako kibao utakutana nao wanakula mahindi ya kuchoma njiani na hulala kitanda kimoja hosteli wanalala hata wanne na wengine hukaa homestay nyumba za watu.Tanzania haiwalengi wala kuwavutia watalii wa aina hiyo ndio maana hata Visa TANZANIA ILIGOMA KUWA NA VISA YA UTALII MOJA KWA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI.

Usifananishe Tanzania na Kenya.WAKITAKA KUVUTIA watalii maskini wafute hata gharama za visa kuingia kenya wakitaka.Tanzania hatulengi hao.
mmmhh kwa hiyo utalii wa tanzania umewalenga akina bill gates. Donald trump..Abramovich..Nilikuwa silijui hili
 
Dr.Mpango akisoma bajeti katika sekta ya utalii alisema watatoza VAT katika gharama mbalimbali za utalii huku akitoa mfano wa Kenya kwamba nchi hiyo pia inatoza VAT katika sekta hiyo.Wakati huo huo Kenya imetangaza bajeti yake huku wakiendelea kutokuweka VAT kwenye sekta ya utalii ili kuvutia watalii na kukuza sekta hiyo
Nchi yetu ina vivutio vingi kuliko kenye watakuja tuu
Nchi yetu ni salama kuzidi kenya..!
Tuwaache kenya wafanye watakavyo na sisi tufanye yetu!
 
Kiukweli tukiweka unafiki pembeni kodi kwenye utalii sio sahihi...nawajua wazungu wako makini sana na matumizi..ndio maana asilimia kubwa ya watalii wanakuja kwa mafungu ili wapunguze gharama..tutasababisha watalii wapungue sana maana nchi nyingi sasa hivi zina vivutio vya utalii sio tanzania pekee
 
Hii ndiyo tofauti ya Viongozi wa Tanzania na Kenya, Tanzania tunakuruputa kuwaiga wengine badala ya kufanya tafiti za kina.
Nilitegemea kwa kuwa Kenye walikuwa wanalipisha tozo sisi tungeachana na huo ushuru kikaka ni moja ya kishawishi cha kutuongezea Watalii.

Inashangaza kuona Serikali iliyojaa MaProf. na MaDr. Inashindwa kuwa na mipango thabiti ya kiushindani, nchi zilizoendelea zinapunguza kodi ili kuwavutia wafanyabiashara na Investors wawe wengi ili wakusanye kodi kidogo kwa watu wengi lakini sisi tumekazania kupandisha kodi.

Serikali lazima ibuni vyanzo vipya vya mapato na kuviboresha vilivyopo, halafu utashangaa tunashangilia kuwa hii budget ni ya mfano imelenga kumkwamua Mtanzania..... hii budget ni finyu mno, 29 Trillion ni ndogo ukilinganisha na hao tunaojifananisha nao ambao budget yao ni 55 Trillion (TSH.) huku wakiwa na idadi ndogo ya watu ukilinganisha na sisi.
 
Tanzania tunalenga watalii matajiri wenye pesa zao wakati kenya wanalenga watalii maskini ambao hata ukiongeza dola moja kwenye visa wanalia kama watoto wadogo.Watalii inaolenga kenya ni wale wanafunzi,walalahoi ambao hawali wala kulala mahoteli ya kitalii wanaokula kwa mama nitilie nk

Wote ni mashahidi kuwa watalii walalahoi walikuwa wengi miaka ya nyuma sio sasa ila ukienda kenya wako kibao utakutana nao wanakula mahindi ya kuchoma njiani na hulala kitanda kimoja hosteli wanalala hata wanne na wengine hukaa homestay nyumba za watu.Tanzania haiwalengi wala kuwavutia watalii wa aina hiyo ndio maana hata Visa TANZANIA ILIGOMA KUWA NA VISA YA UTALII MOJA KWA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI.

Usifananishe Tanzania na Kenya.WAKITAKA KUVUTIA watalii maskini wafute hata gharama za visa kuingia kenya wakitaka.Tanzania hatulengi hao.
Hacha uongo, unadhani matajiri hawataki vitu bora vyenye gharama nafuu?
Hao unaosema wanalenga watalii masikini unajua mwaka jana sekta ya ya Utalii umewaingizia kiasi gani na wewe umeingiza kiasi gani.
 
Sio lazima wanachofanya kenya nasi tufanye,kama wamepanga hesabu zao wakaona watoze VAT hawakuangalia kenya,au na sisi tuige ule utalii mwingine?
 
Kila kitu kukurupuka tu!! Hatuweki pesa bank wala Hatuweki kwenye mobile money! Wapambanae na makampuni ya simu!
mimi nimejitoa kwenye payroll nitajilipa tu kama kibarua
hawapati paye wala hawatanikata bank
 
Back
Top Bottom