Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Tanzania ni ya pili duniani baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vizuri sana vya utalii, hii vat ikipitishwa na bunge pato la taifa litapungua sababu sekta hii inachangia asilimia kubwa kwenye pato la taifa. Vat ikiwekwa itasababisha kampuni za utalii zitoze pesa nyingi zaidi kwa wageni matokeo yake idadi ya wageni watakao kuwa wanakuja nchini itapungua.
 
Kwenye hili la VAT exemption ni muhimu kutoa somo kidogo ili wanaodai exemption wajue kwa uhakika athari ya kile wanachodai.

Kwanza jambo la mwanzo ni kutofautisha kati ya VAT - exemption (read "isiyotozwa kodi") na VAT - zero rating (read "inayotozwa kodi ya asilimia sifuri"). Ingawa dhana hizi mbili zinaonekana kama zinafanana (kwa mtu wa kawaida), lakini kitaalamu zina tofauti kubwa.

VAT Exemption
Mfanya biashara anayeuza bidhaa au huduma ambazo ni exempt haruhusiwi kudai marejesho (VAT input credit) ya VAT aliyotozwa na suppliers wake kwenye manunuzi anayofanya kwa ajili ya biashara yake (inputs). Hii maana yake ni kuwa VAT kwenye manunuizi yake itakuwa ni sehemu ya gharama ya uendeshaji wa biashara yake. Sasa kama VAT kwenye manunuzi ni sehemu ya ghara

Zero rating
Mfanya biashara anayeuza bidhaa au huduma ambazo ni zero-rated anaruhusiwa kudai marejesho (VAT input credit) ya VAT aliyotozwa na suppliers wake kwenye manunuzi anayofanya kwa ajili ya biashara yake (inputs). Hii maana yake ni kuwa VAT kwenye manunuizi yake haitakuwa ni sehemu ya gharama ya uendeshaji wa biashara yake. Vivyo hivyo kwa wafanya biashara ambao wanauza bidhaa ambazo ni standard rated (zintozwa VAT ya 18%).


Ili ieleweke kirahisi natumia mfano wa wafanya biashara A, B na C ambao wote wanataka faida (margin) ya 20% kwenye gharama zao. Tuseme, wote wananunua inputs zinazotozwa kodi kutoka kwa supplier kwa shilingi 100 na kwa sababu ya kodi ya asilimia 18% kila mmoja anamlipa supplier wake shilingi 118 (i.e. sh 100 na VAT sh 18). A anatumia input hizo kutengeneza bidhaa ambayo ni exempt na B anatengeneza bidhaa ambayo ni zero-rated na C anatengeneza bidhaa ambayo inatozwa kodi (standard rated, 18%).

Tuchukulie (kwa urahisi) kuwa A, B na C hawana gharama nyinginge yoyote ukiacha hizo inputs ambazo kila mmoja kalipa sh 118. Kwa A, VAT aliyolipa (sh 18) haruhusiwi kudai marejesho na hivyo kuwa ni sehemu ya gharama yake. Lakini B na C, kwa upande mwingine wanaruhusiwa kudai marejesho (kutoka mamlaka ya mapato) ya sh 18 kwa hivyo VAT waliyolipa kwenye inputs sio sehemu ya gharama zao. Kwa hivyo gharama ya input za A ni sh 118 na B na C ni sh 100 kila mmoja (ni muhimu kuelewa hapa kwa sababu bei ya bidhaa zao inaanzia hapa). Utakumbuka mwazo tulisema hawa watatu wanataka faida (margin) ya 20% kwa hivyo bei ya bidhaa zao zitakuwa ifuatavyo:

A (anauza exempt products): Inputs ni sh 118, akiweka faida ya sh 23.60 (20% ya 118) bei yake inatakiwa iwe sh 141.60;
B (anauza zero rated products):
Inputs ni sh 100, akiweka faida ya sh 20.00 (20% ya 100) bei yake inatakiwa kuwa sh 120.00; na
C (anauza standard rated products): Inputs ni sh 100, akiweka faida ya sh 20.00 (20% ya 100) bei yake inatakiwa kuwa sh 120.00 lakini kwa kuwa bidhaa zake ni standard rated, ataongeza na VAT ya sh 21.60 (18% ya 120) na hivyo bei kwa mteja itakuwa sh sh 141.60

Bei ya A na C zinalingana, lakini bei ya B ipo chini. Hii maana yake nini? Sio mara zote kutotoza VAT (exemption) kunaweza kuleta unafuu kwa mteja wa mwisho. Kimantiki, ili biashara yoyote, iwe na faida, ni lazima mapato yaweze kukidhi matumizi yote na kubakia (faida). Ndio kusema kuwa price anayolipa mteja tayari imeshazingatia gharama za mfanya biashara. Kwa kutoelewa, kuna nyakati watu wanachanganya kati ya zero rated na exemption au hata kama hawachanganyi lakini hawajui athari zake za kikodi. Kwa hivyo kama lengo ni kumpunguzia gharama mteja wa mwisho, makampuni ya utalii ya Tanzania yasidai exemption na badala yake wangedai zero-rating ya huduma zao kwa sababu ni hii pekee inayoweza kupunguza gharama kwa mteja wa mwisho.
 
kutokana na kua na vivutio bora kuliko majirani zetu sisi tunalenga watalii tajiri sio wale wanaokuja na vibegi mgongoni kuvuta bangi pwani.

Ndo ujinga mnaojazana mkiwa Lumumba?
 
Duh....yani wanafanya mambo kwasababu fulani amefanya...hii inasikitisha..!
 
Mipango chini ya Mpango ....wacha tuone mpango huu utatoboa kweli.......??
 
mimi ningekuwa magufuli,ningepunguza hata hiyo taxi wanachajiwa iwapo watakuja kulipia kila kitu ndani ya nchi yetu.Kama wakifanya kila kitu nje ya nchi kupitia wakala rasmi na wale sio rasmi nathani ndio hapo kodi inaweza kuwa juu.Magufuli naomba sana usituharibie nchi.
unamaana huduma ya magari ya biashara ya mjini? ama Taxi bubu?
 
Hivi kweli watanzania wote na akili zetu pamoja na viongozi wetu makini tuwaige wakenya kwa kipi sasa.
Sijui kama umeelewa hoja vzr au unakurupuka tu kama kawaida yako. soma thread ndio uchangie. issue ni waziri kusema 'hata Kenya wanatoza vat" lkn ktk budget yao (Kenya) hawakuweka vat ktk utalii ili kuvutia watalii! haya sasa changia hoja kilaza wewe!
 
Dr.Mpango akisoma bajeti katika sekta ya utalii alisema watatoza VAT katika gharama mbalimbali za utalii huku akitoa mfano wa Kenya kwamba nchi hiyo pia inatoza VAT katika sekta hiyo.Wakati huo huo Kenya imetangaza bajeti yake huku wakiendelea kutokuweka VAT kwenye sekta ya utalii ili kuvutia watalii na kukuza sekta hiyo
Hivi kuna mwaka ambao Tanzania itaikamata kenya kwa maendeleo ?
 
Mi nilidhani hiyo VAT kwenye huduma za utalii imewekwa kwa msingi wa makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki...so Kenya wamekiuka makubaliano!
 
Hii bajeti utadhani imepangwa na mtu mmoja kama walikaa vikao kupanga bajeti hii waludishe tu hela za vikao hamna walichopanga...
 
Back
Top Bottom