Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Kenya yamruka Dr. Mpango kuhusu VAT kwenye Utalii

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,550
Reaction score
139,886
Dr.Mpango akisoma bajeti katika sekta ya utalii alisema watatoza VAT katika gharama mbalimbali za utalii huku akitoa mfano wa Kenya kwamba nchi hiyo pia inatoza VAT katika sekta hiyo.Wakati huo huo Kenya imetangaza bajeti yake huku wakiendelea kutokuweka VAT kwenye sekta ya utalii ili kuvutia watalii na kukuza sekta hiyo
 
mimi ningekuwa magufuli,ningepunguza hata hiyo taxi wanachajiwa iwapo watakuja kulipia kila kitu ndani ya nchi yetu.Kama wakifanya kila kitu nje ya nchi kupitia wakala rasmi na wale sio rasmi nathani ndio hapo kodi inaweza kuwa juu.Magufuli naomba sana usituharibie nchi.
 
Hivi kweli watanzania wote na akili zetu pamoja na viongozi wetu makini tuwaige wakenya kwa kipi sasa.
 
Hahahaha ndio tatizo la kuiga kwa wanaume wenzio hilo, Mara Kenya wamefanya hivi, mara Bunge halionyeshwi LIve south Africa ni lini na sisi tutakua role models wa wengine? Waseme mbona Tanzania hawafanyi hivi??
 
Hivi kweli watanzania wote na akili zetu pamoja na viongozi wetu makini tuwaige wakenya kwa kipi sasa.
Iulize serikali ya chama chetu hilo swali maana ndio waziri wetu wa fedha amesema tunawaiga wakenya, sasa wewe mfia chama mwenzangu unalialia nini tena?
 
Sisi kama tumeweka VAT basi tuboreshe huduma zetu ziwe za hali ya juu sana ili tuwapiku wakenya
 
Tatizo si kuwaiga kenya, Tanzania inampango wa kukuza utalii ili kuongeza pato la taifa na kuilinda shiling isishuke thamani, tunavivutio vingi sana vya utalii hivyo tukiwa na sera makini hili linawezekana. Lakini tunatatizo kubwa sana la kisera. Gharama za kufanya utalii Tanzania zikiwa kubwa watalii wataenda kwenye gharama ndogo, usalama kwa watalii ukiwa mdogo watalii watapungua, hivyo ni muhimu sana kuangalia gharama za kufanya utalii Tanzania ambazo ni kubwa sana kwa sasa, hivyo tunahitaji kuzipunguza na siyo kuziongeza. Hii ni pamoja na gharama za usafiri wa watalii, gharama za kula na kulala watalii, gharama za vibali na kadhalika.
 
Hivi kweli watanzania wote na akili zetu pamoja na viongozi wetu makini tuwaige wakenya kwa kipi sasa.
Hayo Maswali ungemuuliza Bwana MPANGO, yeye ndiye aliyesema kuwa anawaiga wakenya, kumbe wenzie walishaachana na hiyo mambo kitambo.
 
Back
Top Bottom