Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,809
- 11,973
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kufungwa kwa mipaka yake na Mataifa ya Tanzania na Somalia kuanzia usiku wa leo kwa siku 30 zijazo
Rais Kenyatta amesema kuwa ni madereva wa magari ya kubeba mizigo pekee ambao wataruhisiwa kuingia nchini Kenya baada ya kupimwa COVID19 na kupatikana kuwa hawana
Amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya madereva wa malori ya kubeba mizigo 78 raia wa kigeni kunyimwa kibali cha kuingia nchini Kenya baada ya kukutwa na virusi hivyo
Kenya aidha imeongeza muda wa marufuku ya kutoka nje kwa siku 21 zijazo hadi Juni 6