Trust me, namchukia sana Uhuru Kenyatta... namchukia Kenyatta si kwa sababu ni mtu anayestahili kuchukiwa bali namchukia kv mimi ni Mtanzania ninayeipenda nchi yangu and I'll always be there for my country. Namchukia Kenyatta kwa sababu mimi si Mkenya na Kenyatta is very smart for Kenyan interests. Labda usahihi nilipaswa kuwa na wivu lakini kwa ujeuri na hinda inabidi tu nimchukie kv Kenyatta ndie Rais ambae Africa ya leo ndie inamuhitaji. Kenyatta ni mroho tena mroho kweli kweli! Lakini tofauti na uroho wa wenzake kama vile Museven na Kagame ambao ni waroho wa madaraka; uroho wa Kenyatta ni wa kiuchumi... uroho wa kutaka kuifanya Kenya kuwa economic giant now and always! Hapa ndipo ninapomchukia Kenyatta cuz' he can do whatever he can to stand atop of others. The guy is smart, trust me... lile ni bebari la kuzaliwa na kurithi kwahiyo linafahamu hila zote zinazohitajika kwenye dunia ya leo!!! Haya mambo kwamba "hao watalii wakitaka waje, wasipotaka wasije...!" kamwe hayawezi kutoka mdomoni mwa bepari zohefu na lililokubuhu kama Kenyatta... sana sana si ajabu anakesha akiomba tuzidi kukaza ili "tukasanye kodi nyingi zaidi..!"
Kenyatta sikupata kumuogopa wakati wa JK kv nilifahamu JK anafahamu namna ya ku-deal na watu aina ya Kenyatta... ndo maana wakati ule anaruka ruka na akina PK na Ushoroba wa Kaskazini wao JK alikuwa anawacheka tu; kombora moja tu... wakaanza kutafutana wenyewe!!!
Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, popote ulipo fahamu kwamba nakuchukia... lakini nakuchukia kwa sababu tu nafsi yangu imejawa husuda!! Huwa nazidi kukuchukia kila inaponipitia taswira ya Silicon Valley au kitu kinachofanana na Silicon Valley ndani ya Nairobi endapo utapewa fursa ya kuendelea kuongoza Kenya! Hivi katika mazingira hayo, nikupende kwa lipi?!
Go to hell Mr. President!!