Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,692
- 26,584
Kenya haikufika pele kwa bahati mbaya, wale ni strategists na hutafuta maarifa popote pale yanapopatikana. Wanachokifanya hivi sasa ni kutuaminisha kuwa tunawamudu ili tubweteke. Sipati picha hali ingekuwaje kama nchi yetu ndiyo ingekua inapata zile mishe mishe za alshabaab. Lakini pamoja misukosuko jamaa wameendelea kustawi zaidi na zaidi, huku zoezi la UKUTA peke yake utasikia litakavyoyumbisha uchumi wa nchi kwa gharama zilizotumika kulipa per diems za askari, kuviweka vikosi katika hali ya tahadhari pia kutoa silaha kutoka zinakutunzwa na kutembezwa mitaani.Aisee, tusitiane pressure bhana!! Kwenye sakata la bomba la mafuta kutoka Uganda nilishawaonya watendaji wetu kwamba, guys, trust me, Kenyatta hatakaa apumzike hadi siku anaona mabomba yanatandazwa ardhini na kwamba safari ya kuja Tanzania imeanza otherwise, ataendelea ku-lobby hadi siku ya mwisho! Nadhani haikupita hata wiki moja tangu nitamke vizuri mara nasikia Kenyatta kenda Ufaransa kuonana na wenye TOTAL yao na sio huyu Mwakilishi wa TOTAL East Africa... aliamua ku-lobby na mwenye mbwa na sio mbwa mwenyewe! That's Kenyatta!!! Na endapo tutadhani tumeshamaliza kazi, tutakuja kuachwa kwenye mataa kwenye dakika za majeruhi with no time to fight back!! Mbaya zaidi, hata ku-fight back kwenyewe hatuwezi... bomba kuja Tanga ilikuwa ni issue ya kuokota embe dodo kwenye mbuyu but we didn't do anything serious kuipata ile opportunity!
Kenya wapo tayari kwenda kufanya lobbying kwa watakwimu wa kiuchumi wa world bank watoe takwimu zinazoonyesha kuwa Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi huku wa Kenya ukisuasua kwa lengo la kutubwetesha tu.