Rais Samia Suluhu Hassan ni mzalendo, Watanzania twende naye

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
RAIS WETU MPENDWA MAMA #SAMIA SULUHU HASSAN NI MZALENDO WA TAIFA HILI, ALIKOTOKA NA ALIPO, TUNAMUAMINI NA TUMUAMINI Fuatana Nami YonaPAVEA

Rais Mama #SAMIA SULUHU HASSAN amezaliwa, Amekulia, amesomea madarasa mengi Tanzania, Ni Muumini wa Dini Yetu pendwa ya #Kiislamu Tanzania, Amejaliwa Watoto wake Tanzania, Watoto wake Ni Watanzania Kabisaaa, Mama #Samia Suluhu HASSAN anaijua Tanzania Bara na Visiwani, Anajua shida za Watanzania, Naye ameanzia Kazi za Chini kwa juhudi akapanda na MUNGU akambariki, anajua Changamoto za kinamama, kinababa, na Watoto wa Tanzania, amezunguka Tanzania kila kona Zaidi ya wengi wetu tunaochonga, Narudia anaijua Tanzania Bara na Visiwani Atatufikisha.

Rais, Mama Yetu mpendwa #Samia suluhu HASSAN amekuwa Waziri Tanzania miaka kumi Upande wa ZANZIBAR na amehudumu upande wa Tanzania Bara miaka mitano Kama Waziri tena wa Muungano, Lakini nzuri zaidi Rais wetu Mpendwa Mama #Samia Suluhu HASSAN alikuwa makamo mwenyekiti wa Bunge la Katiba ambapo Yeye #SS Yaani #Samia Suluhu na Mwenyekiti wake #SS Yaani Samwel #Sitta (Hayati) Walishiriki na kusimamia katiba Bora ila ikatokea wajeuri mchakato ukafutwa, So Rais Mama #SAMIA SULUHU HASSAN NI Mzalendo wa Taifa hili wa Juu zaidi.

Isitoshe Mama #Samia Suluhu HASSAN kwa Uzalendo wake, Rais wetu Mpendwa wa awamu ya Tano Hayati Dkt #Magufuli alimuona na kumuamini Mama #Samia Suluhu HASSAN na Kuwa Mgombea mwenza wake na wakafanikiwa kuongoza miaka sita, So kwa Ukaribu huo huo wa Rais wa awamu ya sita na aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, Mama #Samia Suluhu HASSAN Rais wetu Mpendwa anajua Direction ya Hayati Dkt #Magufuli na pale penye mapungufu ataongeza na kurekebisha na ndo Maana Mama #Samia Suluhu HASSAN hajafanya Mabadiliko makubwa ya kiuongozi, kwani anawafahamu na anafahamu walikuwa wanaelekea wapi.

#KwendaKenya
Rais, Mama #Samia Suluhu HASSAN wakati anaingia ofisini Lazima amekutana na majukumu mengi yaliyoachwa na mtangulizi wake, Majukumu hayo Ni Pamoja na kuvisha kamisheni wanajeshi wetu waliokuwa wamehitimu, Kusaini Mkataba wa Bomba la Mafuta la #Ohima, Kaenda Nchini Kenya na tumeona manufaa aliyoyasema kwetu nk.
Watanzania wenzangu kumbukumbu zinaonesha Mwaka 2019 Yaani mwaka Juzi Rais Hayati Dkt #Magufuli alimpa Rais wa Kenya zawadi ya ndege wetu wa thamani aina ya #Tausi, Lakini pia Rais Hayati Dkt #Magufuli alizulu Kenya na alifika kijijini kwao Uhuru #Kenyatta na kumjulia hali Mama yake #Uhuru Kenyatta, So Rais wetu Mama #Samia Suluhu HASSAN anaendeleza Kazi na Zege Halilali, Songa Mbele Mama Samia Songaaa.

Sasa, Watanzania wenzangu, Ukweli Ni kwamba Mama #Samia Suluhu HASSAN ndiye Rais wetu Mpendwa, ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ndiye Mkuu wa Nchi Yetu Pendwa, ndiye Mfariji Mkuu wa Watanzania na ndiye Mwenyekiti wa chama Dola Milele CCM, Hivyo kwa Dhamana hiyo aliyopewa na MUNGU kupitia Watanzania Woote Naamini Mama #Samia Suluhu HASSAN atatufikisha tulipokuwa tunaelekea.

Mwisho:-
Tutambue na tuzishike Kauli Mbiu mbali mbali za Rais, Mama #SAMIA SULUHU HASSAN.

CORONAVIRUS
Jiongeze Tuamke Salama.... Means Ulinzi wa Afya Yako Unaanza na wewe Mwenyewe.

Kumtua Mama Ndoo Kichwani-Kusogeza Huduma za Maji Jirani.

Zege Halilali-Kazi Iendelee.
FB_IMG_1620322418037.jpg
 
Kampeni zishaisha na ilani ilipitishwa na wananzengo, sasa mnaletaje kampeni mpya!!
Kazi iendelee.
 
Hata hatukuelewi. Kauli yetu ni:
"Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano" - Kazi Iendelee.
Hizo za kwenu bakini nazo.
Rais na Kiongozi tumetunukiwa na Mungu.
Acha Mungu autwe Mungu na ni fundi haswa.
 
Mbona ni kama mnafanya Kampeni ili Hali Raisi wetu Ni Mama Samia Hadi sasa??

Hamjiamini?
 
Mbona mnatumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa mama ni bora? Maana mapambio yamekuwa mengi mpk unajiuliza kuna nini?????
 
Back
Top Bottom