Kenya kupokea chanjo ya Corona iliyorudishwa na Sudan Kusini

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Kenya inatarajiwa kupokea dozi 72,000 za chanjo ya Oxford/AstraZeneca kutoka Sudan Kusini zilizorudishwa kwa Mpango wa Pamoja wa Chanjo wa Dunia, COVAX.

Sudan Kusini imesema inarudisha chanjo hizo kutokana na kushindwa kuzigawa kwa wananchi kwa wakati kabla hazijaisha muda wake wa matumizi.

Taifa hilo lilipokea chanjo 132,000 mwezi Machi kutoka Mpango wa Chanjo wa COVAX wenye lengo la kuhakikisha Nchi zenye Uchumi mdogo duniani zinapata chanjo. Sudan Kusini hata hivyo, imefanikiwa kutoa chanjo 8,000 tu mpaka sasa.

Kiongozi wa Mpango wa Chanjo wa Kenya amesema kuwa amekamilisha taratibu zote za kupokea chanjo, na zinatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi, ingawa ameeleza kuwa UNICEF ndio wanaopanga tarehe ya kuwasili kwa chanjo hizo.

Kenya ilikuwa imetangaza kuwa imebakiwa na chini ya dozi 100,000 za chanjo hiyo huku Wakenya wengi wakiwa na wasiwasi kutokana na kutopokea chanjo kwa mara ya pili.

Katibu wa Baraza la Afya wa Kenya amewatoa hofu Wakenya kuwa dozi ya kwanza inaounguza hatari ya maambukizi kwa hadi asilimia 70, na ni vyema kuwa wamepata dozi ya kwanza kuliko kutopata kabisa.
Upatikanaji wa dozi ya pili ya chanjo ya corona nchini Kenya unatatizwa na uchache wa dozi hizo na ucheleweshwaji kutoka COVAX.

Chanzo: Nation
 
Kenya ni mabepari wao wanataka tu kuonekana wameheshimu mabeberu hata kama ni sumu watachanja.
 
Back
Top Bottom