Kenya Election 2007: Outcomes

jamani ikiwa matokeo yanakuja haraka namna hii...kwa idadi kubwa namna hii ya wapiga kura vipi zenj matokeo ya kura laki ngapi sijui yachukue two weeks kutangazwa? au wakati huo ndipo wanapofanya madudu ya kumjazia karume kura? hee heheh...heheh...
 
look like Kibaki will be back in the statehouse.

kwanini unafikiri hivyo? Uchaguzi ni tight sana,lakini kwa mwono wangu iwapo matokeo yanayotoka ni random basi Raila atashinda. Kumbuka matokeo mengi yanatoka Nairobi na Central kwa sasa kwa sababu ya mawasiliano ya haraka. Hivyo ninaamini bado ni tight race. Hata hivyo napata wasiwasi na Bunge litakavyokuwa maanainaonesha ODM watakuwa na majority. Ingekuwa tamu kama unakuwa na Rais Kibaki halafu hana majority bungeni. Au Rais Raila halafu hana Bunge upande wake.

tufuatilie
 
I am sure Kibaki will win this elction and is what I pray for.

Mungu Mbariki Kibaki

Wenzako wanashinda kwa kura, wewe unataka ushindi wa wishful thinking na prayer; Ushindwe kabisa na Kibaki/Moi wako, hayo ni mambo ya TZ tu msee, wale kumekucha!
 
Zitto,
Ukienda hapa http://politics.nationmedia.com/
Panaonyesha matokeo yanatoka mikoa mitatu so far, Nyanza, Rift Valley na Central. Sijui mgawanyiko wa Nairobi ukoje, lakini wapiga kura wa Nairobi ni wachache sana. Tuombe Mungu Central kuwe na wapiga kura wachache waliojitokeza, lakini kama wakiwa wametoka kwa wingi kama nilivyosikia BBC, Central inaweza kumbeba sana Kibaki. Sijui influence ya Raila kwenye ya Coast na Eastern.
Lakini tuvute subira mpaka dakika ya mwisho tuone, japo nina matumaini makubwa sana na Raila. Nitasikitika sana iwapo Raila atasikitika.
 
kwanini unafikiri hivyo? Uchaguzi ni tight sana,lakini kwa mwono wangu iwapo matokeo yanayotoka ni random basi Raila atashinda. Kumbuka matokeo mengi yanatoka Nairobi na Central kwa sasa kwa sababu ya mawasiliano ya haraka. Hivyo ninaamini bado ni tight race. Hata hivyo napata wasiwasi na Bunge litakavyokuwa maanainaonesha ODM watakuwa na majority. Ingekuwa tamu kama unakuwa na Rais Kibaki halafu hana majority bungeni. Au Rais Raila halafu hana Bunge upande wake.

tufuatilie

Mh. Zitto (MB), kwa kweli mimi siku zote naamini sana nguvu ya Bunge pale mgawanyo wa idadi ya wabunge kwenye bunge unapomfanya aliyeko madarakani awe na home work ya kuli-convince bunge kwenye mswada wowote ule inaoupeleka bungeni...

Natamani sana nchi yangu Tanzania itakapokuwa na Bunge la namna hiyo... huo mimi ndio nauita ushindi kwa umma, maana wananchi through wabunge wao ndio wanaamua mustakabali wa nchi yao...
 
Zitto,
Ukienda hapa http://politics.nationmedia.com/
Panaonyesha matokeo yanatoka mikoa mitatu so far, Nyanza, Rift Valley na Central. Sijui mgawanyiko wa Nairobi ukoje, lakini wapiga kura wa Nairobi ni wachache sana. Tuombe Mungu Central kuwe na wapiga kura wachache waliojitokeza, lakini kama wakiwa wametoka kwa wingi kama nilivyosikia BBC, Central inaweza kumbeba sana Kibaki. Sijui influence ya Raila kwenye ya Coast na Eastern.
Lakini tuvute subira mpaka dakika ya mwisho tuone, japo nina matumaini makubwa sana na Raila. Nitasikitika sana iwapo Raila atasikitika.

Keil,

Nairobi watakuwa karibu nusu kwa nusu kati ya Raila na Kibaki kwahiyo hapo hakuna tatizo sana. Tatizo ni Central ambako kuna watu wengi sana. Nafikiri waliojiandikisha walikuwa milioni tatu.

Kitakachomsaidia Raila ni kwamba inaelekea anafanya vizuri sana Rift Valley ambako kuna watu wengi pia ukiachia kwao Nyanza.

Pia inaelekea Eastern Kalonzo anaanza kufanya vizuri, jambo ambalo ni zuri kwa Raila pia ili kupunguza kura za Kibaki.

Ukiachia hapo kwingine kote ni Raila, inaelekea Raila atashinda majimbo matano, Kibaki mawili na Kalonzo moja. Suala ni je hizo kura za central zitakuwa nyingi kiasi gani, kiasi cha kumfanya mzee arudi madarakani?

Hata kama wote 3 milioni wamepiga kura, kama idadi ya waliopiga kura ni 14M, basi bado Raila ana nafasi kubwa ya kupata kura za kutosha.
 
An exit poll by the Institute for Education in Democracy, a respected non-governmental organisation, gave the president 50.3 percent versus 40.7 for Odinga. But its figures were based on just 311 polling stations of a total of 27,000.

Hapa nakumbuka mambo ya Zenji, Dr Salmin na Seif. lakini mambo ni mazuto kwa mze mzima.
The unofficial results by the TV channels were compiled from tallies at counting centres. The latest, from KTN at 11 a.m. (8 a.m. British time), gave Odinga 1,370,938 votes to 916,804 for Kibaki.

Naamini hiki ni kipindi cha mageuzi makubwa ya kisiasa Afrika. Kuna upepo wa mabadiliko. Tutarajie mambo makubwa zaidi katika nchi nyingi za Afrika. Matokeo mengine yanaweza yasitufurahishe lakini tujue kwamba sasa Waafrika (wakiwamo Watanzania) wana mwamko mkubwa na wanapenda mabadiliko na tujue kwamba "La kuvunda halina ubani"
 
Zitto,
Ukienda hapa http://politics.nationmedia.com/
Panaonyesha matokeo yanatoka mikoa mitatu so far, Nyanza, Rift Valley na Central. Sijui mgawanyiko wa Nairobi ukoje, lakini wapiga kura wa Nairobi ni wachache sana. Tuombe Mungu Central kuwe na wapiga kura wachache waliojitokeza, lakini kama wakiwa wametoka kwa wingi kama nilivyosikia BBC, Central inaweza kumbeba sana Kibaki. Sijui influence ya Raila kwenye ya Coast na Eastern.
Lakini tuvute subira mpaka dakika ya mwisho tuone, japo nina matumaini makubwa sana na Raila. Nitasikitika sana iwapo Raila atasikitika.

Nyanza, Rift Valley na Central ndio wataamua Rais wa Kenya atakuwa nani. Mwanzoni niliamini Western itakuwa highly divided lakini kitendo cha Musikari Kombo kushindwa na pia Awori inaonesha Western yote imeenda ODM. Kama Raila atachukua Nyanza, Rift Valley na Western then atakuwa ameshinda. Coast nadhani imegawanyika, Mombasa Raila lakini maeneo ya Malindi na pwani kusini ni mchanganyiko sana maana hata Kalonzo anazo kura zake.

Kama mchangiaji mmoja alivyosema, inategemea sana turn out ya central na maeneo ya Kikuyuland. Eastern ni Kibaki na Kalonzo. Kalonzo Lower Eastern na Kibaki Upper. Unajua Eastern ni so vast.
Matokeo ya North Eastern yapoje? Wanaweza kuwa decisive hawa wasomali
 
Kwa tanzania hii inawezekana pia kupat wabunge ila electoral system yetu iko mikononi mwa serikali siyo kama hii ya kenya. Unakumbuka mwaka 1995 upinzani ulikuwa uchikue viti vyote vya Dar ila tume ilipoona vile ikaamuliwa kufuta matokeo yote. Tufanye kazi ya kuifanya tume yetu iwe huru. Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wasimamizi wa chaguzi majimboni, maana hawa huwa wanaambiwa kabisa kuwa jimbo likienda nawe huna kazi.
 
Matokeo ya North Eastern yapoje? Wanaweza kuwa decisive hawa wasomali

North Eastern wapiga kura ni wachache sana, wako kama 600,000 na sijui kama watakuwa wameenda wote kupiga kura. Nadhani ndiyo maana Nation Media wamewa-ignore kwenye data zao, ingawa inawezekana kupata results za huko zikawa ngumu kupatikana kwa sababu ya matatizo ya mawasiliano.

Tuendelee kusubiri, labda kitaeleweka ingawa tayari naona kimeishaanza kueleweka kwa kuwa mpaka sasa ODM wana viti 53 vya wabunge, wakati PNU ina viti 15 tu na Kalonzo (ODM-Kenya) ana viti 2 na Safina wana kiti 1! Hapo lazima Kibaki awe na kibarua cha ziada kwenye Bunge la Kenya! (Source: BBC na siyo official results)
 
leo nimeamini kwamba sisi Watanzania pia tuna mwamko wa kisiasa sana kwa jinsi ambavyo tunafuatilia na kupata matokeo ya nchi jirani!
Lets get it going in our side as well.... all the Best to Kenyans! Tuko pamoja K-T
 
sina hakika kama akishinda ye yote rafiki yangu Shy kama atakukumbuka !!! wewe wacha democrasia ifanye vitu vyake,hujasikia yule jamaa kwa Madiba alivyopiga bao pamoja na kurundikiwa mikesi !!!!
 
Sorry, North Eastern nayo imewekwa kwenye site ya Nation Media, so watu wanaweza kupata full picture ya matokeo jinsi ilivyo mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom