Kenya Airways, Mombasa harbour, Viwanda, reli za kenya wanapaa, while Tanzania ziiii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya Airways, Mombasa harbour, Viwanda, reli za kenya wanapaa, while Tanzania ziiii!

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by MPadmire, Jul 3, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Kenya Airways, Reli zao wameunganisha na Uganda, Bandari ya mombasa, viwanda vya kusindika matunda, Viwanja vya ndege n.k viko vizuri kiuchumi wakati sisi watanzania tumelala wajameni??

  Watanzania wengi wanaagiza magari na bidhaa na wanapitisha bandari ya Mombasa, why??? ukiritimba usio na sababu.

  Kenya Airways wamepanua biashara zao na wanaenda nchi nyingi duniani, sisi bado tunatambaa.

  Reli zao bomba.

  Mie naona hata kwenye Jumuiya ya Africa Mashariki tujiondoe kwanza hadi tutakapo pata watendaji wazalendo na hodari kwanza serikalini.

  Hata Rwanda wanatushinda jamani, mh

  Ndio sababu sio ufisadi tu bali hata uzembe na kubweteka?

  KWa sababu hata kenya kuna ufisadi lakini ni wajanja wanazalisha. Mfano ni sawa na mtu ana shamba la mnazi, badala ya kuhudumia minazi vizuri avune nazi, kwa watanzania hata ule mnazi unaachwa uliwe na mchwa au anakata minazi anauza kama mbao au anaumza shamba. Du kali hiyo.

  Wana jamii tuendelee kuwapigia hawa watu kelele.
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu mpadmire,
  Mimi huwa najiuliza swali sipati jibu sahihi, kwamba sisi waafrika tuna matatizo gani? Je ni laana gani tuliyonayo? Maana hata kama una rasilimali kama ilivyo kwa Tanzania lakini maendeleo hakuna. Iangalie Nigeria na utajiri wao wa mafuta na gesi lakini hali ni mbaya tu. Katika nchi za Kiafrika viongozi wanagombea nafasi ili wakajilimbikizie mali na si kuwasaidia wananchi wao. Ufisadi wa kutisha unaoambatana na mikataba ya kinyonyaji. Ukikuta nchi ya Afrika imeendelea lazima utakuta kuna mkono wa mzungu inatia uchungu sana. Angalia Afrika ya Kusini maendeleo waliyonayo ni kwa sababu ya wazungu na kama wangekuwa tu wazulu wangekuwa na hali mbaya sana.

  Ukija kwa upande wa Kenya, ni kwamba Kenya Airways inamilikiwa na KLM kwa asilimia 26 pia wako wawezezaji wengine wa ndani na nje. Kwa maana nyingine wana wawekezaji wenye uzoefu mzuri kwenye sekta hiyo. Kumbuka pia kuwa Kenya lilikuwa koloni kwa ajili ya makazi kama ilivyokuwa Zimbabwe kwahiyo wazungu wameweka base kubwa Kenya na hata wamiliki wa mashamaba makubwa yenye rutuba huko ni wazungu, wananchi wa kawaida wanateseka hawana ardhi ya kutosha yenye rutuba. Viwanda vingi pia vinamilikiwa na wazungu wakati kwetu hapa kuna wahindi ambao ni wezi na matapeli wasiotaka hata kulipa kodi na viongozi wetu wanacheka nao tu. Pia international organizations nyingi ziko Kenya yote haya yanachangia maendeleo yao. Bandari ya Mombasa, reli na barabara nzuri pia kwa kiasi kikubwa zianchangiwa na biashara za wazungu huko Kenya.

  Ni wakati wa viongozi wetu sasa kubadili nia zao na kumrudia MUNGU waache ufisadi waonyeshe uzalendo kwa nchi yao ili taifa letu lipate kupona.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  ILI TUENDELEE TUNAITAJI VITU VITANO,

  1:WATU (WATANZANIA_WAAFRIKA)

  2:ARDHI

  3: SIASA SAFI

  4: UONGOZI BORA na

  5: MZUNGU
   
 4. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Tuendelee kuwa na Kenya, tujifunze kupanga mipango-uchumi makini ya maendeleo na kujitegemea kutoka kwao. Kujitenga hakuwezi kutusaidia.
  Karagebaho
   
 5. m

  msabato masalia Senior Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo kwenye No.5 ndo panausika,ila najua watu watanishambulia kama ashambuliwavyo RA au EL ila kusema nakuleta mifano ya Botswana, ukweli ni kwamba :mad:kwenye kujali nchi yetu,watanzania tumefulia except Dk.SLAAAAAAAA
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  sijawahi kuona nchi iliyoendelea kutokana na investments za wahindi ukiacha india yenyewe. Sasa ajabu CCM yetu inakumbatia watu ambao wanahifadi pesa zao canada.....Nadhani CCM na watu wake ni vichaa.....sina hakika
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hakuna anayesema tujitenge na jirani zetu, nadhani mtoa thread anaonyesha hasira kwamba kama wenzetu wametuzidi kiasi hicho hatutaweza kwenda nao sambamba inabidi tujiandae then twende sawa
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kama kweli tunataka kujifunza na kuratibu maendeleo yetu mahali pa kuanzia kujifunza na kujifananisha na kujiona sisi tuko mkiani siyo Kenya.
  Wakenya wanajitahidi sana lakini siyo nchi iliyomfano wa kuigwa na Watanzania.
  Tuna nchi nyingi za dunia ya kwanza ambazo zina mambo mengi tuwezayo kujifunza na kutengeneza utaratibu wetu wenyewe.
  Wachina walizinguliwa na maendeleo ya 4 Tigers, lakini walipo azimia kubadili mambo walifunza kutoka Dunia ya kwanza.
  Watanzania tuna hamu moja tu kujaza mapesa mifukoni mwetu kwa kuuza sehemu ya Uhuru wetu na urithi wetu mkuu, Ardhi.
  Hatuwezi kuendelea kupona njaa kwa kujitafuna viungo vyetu wenyewe.
  Sisi wananchi hatuna hamu ya kujenga nchi.
  Viongozi wetu walio sehemu yetu pia hawana hamu ya kjenga nchi.
  Kila mtu katika umoja wake anadhani akishiba yeye, barbara zitajijenga, uchumi utajipiga fimbo, nidhamu ya kazi itajisimika yenyewe zaidi taifa litasonga mbele bila mawaa.
   
 9. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tanzania pia tunayo reli ambayo tumeiunganisha na Zambia, na kuna wazambia wengi tu na wacongo wanatumia bandari yetu kuagiza magari. reli ya tazara imeeenda hadi kaprimposhi zambia. tatizo ni nini kwani? ni kwasababu hatujaunganisha na uganda kama walivyofanya kenya? au ni ubovu wa reli?

  Reli mbovu tz ni reli ya kati, reli ya tazara ni nzuri na inaridhisha at least. kwa habari ya bandari, nakubaliana na wewe, viongozi wetu hawana akili, kichwani wamejaa ukoko. wanachowaza ni kwenda tu kuzindika uchawi wao wa zindiko la taifa kule Lindi, na kuzindika ili waendelee kuwepo madarakani, lakini sio kufanya mambo mazuri ili wa prove kwamba wamefanya kitu katika uongozi wao. hakika muda umefika, watz tunatakiwa kuwaondoa hawa viongozi na ikiwezekana na chama chao kabisa cha ccm. hapo ndo uponyaji wetu, kwasababu tunaumia, tunateseka, hatuendelei, na tunapigwa changa la macho kama watoto. ukiona wamevaa mavazi ya kijani, hadi kwenye damu yao ni damu ya kijani, fikiri wewe ni daktari unamfanyia mtu operation unakutana na damu za kijani?| hahahah utakimbia sana. hivyo ndivyo walivyo viongozi wetu wanaodumisha chama chao. Mungu awasamehe lakini awaondoe madarakani kwa namna yoyote ile hata ya kuwapiga pressure tu. tumechoka kwakweli, na watu mtaani wamechokaaaaa.
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Siasa safi( weka upinzani)
  Uongozi bora( katiba mpya)
  Mzungu (Masoko)
   
 11. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani mambo mengine muwe mnanyamanza maana hii post imeniumiza sana yaani sisi tumefulia sijui tumemkosea nini Muumba.
  Wachina na wahindi ndo wamejaa na wahindi wengi sio wazalendo kila kukicha wanaenda kwao na kurudi.,wachina wanaleta bidhaa zao kwanini wasijenge viwanda?
  Alafu kwanini wawe Wachina,wahindi na Warabu why not Wazungu (wajerumani , warusi na wajapani ) ?
  Ndo maana sipendi siasa sichelewi kukasirika.
   
 12. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kituko,

  Badala ya MZUNGU, naamini KIONGOZI BORA, MZALENDO ANAYETUMIA KIBOKO angetuondoa ktk matatizo ya kutopiga hatua mbele.
   
 13. m

  mwashiuyad New Member

  #13
  Jul 5, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahi kusikia watanzania wako makini na vitega uchumi vyao,

  Ndugu Mpadmire Nakupongeza kwa Mada yako .
  Kimsingi watanzania bado tunajiona wajanja huku mali zetu zikiliwa na wachache walopo madarakani,Inauma sana kuona kodi zetu zinatumiwa hovyo!, rasilimali kama reli,bandari vinatumika kwa maslahi ya mtu tena yeye na familia yake ndo wanaongoza rasilimali za Taifa lenye watu zaidi ya milion 32.
  Tunahitaji heshima na busara katika kutumia mali za uma.

  Ni hayo Tu!!
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Niwaambieni ukweli. Wakenya si Bomba sana kutuzidi sisi. Wao na sisi ni dugu moja. Hizo mali unazoiona, Wakenya wa kawaida wanafanya window-shoping.

  Ili tuendelee ni kitu kimoja chahitajika. RULE OF LAWS. Wengine kama Peter Tosh wanasema EQUAL RIGHT and JUSTICE. Utaenda kushoto, utaenda kulia ila huo ndiyo ukweli wenyewe.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  We Tanzanians can talk the talk but rarely walk the walk. We have many plans which look good on paper but the problem is implimentation and maintenance. We also have the problem of coming up with impractical solutions to our problems. Our leaders make promises which they forget soon after being elected. We lack leaders who are visionaries and the wananchi lack incentives to contribute they talents, skills and interests in to the economy. We are called the "sleeping giant" of East Africa everyday but if we don't wake up soon we will realize that we are the dwarfs of East Africa. Tanzania has potential but the problem is fulfilling that potential.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tunahitaji vision na kuacha uvivu.
   
 17. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  'Sup Mwana,
  East Africa as a whole has great potential, this is seen in the way we conduct our businesses, how we manage to make it in life though the odds are usually against us, that is why I usually support the EAC. Two heads are better than one, we can develop faster if we unite as one, we all have our strength and weaknesses and we can complement each others strength and look for a way around our weaknesses.

  Lets embrace this chance and join hands to form the community which will be of great benefit to us and generations to come. Thats the only way forward, the decision our leaders make today will affect our lives forever.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I'm seeing your point bro. Let as hope our leaders will put aside greed and come up with something that can work for all of us. The only problem I have with our leaders is that they tend to think of their offices and pockets before the rest of us. I truly believe that if done in a proper way the EAF will benefit all of us. Let's keep praying that our leaders come up with something that will work.
   
 19. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ili tuendelee tunahitaji.

  1. Tanzania bila ccm.
  2. Fisadiless tanzania
  3. Tanzania with few indians..!
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hiyo number tatu sijui kama itatusaidia kwa dunia ya leo, Indians are very easy people to control if you have good laws..mbona wako UK,US wanafanya vema kwasababu sheria zinasimamiwa na wazalendo vizuri..I don't support the idea of leballing and generalizing crime to the entire group of people in the society...wengine wamezaliwa pale kisutu miaka mingi sana...itakuwa ngumu..wengine ni wazalendo kwa matendo yao mengi..wengine ni majizi (Mafisadi) ha ndio tuwa identify..kwa sheria nzuri..
   
Loading...