Kelele za mfumo dume hazisikiki tena

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Ni kama vile zimekufa kifo cha asili. Kelele za Uwakilishi wa 50/50 kwenye nafasi mbalimbali za uongozi nazo zimetokomea kizani.

Misemo maarufu ya wanawake wanaweza haisikiki tena! Huu ni wakati wao sasa. Na hakuna wakati mwingine zaidi ya huu. ITS NOW OR NEVER!

No wakati wa kuthibitisha kwa vitendo sasa slogans za #wakiwezeshwa wanaweza! #wanawake na maendeleo. Nknk!

Ukisoma historia ya Afrika wanawake walikuwa watawala na baadhi yao walikuwa majemadari hodari wa vita na wakafanya vema sana.

Hapo katikati mambo yaliyumba kidogo, mpaka ulipofanyika mkutano wao maalum mnamo mwaka 1994 hapo Beijing China ndio mabadiliko mbalimbali yakaanza kufanyika ili kuleta usawa wa jinsia kwenye ushiriki wa shughuli za maendeleo na nyadhifa za kisiasa na kiutawala

Miaka chini ya 30 ni kama bahati ya mtende imewaangukia.. Pengine mkutano ule wa Beijing umechagiza pakubwa sana kwenye hili.. Sasa uwanja ni wao hatutaki hadithi tena tunataka MATOKEO MAKUBWA SASA!

Kama mfumo dume ulichewesha maendeleo, tunataka kuona cheche za mfumo jike.

Kama mfumo dume ulijaa unyanyapaa, tunataka kuona mfumo jike ukimaliza hilo tatizo.

Kama mfumo dume ulishindwa kuleta haki sawa kwenye jamii, tunaanini mfumo jike hautarudia hilo kosa!

Wanasema kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanaume! Sasa kwasasa wako mbele. Tunataka matokeo makubwa sasa.

Mmewezeshwa wezeni sasa! Hatutaki kuona vijembe, husuda, wivu, majungu, masengenyo, kuchafukwa wala makasiriko yasiyo na msingi. Hatutaki kuona ya Cleopatra yakijirudia. Tunataka kuona kazi ikiendelea

Msibaguane kwa misingi ya itikadi,vyama, imani, uwezo, ukwasi, asili, ukabila,ukanda na mambo yote yanayofanana na hayo. Mkishindwa sasa mtashindwa milele. Mkiweza sasa mmepanda mbegu bora

Sisi tupo tu hapa tumevuta hand break. Tunakula mtori taratibu nyama tutazikuta huko chini naamini.

giphy.gif
 
Upande wao wa pili inaaminika huwa hawapendani. Hawakawii kuanza kucharurana wao kwa wao.

Na kila kitu kinatisha ukiwa unakifanya kwa mara ya kwanza, inaweza ikakukuta hali ya kutokujiamini (Imposter syndrome). Mwenyezi awaepushie mbali na hayo.
 
(Imposter syndrome).
 
Mm binafsi yangu nawaunga mkono Wanawake kwenye suala zima hili LA utawala na uongozi.

Wacha wafanye kazi,wacha wachape kazi.Wanawake hawana nongwa makazini kama UTAWAHESHIMU na kufata TARATIBU ZA KAZI.

Sisi wanaume tuna nongwa sana,tunapenda KUABUDIWA,kuonekana MIUNGU WATU hata ktk sehemu ambazo hazina maana yeyote.

Mwanamke akiwa boss wako MPE heshima yake tu basi utakuwa umemaliza kazi,usitumie uanamke wake kutaka kumuonyesha kuwa yeye si kitu,or si lolote wala chochote hapo utakuwa umechokoza vita kwa makusudi kabisa.

Kwa sasa Nchi imetulia,haina Mbwembwe, haina sifa za kijinga,haina ubabe wa kipumbavu wala haina mikurupuko.Full amani full respect.

Tuachie nizamu yao sasa waonyeshe walichonacho.mana sisi wanaume miaka na mikaka hakuna cha maana tunachofanya zaidi ya kujimwambafai tu basi.

Ngoja tuone mawazo na fikra Mpya zitatufikisha wapi!??

Go Go Go
Mama Samia..
Go Madam President..
We Love you Mama..
 
Now tuna kelele za Mfumo Jike, Nimezingatia kichwa cha Maada , Haabari sijaisoma kwa ujumla
 
Back
Top Bottom