Angalia kwenye picha mkono wako wa kushoto - huo ni ukumbi wa mikutano na sherehe wa Diamond Jubilee. Kuhusu rangi kumbuka tuna watanzania wenye asili ya asia wengi tu hapa Dar es salaam na ndio walioshiriki shughuli hii kwani inahusu dhehebu lao.
Mie niliona jana ilioneshwa na ITV. Hapo Dar Jumuiya ya Mabohora walikuwa wanasherehekea miaka 100 ya kiongozi wao. Hiyo keki pia ilipewa umuhimu kwa kuelezewa kwamba ina uzito wa kg. 100.