KCMC yajenga wodi ya majeruhi wa pikipiki

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
16,940
24,499
HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC imelazimika kujenga wodi nyingine ya wagonjwa maalumu kwa ajili ya wanaopata ajali za pikipiki ili kutoa nafasi kwa wagonjwa wengine kutumia wodi za kawaida zinazotumiwa sasa na majeruhi wa bodaboda.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini linalomiliki hospitali hiyo, Dk. Martin Shao alisema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa saba wa jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro.

Alisema hatua hiyo inafuatia majeruhi wa ajali za pikipiki ambao baadhi yao hupata ulemavu wa kudumu, kukaa muda mrefu hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu huku baadhi ya wagonjwa wa maradhi mengine wakikosa nafasi ya kuhudumiwa ipasavyo.

Dk Shao alikuwa akizungumzia ajali ya meli ya mv Spice Islander iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200, alisema baadhi ya ajali nchini zikiwamo za pikipiki husababishwa na uzembe wa madereva na baadhi ya mamlaka zinazosimamia vyombo vya usafiri.

Askofu Shao alisema pamoja na mipango ya Mungu lakini vyanzo vya ajali nyingi ni uzembe wa madereva jambo ambalo linapaswa kufuatiliwa kwa kina na serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ili kuepusha mamia ya watanzania kupoteza maisha.

Alisema ipo haja kwa serikali kuchukua hatua kali za kisheria kwa baadhi ya watu wanaobainika kufanya uzembe kwa namna moja au nyingine na kusababisha vifo vya mamia ya Watanzania wasio na hatia.

“Mara zote tumeshuhudia vyombo vinavyosimamia usafiri vikijadili na kutoa matamko kwa wamiliki na madereva wa vyombo vinavyotumia barabara lakini usafiri wa maji na anga huwa haujadiliwi sana...kuna kila sababu kujitathmini upya,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya KCMC, Dk. Moshi Ntabaye alisita kuzungumzia taarifa hiyo ya Askofu Shao lakini alikiri kuongezwa kwa wodi tatu hospitalini hapo.

“Kwa sasa sipo tayari kuzungumza na waandishi wa habari kwa simu, maana kuna mwandishi nilizungumza naye (Siyo wa HabariLeo) lakini alipokwenda kuandika aliongeza vitu ambavyo sikumueleza,” alisema.

Mmoja wa wauguzi aliyepo hospitalini hapo ambaye aliomba asitajwe kwa kuwa siyo msemaji alisema kwa sasa hospitali hiyo imeongeza wodi tatu kubwa zikiwamo za walioungua, majeruhi na ngozi ambazo ujenzi wake unafuatia msongamano wagonjwa.

Awali kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kilimanjaro, Peter Sima alisema ajali za pikipiki zimeongezeka mkoani humo ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2010 walikufa watu 29 na majeruhi 113.

Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu waliokufa ni 39 na majeruhi 151 ambapo ni wastani wa watu wanne kufa kila siku huku wastani wa watu 17 kujeruhiwa kila siku.

“Ajali za pikipiki ni kubwa…majeruhi wote wanalazwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi na rufaa ya KCMC, hata hivyo tumetoa elimu kwa waendeshaji wa pikipiki ikiwemo kukamata madereva 17,762 na wengine 286 wamefikishwa mahakamani,” alisema.

Kwa upande wa ajali za vyombo vingine vya usafiri yakiwamo magari kwa kipindi cha mwaka Januari hadi Septemba 2010 zilitokea ajali 932 na waliokufa ni 123 na ajali hizo kwa Januari/Septemba 2011 zilitokea ajali 937 na waliokufa ni 170 na majeruhi 666.


Source. Habarileo.

Duh hizi Toyo zitatumaliza nashauri hiyo wodi iitwe Toyo wadi.


 

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
625
Mimi nakuwa sielewi kabisa, hawa jamaa wa bodaboda wakisikia habari kama hizi wanajisikiaje. Siamini kama wanapenda kufa ila nikiwaona wengine wanavyoendesha, ni wazi wanapenda kufa.

OK, kazi kwao....
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
16,940
24,499
Mkuu Mrimi.

Tatizo la Tanzania siku zote hawangalii chanzo cha tatizo ndiyo maana ndugu zetu afya wamekimbilia kujenga wodi jeshi la polisi hawana habari kabisa.Siku hizi ukipelekwa Mt Meru kwa case ya kuvunjika swali la kwanza ni ajali ya Toyo au !!!!!.


Mimi nakuwa sielewi kabisa, hawa jamaa wa bodaboda wakisikia habari kama hizi wanajisikiaje. Siamini kama wanapenda kufa ila nikiwaona wengine wanavyoendesha, ni wazi wanapenda kufa.

OK, kazi kwao....
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,863
4,784
ukipelekwa moi bora useme nimegongwa na gari. Ikifahamika ni toyo,wale jamaa hawajigusi kuumiza kichwa namna ya kupanga mifupa. Wanakata mguu aafu wanakudischarge ukaponee hom
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
9,764
9,147
dah aisee hata mitaani vijana wanapungua kwa kufa kwa ajali,pia ukiwaona wanavyoendesha unaona hawa bora waanguke na kuvunja miguu
nasikia sikuhizi ukinunua toyo unapewa na magongo for free
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
24,205
20,911
Toyo ndiyo piki piki wakuu?Nakubaliana na wewe Ngongo.Kujenga hospitals specifically for motorbikes accidents ni kuangalia ulipoangukia badala ya pale ulipojikwaa.
 

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,850
861
Toyo ndiyo piki piki wakuu?Nakubaliana na wewe Ngongo.Kujenga hospitals specifically for motorbikes accidents ni kuangalia ulipoangukia badala ya pale ulipojikwaa.

kwani hawa waendesha pikipiki wanaelewa sasa? Wanatoka kumzika mwenzao aliyegongwa akikimbiza pikipiki, lakini hawajifunzi,wanaendesha kwa fujo, kwa sifa, na kwa kutofata sheria...dawa ni kuwajengea wodi yao tu hawa!
 

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,650
586
kwani hawa waendesha pikipiki wanaelewa sasa? Wanatoka kumzika mwenzao aliyegongwa akikimbiza pikipiki, lakini hawajifunzi,wanaendesha kwa fujo, kwa sifa, na kwa kutofata sheria...dawa ni kuwajengea wodi yao tu hawa!

Kama hivyo ndivyo; dawa ni kuwajengea wodi au kuwachimbia makaburi?
 

Black Devil

Member
Mar 16, 2011
58
8
Mkuu Ngongo,

Tatizo la Tanzania ni mfumo mzima.
1. Barabara hazina ugao wa matumizi- baiskeli, Toyo wala Miguu Hamna. Ni magari pekee Kama mkoloni alivyo acha.
2. Madharau kwa wandesha magari kwa Toyo.
3. Toyo inavuta stimu, unavyozidi kukoleza ndo nyege Zake zina Panda...

Mkuu Mrimi.

Tatizo la Tanzania siku zote hawangalii chanzo cha tatizo ndiyo maana ndugu zetu afya wamekimbilia kujenga wodi jeshi la polisi hawana habari kabisa.Siku hizi ukipelekwa Mt Meru kwa case ya kuvunjika swali la kwanza ni ajali ya Toyo au !!!!!.
 

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,436
Basi hii ni hatari sana ,kweli haya mambo yanatokea ama ni uzushi.?
ukipelekwa moi bora useme nimegongwa na gari. Ikifahamika ni toyo,wale jamaa hawajigusi kuumiza kichwa namna ya kupanga mifupa. Wanakata mguu aafu wanakudischarge ukaponee hom
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
9,764
9,147
Basi hii ni hatari sana ,kweli haya mambo yanatokea ama ni uzushi.?[/QUOTE
ni kweli mkuu nimeona hii kwa macho yangu,ni kwamba siku hizi ukipata ajali yoyote pale moi wanaona ni pikipiki tu,na ni rahisi sana kujikuta huna mguu
Kuna jamaa pale yupo maalum kwa ajili ya kuchukua oda ya magongo wakishafyeka mguu
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
16,940
24,499
Mkuu Nyalotsi hii nadhani liko hospital zote Mt Meru ukisema umepata ajali ya Toyo allocation ya akitanda na kumwona mtaalamu wa mifupa inakuwa taabu kabisa nimeshuhudia jamaa yangu aliuvunjika mguu nakwambia kuanzia mhudumu,nesi hadi madakatari hawakuwa na muda wa kumuhudumia zaidi ya masimamgo "Toyo zitawamaliza".


ukipelekwa moi bora useme nimegongwa na gari. Ikifahamika ni toyo,wale jamaa hawajigusi kuumiza kichwa namna ya kupanga mifupa. Wanakata mguu aafu wanakudischarge ukaponee hom
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,777
4,625
ukipelekwa tu pale wanauliza ajali ya nini wakisikia tu sanlg kaumia nni mkono utasikia kaaaata mkono
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,288
16,244
dah aisee hata mitaani vijana wanapungua kwa kufa kwa ajali,pia ukiwaona wanavyoendesha unaona hawa bora waanguke na kuvunja miguu
nasikia sikuhizi ukinunua toyo unapewa na magongo for free

hahahaaa nayo inakuwa free kama helmet aisii
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,546
5,674
Hawa jamaa wanaoendesha hizi bodaboda sijui wana roho za aina gani. Kila siku kunatokea ajali za pikipiki, zinaua na wengine wanapata ukilema wa maisha. Lakini bado hawajifunzi..Kujenga wodi maalumu kwa ajili ya wahanga wa bodaboda hiyo sio suluhisho. Lazma jeshi la polisi liamke ktk hili.
 

jameeyla

Senior Member
Aug 12, 2011
119
29
hii ni kweli nafikiri chanzo cha tatizo kwanza hizi TOYO hazina ubora unaotakiwa yaani serikali wamekubali kuyaingiza haya mapikipiki sijui kwa ajili ya vigezo gani,pili waendesha pikipiki hawana vifaa vya kujikinga kwa ajali-HELMET za kichina yaani ukianguka nayo badala ya kukulinda wewe usiumie yenyewe ndiyo inakuwa ya kwanza kukupasua kichwa,,hebu turudi enzi za HONDA kweli na HELMET zake kwanza kama huna nguvu ya kutosha huwezi kuiendesha na kofia yake pia ni ya kuziba kichwa kizima mpaka shingo na ukipata ajali nayo basi ukipona mshukuru mungu, kuliko hizi ajali za kila siku tukifanya tathmini ya haraka inawezekana baada ya miaka 3 mbele taifa likawa na vilema wengi na hii kupunguza ujenzi wa taifa kwa kiasi kikubwa.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom