Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,895
- 31,106
HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC imelazimika kujenga wodi nyingine ya wagonjwa maalumu kwa ajili ya wanaopata ajali za pikipiki ili kutoa nafasi kwa wagonjwa wengine kutumia wodi za kawaida zinazotumiwa sasa na majeruhi wa bodaboda. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini linalomiliki hospitali hiyo, Dk. Martin Shao alisema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa saba wa jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro. Alisema hatua hiyo inafuatia majeruhi wa ajali za pikipiki ambao baadhi yao hupata ulemavu wa kudumu, kukaa muda mrefu hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu huku baadhi ya wagonjwa wa maradhi mengine wakikosa nafasi ya kuhudumiwa ipasavyo. Dk Shao alikuwa akizungumzia ajali ya meli ya mv Spice Islander iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200, alisema baadhi ya ajali nchini zikiwamo za pikipiki husababishwa na uzembe wa madereva na baadhi ya mamlaka zinazosimamia vyombo vya usafiri. Askofu Shao alisema pamoja na mipango ya Mungu lakini vyanzo vya ajali nyingi ni uzembe wa madereva jambo ambalo linapaswa kufuatiliwa kwa kina na serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ili kuepusha mamia ya watanzania kupoteza maisha. Alisema ipo haja kwa serikali kuchukua hatua kali za kisheria kwa baadhi ya watu wanaobainika kufanya uzembe kwa namna moja au nyingine na kusababisha vifo vya mamia ya Watanzania wasio na hatia. Mara zote tumeshuhudia vyombo vinavyosimamia usafiri vikijadili na kutoa matamko kwa wamiliki na madereva wa vyombo vinavyotumia barabara lakini usafiri wa maji na anga huwa haujadiliwi sana...kuna kila sababu kujitathmini upya, alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya KCMC, Dk. Moshi Ntabaye alisita kuzungumzia taarifa hiyo ya Askofu Shao lakini alikiri kuongezwa kwa wodi tatu hospitalini hapo. Kwa sasa sipo tayari kuzungumza na waandishi wa habari kwa simu, maana kuna mwandishi nilizungumza naye (Siyo wa HabariLeo) lakini alipokwenda kuandika aliongeza vitu ambavyo sikumueleza, alisema. Mmoja wa wauguzi aliyepo hospitalini hapo ambaye aliomba asitajwe kwa kuwa siyo msemaji alisema kwa sasa hospitali hiyo imeongeza wodi tatu kubwa zikiwamo za walioungua, majeruhi na ngozi ambazo ujenzi wake unafuatia msongamano wagonjwa. Awali kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kilimanjaro, Peter Sima alisema ajali za pikipiki zimeongezeka mkoani humo ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2010 walikufa watu 29 na majeruhi 113. Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu waliokufa ni 39 na majeruhi 151 ambapo ni wastani wa watu wanne kufa kila siku huku wastani wa watu 17 kujeruhiwa kila siku. Ajali za pikipiki ni kubwa majeruhi wote wanalazwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi na rufaa ya KCMC, hata hivyo tumetoa elimu kwa waendeshaji wa pikipiki ikiwemo kukamata madereva 17,762 na wengine 286 wamefikishwa mahakamani, alisema. Kwa upande wa ajali za vyombo vingine vya usafiri yakiwamo magari kwa kipindi cha mwaka Januari hadi Septemba 2010 zilitokea ajali 932 na waliokufa ni 123 na ajali hizo kwa Januari/Septemba 2011 zilitokea ajali 937 na waliokufa ni 170 na majeruhi 666. Source. Habarileo. Duh hizi Toyo zitatumaliza nashauri hiyo wodi iitwe Toyo wadi. | |