Asilimia 94 ya majeruhi wanaopokelewa MOI wanafika kwa kuchelewa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Imebainishwa kuwa asilimia 94 ya majeruhi wa mifupa na ubongo hupokelewa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) masaa sita baada ya kutokea kwa ajali kinyume na viwango vya kimataifa vinavyotaka majeruhi kufikishwa hospitalini hapo ndani ya saa moja ili kuokoa maisha yao.
25f6ecb0-fb6a-4620-a9d6-40dbcfdf7bc5.jpg

878ea967-7383-4ea5-89c2-8fca0275475b.jpg

Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha kimkakati baina ya MOI na hospitali ya za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kwa lengo la kuboresha huduma kwa majeruhi wa mifupa ,mgongo na ubongo.

Katika kikao hicho kilichofanyika MOI kwa lengo la kuboresha matumizi ya ‘saa la dhahabu’ inayomtaka majeruhi kupata matibabu ya uhakika ndani ya saa moja tangu kutokea kwa ajali.

Mkuu wa kitengo cha utafiti MOi Dkt.Joel Bwemelo amesema kuchelewa kufikishwa majeruhi hospitalini hapo kunapunguza uwezekazo wa kunusuru maisha yao.
ce700db8-df72-46a2-a916-31a818b7b612.jpg

5b2c2215-7efa-475b-bd85-a4a9d5dc98d6.jpg

“Kuna saa moja la dhahabu linaloweza kuokoa msiaha ya majeruhi tangu ajali itokee…hapa MOI asilimia 94 ya majeruhi huja masaa sita tangu kutokea kwa ajali, wakati huu ule muda wa saa la dhahabu la kuokoa maisha yake huwa limepita”

Kwa upande wake Dkt. Anthony Assey amesema miongoni mwa sababu za kucheleweshwa kwa majeruhi kufika MOI ni pamoja na utaratibu wa rufaa unachokua muda mwingi na kwamba kikao hicho kinalenga kuboresha mfumo wa rufaa ili kuwawahisha wangonjwa kufika.

“Kitu cha msingi kabla ya kumrufani majeruhi, hakikisha umemuhidumia na amekuwa stahimilivu (stabilize), tukumbuke kuna suala la barabara zetu, foleni, hivi vyote vinahitaji kuzingatiwa kwa kumuandaa majeruhi kuweza kuhimili hali hiyo ili asipate athari za pili” amesema Dkt. Assey

Naye mratibu wa kikao kazi hicho Dkt. Bryson Mcharo amesema lengo ni kuondoa changamoto zinazozuia majeruhi kupatiwa matibabu ndani ya saa moja tangu kutokea kwa ajali.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana Dkt. Bryson Kiwelu ameipongeza MOI chuni ya utaratibu mpya utakaowawezesha kumpa rufaa majeruhi kwenda MOI moja kwa moja bila ya kupitia hospitali zingine.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Laurent Lemery amesema kikao hicho kinalenga kutetekeleza sera ya wizara ya afya ya kuboresha utoaji huduma na hasa kwa wagonjwa wanaopata rufaa kwa ajili ya kuja MOI kwa matibabu zaidi.
73c8f84a-4f53-46e5-9534-c00a8a1a7039.jpg
 
Back
Top Bottom