KCMC inapokea Wagonjwa 300 wa Akili kwa mwezi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Daktari bingwa wa afya na magoniwa ya akili wa Hospitali ya Rufani ya Kanda ya KCMC, Dk. Editruda Gamassa, amesema hivi sasa wanapokea wagonjwa wa nie wenye matatizo ya afya ya akili, zaidi ya 300 kwa mwezi mmoja. Magonjwa ya afya ya akili ambayo ni tishio nchini ni Kihoro (Anxiety), Sonona (Depression), PTSD-Trauma (Post Traumatic Stress Disorder), Baipola (BPD), Skizofrenia na Uraibu.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, wakati wa kikao cha kushirikisha wadau matokeo ya mradi wa afya ya akili, uliotekelezwa kwa miezi sita na Shirika la Kilimaniaro Women Information Exchange and Community Organization (KWIECO) katika Kata za Uru Kusini, Uru Mashariki na Kibosho Kindi katika Wilava ya Moshi, Dk. Gamassa alisema kutokana na ongezeko hilo la wagonjwa wa afya ya akili, kwa sasa wanalazimika kutoa huduma ya kliniki mara mbili kwa wiki.

Kwa mujibu wa Dk. Gamassa, hospitali ambazo zinatoa huduma ya kliniki va afya ya akili kwa wagonjwa wa nje katika Mkoa wa Kilimanjaro ni Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) na KCMC.

"KCMC kwa mwezi, huwa tunawaona na kuwahudumia wagoniwa hadi 300 Kama wagonjwa wa nje, kwa sababu kliniki tunafanya mara mbili kwa wiki na tunawaona wagonjwa wa aina mbalimbali, wenye matatizo ya afya ya akili kuanzia magonjwa kama ya sonona, wasiwasi au hofu iliyopitiliza, skizofenia, baipola na pia watu wenye matatizo ya uraibu, hasa utumiaji wa vilevi kama pombe, bangi na wachache wanaotumia dawa za kulevya kama heroine.

"Kwa wa upande wa matibabu, sana sana tunatoa huduma kwa wagonjwa wa nje, yaani matibabu kwa aina ya dawa kulingana na ugonjwa alionao na tunatoa huduma za kisaikolojia, tiba za saikotherapia (tiba ya maongezi); na pia tunatoa tiba ya vitendo," alisema Dk. Gamassa.
 
Mashabiki wa timu fulani watakuwa wengi sana hapo maana msimu huu wamepitia magumu mengi!!!
 
Watanzania wengi ni wagonjwa wa akili kwasababu ya ugumu wa maisha na wanaosababisha haya yote ni wajanja wachache wanaoishi kama wako peponi kwasababu ya kula rushwa kwenye usimamizi wa rasilimali za nchi tumechoka kuona wachache wanafaidi bandari iwekezwe tufaidi wote.
 
Back
Top Bottom