Kazi zenye pesa zisizojadiliwa na vijana hizi hapa

Suala la kutapisha vyoo umenichanganya..maana kama huna zile gari za maji taka cjui utavutaje...au nyie ndio wale mnaosubir mvua inyeshe afu ndio mnafungua machember mpaka tunakanyaga maji machafu
 
Hiyo pesa ya kusajili na kufungua Kampuni wataitoa wapi hao Vijana, wakati CCM imewanyang'anya kila kitu na kuwaacha masikini wa masikini?
Kuibuka kwa hili GENGE KUBWA la mapambio, kutetea uozo na kusifu kwa ujira wa elfu saba na simu ya smartphone, ni uthibitisho wa hali halisi ya maisha ya vijana wengi kwa sasa, utapata picha hali waliyonayo vijana kwa sasa huko mitaani.

mr chopa karibu kwa ufafanuzi tafadhali!!
 
Mawazo mazuri sana ila tu angalizo kwa biashara yoyote ile inahitaji uvumilivu sana na kutokata tamaa, biashara mwanzo huwa inakuwa ngumu, maana unakuwa hauna base nzuri ya wateja.

Ila ukifanya kazi kwa uhakika au bidhaa yako au huduma zako zikiwa na kiwango kizuri, basi utasimama vizuri mda unavyoenda....
 
ukizibua choo bila kua na elimu ya uzibuaji utaloa mavi mkuu.
kila kazi inahitaji elimu, hata ufundi viatu usipokua na elimu yake utajichoma sana sindano.
Ha! ha! ni kweli. Ata kula kuna hitaji elimu sbb unaweza kosea ukaingiza chakula puani
 
Natumai hamjambo, kichwa Cha habari kinajieleza, Kuna kazi vijana wengi hawazijadili ila ukizizingatia unaweza ukatengeneza kampuni kubwa Tena yenye kuheshimika
1; Shoe care, hi inajumuisha kushona viatu vilivyochanika, mikoba, begi, nk, kung'arisha viatu na kufua viatu, Hakika, kwa mtaji wa elfu 50 unaheshimika mtaani na familia pia, Mimi nipo naifanya hii, sema nipo kijijini, natamani nipate mtu wa kuungana nae sehemu ya mjini, kwa siku huwa sikosi elf 7
2. Ku repair viti vya plastic na vombo vyote vitokanavyo na plastic. Hapa ukitaka utajirike haraka, tafuta eneo la kuhifadhia bidhaa za wateja wako, pia uwe na electronic drill nyembamba na zile waya laini zakwenye transformer za redio au hata wire mesh lain kwa kushonea viti, nakwambia wateja utawakataa, hili wazo nalifanyia kazi sema Sina nakosa mtu wa kuungana nae ili tuwe tunakimbiza kazi hiyo haraka
3. Kuchimba vyoo, na kutapisha vyoo. Kuchimba shimo la choo, futi inagharimu Tsh 7000 mpaka elf 10000 Sasa ukiwa na bidii, ukachimba futi 5 kwa siku, utalala njaa? Hapa kinachotakiwa, ili mheshimike, mnakuwa na ofsi yenu yenye bango kubwa likisema, TUNACHIMBA VYOO NA KUTAPISHA VYOO VILIVYOJAA KWA BEI RAHISI. Mnaweka na mawasiliano, kwasababu nyie Ni kampuni, mkipata kazi, mnagawanya majukumu, yaani Kama wanavyofanya kazi TANROAD na TANESCO. Hapa kampuni yenu itaheshimika na hakuna mtu wa kuwadhalau/ kuwakejeri
4. Kutengeneza vifàa vya michezo ya watoto. Mfano, gari zitokanazo na spoku za baiskeli/ pikipiki, gari za mabox na yeboyebe/ slippers, kuchonga puzzles kwa kutumia slippers, na vitu vingine vinavyovutia watoto. Nakwambia, wateja wapo hasa shule za English medium, pia mnatakiwa muwe kampuni ili bidhaa zenu ziwe na label kuzifanya ziheshimike zaidi. Kea atakaye penda mawazo yangu anataka tushirikiane, tafadhari njoo PM/ INBOX tujadiliane. Kwa mwenye pesa ila amependa mawazo haya/ wazo mojawapo, anaweza akatuunganisha vijana tutakaokuwa tayari ili tujikwamue zaidi. Note: UOGA WAKO NDIYO UMASIKINI WAKO
Safi kabisa...
Kuuza barafu
Kuuza karanga
Kuuza maji
Gardening
Kulima bustani...
 
Kuzifanya hizo kazi mjini inabidi uwe kauzu kwelikweli maana vinginevyo itakuwa akitokea mtu anayekufahamu unakimbia kwenda kujificha then badae unarudi tena kwenye ofisi na saa zote unakuwa mtu wa machale machale,yaani wasiwasi haukuishi
Ukifanya kazi kama hizo, huwezi kupata mke.. Nani atampenda kijana mtapisha vyoo? Hizo ni kazi za wazee waliokwisha jichokea.
 
Kuzifanya hizo kazi mjini inabidi uwe kauzu kwelikweli maana vinginevyo itakuwa akitokea mtu anayekufahamu unakimbia kwenda kujificha then badae unarudi tena kwenye ofisi na saa zote unakuwa mtu wa machale machale,yaani wasiwasi haukuishi
😂 😂 😂 😂 😂 ukishaamua kua na kazi kama iyo alaf ukawa hivyo hamna mahali utafika utaacha tu hiyo kazi kwani huyo mtu akikuona anakulisha au anakulipia kodi ya nyumba mjini tena akipita unamkaribisha na biznez kadi unampa kabisa amna kujishtukia.
 
sawa ila inataka roho ngumu sana hasa kwa vijana tuliozaliwa mjini
ukishaamua kua na kazi kama iyo alaf ukawa hivyo hamna mahali utafika utaacha tu hiyo kazi kwani huyo mtu akikuona anakulisha au anakulipia kodi ya nyumba mjini tena akipita unamkaribisha na biznez kadi unampa kabisa amna kujishtukia.
 
Back
Top Bottom