Vijana acheni tabia hizi na mjikite kutafuta pesa

Kiongozi Miongoni

Senior Member
Feb 6, 2021
197
255
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Tanganyika,

Kuna tabia ambazo zimekuwa hazipendezi miongoni mwa vijana na baadhi ya watu wazima na tabia hizo zinatakiwa kuachwa mara moja. Na miongoni mwa tabia hizo ni kama zifuatazo;

  1. Vijana kukaa kwenye saluni za kiume kwenye viti vya wateja kanakwamba wanataka kunyoa kumbe wapo wanaojulika mziki, kuangalia tv na kukaguliwa watu, nenda kazini kijana.
  2. Kuna tabia ya vijana wanakaa juu ya pikipiki za boda kama vile wao ni madreva, kumbe hawajui chochote na wahusika kumbe wapo huko wanacheza pull table. Ukitaka huduma wanakimbia kuwaita wahusika, nenda kafanye kazi.
  3. Kuna watu wanaenda kwenye viduka vya mangi mitaani wanaagiza soda au juice wanakaa mlangoni wankunywa, hii ni tabia mbaya inazuia wateja kupata huduma, kunywa nenda ufanye kazi.
  4. Kuna watu wanakaa stendi wanajiiita wapiga debe, huu ni upuuzi kila mtu anajua anapoenda. Matokeo ya kukaa kusubiria pesa ambayo haujaitolea jasho ni kuwa mwizi au teja, rejea vituo vingi vya mabasi mfano Mbezi na huko mikoani mateja ni wengi.
  5. Kuwatembele marafiki wakati wa kazi, mfano mtu anafanya kazi benki wewe unataka uende kumtembelea saa tatu kazini, nenda unafanyaje kazi zako.
  6. Unaamka unawaza kubeti, nenda ufanye kazi.
  7. Unatembea na watoto wa shule, kafanye kazi utaishia jela miaka 30.
  8. Unajifanya mbabe wa kila jambo, polisi wakikushika unaanza kuwasumbua wazazi wakutoe, tafuta kazi hata kibarua ufanye.
Ni msimu wa kilimo sehemu nyingi za Tanganyika, vijana jikiteni kwenye kilimo, lima 20×20 shamba la mahindi utapata faida kuliko kufanya hayo hapo juu.

Kazi hazipo lakini vibarua vipo!

Wasalaam.
 
Sisi majobless kama majobless, Betting ni mkombozi wetu. Tunakula,kuvaa,kulipa kodi na hanasa mingine juu ya Betting na tunalipa kodi mnoo kuliko hata wewe mtoa mada
Give us some respect buda juss respect!!!
 
Mkuu wanakaa hivyo kwa boda boda kuwinda day work saluni kujifunza

Any way iyo kazi unayo apo tuje tuifanye kwa weredi mkubwa
 
Back
Top Bottom