Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 559
Habari Wadau.
Naomba kufungua mazungumzo haya kuzungumzia Suala la Kazi za Kujitolea na Umuhimu wake sambamba na madhara yake unapochukulia kwa wepesi nafasi hizi pindi unapozipata. (Kutokana na uzi huu kutokuwa maandiko matakatifu, ninaweza kurekebishwa, unaweza kutoa mchango chanya na kutoa taarifa jengefu ili kusaidia kuwafumbua macho vijana wenzetu juu ya fursa za kujitolea hususan wanaosubiria Ajira rasmi na wanafunzi wanaokuwa likizo ndefu na fupi)
1.) KAZI ZA KUJITOLEA NI NINI?
Kazi za kujitolea zina maanisha kufanya Shughuli/kazi isiyotegemea malipo (Ujira/Mshahara) ambapo mtu anatoa muda wake kusaidia shughuli/kazi za kijamii, kupitia taasisi au mtu asiyehusiana nae.
Badala ya kutegemea malipo ya pesa (Ujira/ Mshahara) hupata uzoefu na kutengeneza Mtandao (Network) unaoweza kumsaidia katika kazi/taaluma yake hapo baadaye. Baadhi ya Taasisi kulingana na sera zao na majukumu husika hutoa Posho kidogo ya nauli kuwawezesha wafanyakazi wao wa kujitolea (Volunteers)
2.) UMUHIMU WA KAZI ZA KUJITOLEA!
Kazi za kujitolea zina Tija kubwa sana kuliko tunavyofikiria, hii ni katika pande zote BINAFSI, na KIJAMII.
KIBINAFSI : Mtu anayefanya kazi hizi za kujitolea hujiongezea ufahamu na ujuzi zaidi wa shughuli anayoifanya nje ya ajira rasmi, hii inaweza kuwa ni kupitia maombi binafsi ya kujitolea kwa nafasi husika, au kupitia maombi maalum yanayotumwa kwa niaba ya mhusika kupitia Taasisi za elimu ya Juu na Vyuo.( Field Work)
KIBINAFSI:
Hebu Fikiria kuwa umeenda kuomba nafasi ya kazi sehemu (Fresh From College/ Uni) ukiwa na vyeti na sifa zinazostahili kitaaluma kwa nafasi husika halafu unaambiwa huwezi kuchaguliwa sababu huna uzoefu na kazi.
NB: Baadhi ya Taasisi zilizoendelea pia huwa wana utaratibu wa kuchagua Experience Over Academic Qualification kwa sababu mbalimbali.
5 Reasons Why Experience Matters More Than Education
KIJAMII :
Athari inayoweza kupatikana ni kuwa na vijana wengi wasiojishughulisha mtaani na kupelekea makundi yasiyo na tija, sambamba na kudumaza maendeleo kutokana na jamii kuwa tegemezi kwa kukosa watendaji kazi wa kutosha, au hata watoa mawazo jengefu yanayoakisi hali halisi ya kijamii na kiutendaji ili kufanikisha maendeleo.
TATIZO LA KUCHUKULIA KWA WEPESI SUALA HILI:
Iwapo suala la kujitolea likichukuliwa kwa wepesi, na vijana wasipokuwa na muamko wa kujitolea na kuonyesha mfano suala la maendeleo binafsi na kijamii haliwezi kufanikiwa.
Kwa wale wanaopata fursa hizi za kujitolea wanapozitendea haki ni rahisi kufanya Mashirika,taasisi na Jumuiya zetu za kijamii kuona umuhimu wa kuendelea kutoa nafasi zaidi kwa vijana wengine na kufanya nao kazi na kuwa endeleza kupitia ushiriki wao katika mazingira halisi ya kazi.
(Baadhi ya wanaopata kazi hizi za kujitolea huzembea nafasi hizo na kuharibu sifa za wengine ambao ni wachapa kazi na wenye nia ya dhati ya kujifunza wanaotafuta fursa hizi- Unapopata Wasaa wa kufanya shughuli hizi Fanya kwa Moyo na Jitihada zote huenda hapo ndipo utapokuja kupata ajira, kuzoa uzoefu na kuwa bora zaidi au kutengeneza Network zenye manufaa zaidi baadae).
SUALA LA MUDA na WAPI UTAFANYA KAZI ZA KUITOLEA:
Changamoto nyingi za Vijana wenzangu utasikia "Tatizo sina Muda Unaba, sina muda wa kutosha Kufanya kazi za Kujitolea" au "Wapi naweza kwenda Kujitolea?"
Kujitolea hata kwa saa Moja au Mbili tu Kila siku kama upo sehemu sahihi na unafanya kilichokupeleka ina COUNT, mfano: Unajitolea saa moja kuwa kiongozi kanisani, kushiriki katika Vikao vya maendeleo, au Kusaidia Kufundisha katika kituo cha Watoto Yatima mtaani nk. kwako hiyo ni BIG STEP!
Mbali na kufanya kazi za kujitolea, kutana na watu, Ongea nao vizuri badilishana nao mawazo hapo unaweza kuongeza au kupata kitu cha ziada pia.
Iwapo ni Mwanafunzi kipindi cha Likizo unaweza kuomba kushiriki kazi za kujitolea katika kikundi rasmi cha vijana Mtaani kwako/ Serikali ya mtaa au Taasisi iliyo karibu na wewe kisha give it 100% hiyo inaweza kukuinua na kuongeza wigo wa Ufahamu wa mambo pamoja na kujuana na watu wa Tabaka, Rika, Taaluma na Utashi tofauti kisha ukajifunza au wao kujifunza jambo kutoka kwako.
Inafahamika kuwa Kujitolea kuna umiza katika suala la nauli iwapo sehemu ya kazi ni mbali na ulipo ukiwa bado huna chanzo cha uhakika cha mapato na hususani kama sehemu unayofanyia kazi haina utaratibu wa Posho/nauli, ufanikiwa kujiwezesha katika hili hesabu kama ni Investment kwa ajili ya future yako.
Naomba kuwasilisha na karibuni kwa Maswali, Maoni na Ushauri wa kujenga zaidi ili kuangaza jamii yetu Vijana katika kushika hatamu ya maendeleo
Kaka Pekee!
0677679339

- WASIFU-Kujiongezea Ufahamu na Ujuzi zaidi wa shughuli/Kazi humsaidia mhusika kuongeza thamani katika wasifu wake (CV) katika ushindani wa nafasi za kazi.
- USHINDANI KATIKA AJIRA- Waajiri wengi siku hizi huangalia Vyeti na Uzoefu pindi unapotuma maombi ya kazi, kupitia hizi hizi kazi za kujitolea unaweza kupenya katika uchaguzi wa awali (Screening) na kuzingatiwa kwa hatua ya Usahili wa ana kwa ana (Personal Interview).
- UBOBEZI- Kazi za kujitolea husaidia Mhusika kujiamini zaidi katika uwanja wake wa kazi sababu ya kuwa mbobezi/ mzoefu kutokana na muda wa kufanyia kazi vile alivyojifunza kwa vitendo zaidi, kupata muda wa kufanya makosa na kujirekebisha.
- MTANDAO-Pia Mtu anayefanya kazi za kujitolea huwa na wigo mpana wa kufahamiana na watu katika fani, tasnia husika hivyo kutengeneza Mtandao (Network) ambayo huweza kuwa na manufaa baadaye iwapo utautumia vizuri. Watu unaokutana nao hutathimini na kuona utendaji, wanaweza kuwa washauri, walezi wako na kuwa rahisi kwao kukutambulisha kwa wadau wengine zaidi au hata kukupa ajira rasmi...lakini pia hata kuwa rahisi kufanya nao kazi kutokea nje ya taasisi husika iwapo utakuwa na uhitaji.
- MTAZAMO NA KUFANYA MAAMUZI- Kusaidia kumjenga mhusika kimawazo na kimtazamo, kumfanya awe na tija kwa jamii (Mawazo atakayokuwa akitoa huakisi yale anayoyafahamu na watu wanaomzunguka hivyo akifahamu mengi zaidi kwa nadharia na vitendo kutamfanya afikiri na kutoa mawazo chanya, na kushiriki katika kutoa maamuzi) pia kupitia kujishughulisha na kazi kutampunguzia kujihusisha na makundi yasiyo na tija na kumfanya awe Productive.
- KUWA SEHEMU YA MAENDELEO- Kazi za kujitolea zinazohusisha jamii husaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Taasisi/ Jumuiya zinazofanya kazi za kujamii humuwezesha kijana anayefanya kazi hizo kuwa sehemu ya maendeleo na kusaidia kufanikisha Maendeleo chanya. (Hata Ukiamua kufanya kazi ya kujitolea kufanya usafi, kuhamasisha vijana kupima nk. inakuwa ni mchango mkubwa sana kijamii)