Kijana kataa kujitolea, kujitolea ni utumwa, kujitolea ni laana

Sharbel

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,076
2,242
Hivi karibuni, kumetokea na wimbi kubwa la taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali kutoa nafasi za kujitolea kufanya kazi.

Kimsingi huo ni unyonyaji tu maana wao unawazalishia alafu wanakupa ujira mdogo au kutokukulipa kabisa.

Vijana wengi wameingia huko labda wanadhani kujitolea pengine inaweza kukupatia nafasi ya kupata ajira, lakini wanajikuta miaka inaenda na ajira hamna.

Zipo taasisi asilimia 60% ya wafanyakazi wake ni wakujitolea tu, yaani wao wanaingiza pesa na huku kutolipa chochote kwa hao wafanyakazi wao.

Mwisho nimeshangaa sana wizara ya afya inatoa nafasi za kujitolea katika hospital ya maweni kigoma na kuwalipa asilimia 50% ya mshahara wao, ilhali inao uwezo wa kutoa hizo ajira.

Kijana kataa kujitolea,
Kujitolea ni utumwa,
Kujitolea ni laana,
Kujitolea ni wizi,
Kujitolea ni utapeli,
Kujitolea ni unyonyaji,
Kataa kujitolea,
Kataa kujitolea.

2000102296.jpg
 
Makampuni mengi tu hayaajiri Bali uchukua watu wa kujitolea wanatumikisha hasa,wakija wakaguzi wanasema anajitolea ili kukwepa mkono wa sheria.
Watakunyonya hadi uondoke mwenyewe ajira no.
Kama unapata cheap labour kwa nn uajiri uingie gharama za kulipa mshahara,kodi,nssf,afya,nk
 
View attachment 2660166

Huenda ukawa umejaribu kuweka upande mbovu wa sarafu.
Ni kweli inayosema ndugu.

Ila kuliko vijana kushinda mtaani, kujiigiza kwenye madawa, wizi n.k ni bora kujitolea kwanza unafahamiana na watu wengi hapa unatengeneza connection doesn't matter utaajiriwa hapo au hautaajiriwa.
Pili utapata experience ya kutosha jinsi ya kuishi na watu, kuongea kama na wateja n.k
HALI ni ngumu kitaa ACHA watu wapambane.
 
Vijana waamke la sivyo watakumbuka shuka alfajiri, ila kinachoniuma zaidi kuona serikali nayo wameanza haka katabia. Sasa wizara ya afya juzi tu hapo imetoa ajira na bado hawajarudisha majibu, sasa kwanini wasijumuishe na hizo za kigoma, kuna kitu gani hapo ? au serikali haina hela
 
Utakuta inaajiri wapya inaacha kuwapa kipaumbele waliojitolea
 
Huenda ukawa umejaribu kuweka upande mbovu wa sarafu.
Ni kweli inayosema ndugu.

Ila kuliko vijana kushinda mtaani, kujiigiza kwenye madawa, wizi n.k ni bora kujitolea kwanza unafahamiana na watu wengi hapa unatengeneza connection doesn't matter utaajiriwa hapo au hautaajiriwa.
Pili utapata experience ya kutosha jinsi ya kuishi na watu, kuongea kama na wateja n.k
HALI ni ngumu kitaa ACHA watu wapambane.
Hivi si kila kozi sasa inafundisha entrepreneurship huko mavyuoni inalenga hasa kuwaandaa vijana wakajiajiri, kwanini ujitolee, hamna shughuli nyingine za kufanya na zikakuingizia pesa, na ukiwa kijana ndio mda wa kuandaa maisha, sasa fikira unatumia huo mda kumzalishia mwingine na wewe unatoka patupu.
 
Ushuhuda

Nimeshawahi kujitolea kwenye kikampuni falani hivi- nilipigika miezi sita bila chochote na uzoefu nilipata sema uzoefu ambao nisingeweza ufanyia kazi popote isipokuwa hapo nilipoupata, posho ilikuwa elf 3 , pengine aje? Mteja umpandishie bei ya huduma ndio utapata zaidi, nauli hapo hapo kwenye elf 3 yako, kula ofisini- nilikimbia mbio ndefu sanaa baada ya kugundua boss wa ofic ndio michezo yake hiyo kufanyisha watu kazi bure

Watu wengine ovyoo sanaa
 
Ndio maana kwenye taasisi upigaji hauishi, anayejitolea ili ku survive analazimika afanye upigaji apate hela ya ugali.
 
Back
Top Bottom