Jinsi ya kuandika CV, wasifu wa kazi unaovutia

Jan 17, 2024
47
71
Sehemu ya Kwanza: Maelezo Binafsi na Mawasiliano

Maelezo ya Kibinafsi:
Anza CV yako kwa kujitambulisha kwa jina lako kamili, anwani, namba ya simu, na anwani ya barua pepe. Hakikisha maelezo haya yako wazi na sahihi.

Muhtasari wa Kibinafsi:
Ongeza muhtasari mfupi wa kibinafsi unaoweka bayana malengo yako ya kazi na sifa zako kuu. Sehemu ya Pili: Elimu na Mafunzo

Elimu:
Orodhesha taasisi zote ulizohudhuria, shahada zako, na tarehe za kuhitimu. Tambua pia mafunzo yoyote ya ziada au kozi ambazo zinaongezea uwezo wako wa kitaaluma.

Mafunzo ya Kazi:
Kama umepata mafunzo ya ziada yanayohusiana na nyanja yako ya kazi, weka maelezo kuhusu hilo.

Sehemu ya Tatu: Uzoefu wa Kazi

Uzoefu wa Kazi:
Anza na kazi yako ya hivi karibuni na endelea kuelekea nyuma. Eleza majukumu yako na mafanikio muhimu uliyopata kwa kila jukumu.

Mafanikio na Utendaji:
Ongeza maelezo kuhusu mafanikio yako na jinsi ulivyochangia katika maendeleo ya kampuni au taasisi zilizopita. Sehemu ya Nne: Uwezo na Maarifa

Lugha na Uwezo wa Kompyuta:
Eleza lugha unazojua na uwezo wako wa kutumia programu na zana za kompyuta.

Ujuzi na Stadi:
Andika kuhusu ujuzi wa kitaaluma na stadi za kazi kama vile uongozi, timu, na mawasiliano.

Sehemu ya Tano: Kazi za Kujitolea na Hobbies

Kazi za Kujitolea:
Kama umeshiriki kwenye shughuli za kujitolea, eleza jukumu lako na jinsi shughuli hizo zimekuongezea uzoefu.

Hobbies na Shughuli Binafsi:
Pia, onyesha muda wako wa burudani na shughuli binafsi zinazojenga taswira yako nje ya eneo la kazi.

Sehemu ya Sita: Marejeo na Vifaa Zaidi

Marejeo:
Kama una marejeo, orodhesha majina na maelezo ya mawasiliano ya watu wanaoweza kutoa mapendekezo kuhusu uwezo wako.

Vifaa Zaidi:
Kama una nyaraka zaidi kama barua za mapendekezo au vyeti vya mafunzo, hizi zinaweza kuambatishwa mwishoni.

Kupata Elimu zakibiashara zaidi usisahau Kudownload Swahili Explore - Apps on Google Play au kutembelea Home - Swahili Explore
 
CV unayoweza kuipa madodoso yote hayo na ikapewa nafasi kwenye nchi aliyoiimba Ney wa Mitego nadhani bado sana.

Hiyo kitu kwa nchi zetu za dunia inayochipuka bado sana, labda kwa waliotangulia hapo kabla.
 
Bongo CV inayovutia bila connection ni kazi bure.
Sio kweli Nina uhakika ninachoongea Kuna bosi alisimamia interview ya kampuni ya marketing officer officer ya kampuni moja ya mafuta ya kimataifa
Serikali ilikomaa kuwa hawatakiwi kuajiri makerting officer raia wa nje wakati vyuo vyetu wamejaa waliosoma Makerting officers kibao hawana kazi na Wana degree na diploma

Anyway waombaji walioomba wenye sifa walizopewa na serikali wakifika elfu mbili Wao wakati walihitaji wawili tu wakaambiwa Kila mtu atume CV yake alifanikiwa mmoja tu na yeye aliandika mbaki na kuwa na Digrii ya Marketing ni mwanasheria wakili tatizo likitokea kwenye bidhaa au kesi aweza simama mahakamani yeye kama wakili Kwa mshahara huo huo wa Makerting officer na pia anajua kifaransa lugha inayotumiwa na masoko ya nchi jirani kama Congo nk ni multilingua na kifaransa alisoma Kipindi Hana kazi akapata kazi chap chap baada ya kuamua kumwita Kwa oral

CV sio kupamba maneno kama mwali anayejipodoa ni reality ya who you are
 
Kampuni ya kimataifa sawa mkuu wenzetu wananyoosha mambo yao.

Fanya utafiti wa kampuni zilizopo bongo ambazo mchakato wa ajira unasimamiwa na ngozi nyeusi uone mambo yalivyo meusi.
 
Uko sahihi kampuni za kimataifa huhitaji vichwa best hawana utani Wala michezo ya kijinga kama hiyo .Wakitaka mtu wa fani yeyote kichwa chake lazima wahakikishe Kiko fit

Nakubaliana na wewe ndio maana nchi za Africa kuendelea Vigumu sababu wanawekana ohh Huyu dini yangu kaa pale ohh Huyu wa kijijini kwetu kaa pale ohh Huyu mtoto wa ndugu yangu kaa pale ohh Huyu mtoto wa rafiki yangu kaa pale ohh Huyu hawara yangu kaa pale nk hakuna mfanyakazi Wala mtu wa maana Kwa mchujo huo ujinga mtupu
 
Hakika.

Wenzentu wanazidi kutupiga bao kwasababu wapo serious sana.
 
Sehemu ya Kwanza: Maelezo Binafsi na Mawasiliano

Maelezo ya Kibinafsi:
Anza CV yako kwa kujitambulisha kwa jina lako kamili, anwani, namba ya simu, na anwani ya barua pepe. Hakikisha maelezo haya yako wazi na sahihi.

Muhtasari wa Kibinafsi:
Ongeza muhtasari mfupi wa kibinafsi unaoweka bayana malengo yako ya kazi na sifa zako kuu. Sehemu ya Pili: Elimu na Mafunzo

Elimu:
Orodhesha taasisi zote ulizohudhuria, shahada zako, na tarehe za kuhitimu. Tambua pia mafunzo yoyote ya ziada au kozi ambazo zinaongezea uwezo wako wa kitaaluma.

Mafunzo ya Kazi:
Kama umepata mafunzo ya ziada yanayohusiana na nyanja yako ya kazi, weka maelezo kuhusu hilo.

Sehemu ya Tatu: Uzoefu wa Kazi

Uzoefu wa Kazi:
Anza na kazi yako ya hivi karibuni na endelea kuelekea nyuma. Eleza majukumu yako na mafanikio muhimu uliyopata kwa kila jukumu.

Mafanikio na Utendaji:
Ongeza maelezo kuhusu mafanikio yako na jinsi ulivyochangia katika maendeleo ya kampuni au taasisi zilizopita. Sehemu ya Nne: Uwezo na Maarifa

Lugha na Uwezo wa Kompyuta:
Eleza lugha unazojua na uwezo wako wa kutumia programu na zana za kompyuta.

Ujuzi na Stadi:
Andika kuhusu ujuzi wa kitaaluma na stadi za kazi kama vile uongozi, timu, na mawasiliano.

Sehemu ya Tano: Kazi za Kujitolea na Hobbies

Kazi za Kujitolea:
Kama umeshiriki kwenye shughuli za kujitolea, eleza jukumu lako na jinsi shughuli hizo zimekuongezea uzoefu.

Hobbies na Shughuli Binafsi:
Pia, onyesha muda wako wa burudani na shughuli binafsi zinazojenga taswira yako nje ya eneo la kazi.

Sehemu ya Sita: Marejeo na Vifaa Zaidi

Marejeo:
Kama una marejeo, orodhesha majina na maelezo ya mawasiliano ya watu wanaoweza kutoa mapendekezo kuhusu uwezo wako.

Vifaa Zaidi:
Kama una nyaraka zaidi kama barua za mapendekezo au vyeti vya mafunzo, hizi zinaweza kuambatishwa mwishoni.

Kupata Elimu zakibiashara zaidi usisahau Kudownload Swahili Explore - Apps on Google Play au kutembelea Home - Swahili Explore
Asante

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom