Kwa hakika mwanaume aliyekamilika na anayejitambua kamwe hawezi kuwa hivyo kwa kuwa inafahamika kuwa ni jukumu la mwanaume kutunza familia....lakini dada yangu siku hizi kidogo mambo yamebadilika wanawake nao wanajishughulisha sasa kuna ugumu gani kusaidiana na mwenzio katika mambo madogo madogo kama hayo.....??...kwa mfano utamuombaje mumeo hela ya pedi ikiwa nawe umaingiza kipato.....unapogoma kuchangia au kulipa ada ya mtoto wenu wakati unatambua kuwa mumeo yupo kwenye kipindi kigumu kifedha unadhani unamkomoa nani....???
Ndoa ni kusaidiana na kuthaminiana.....
Napata tabu kujua huo usawa mnaoulilia sijui unalenga nini....??.maana kwa maoni yangu ingetakiwa usawa muuonyeshe hapo kwenye kukabiliana na majukumu ya kifamilia....na sio kwenye mambo ya kipuuzi......
Akichangia, hand bag ya laki mbili na wigi la gharama atalipiaje? Unataka kazini muda wa breakfast na lunch aonekane ye mtu wa kawaida kuonekana anakula mgahawa wa pembeni local na sio kuagiza kile cha kule steers?
Asante Mungu yeye si mke wangu.