Kazi ya pesa ya mwanamke ni kufanya nini?

Kwani ni mkewe? Kwenye tendo Raha si wanapata wote? Ingekuwa huyo mdada ni jobless, ningemwelewa, sasa pesa ya uyo mdada inaenda wapi Missy Gf
Sasa jamaa anashindwa kumuhudumia dada kwa vitu vidogo vidogo tu hadi demu anaishia kulalamika
Hata kama anafanya kazi huduma za hapa na pale mwanaume zisikushinde
Ukiona haummudu tafuta pa kula bure asimchoshe dada wa watu
 
Money of woman(hela za wanawake)
Zinaliwa na ndugu zao wa kiume
Wanawake wengi ndio wanaingia kwa kujenga kwao na kuwasaidia watoto wa kaka zao

Nina mwanamke mmoja now ni muajiriwa IRC kawajengea kaka zake wawili nyumba na anasomesha watoto wa ndugu zake jumla watoto 5 alafu Ada ya mwanangu Mimi na yeye lazima anitafute nilipe na nikijikausha anakuandikia deni
Nawewe mkuu somesha ndugu zako, Wanawake kama huyo wako wanakuwa na Bahati ya kuolewa na mwanaume ambaye hatoki kwenye familia yenye njaa njaa

Sent from my SCV48 using JamiiForums mobile app
 
Hamna kiumbe mbinafsi kama mwanamke na ndio maana kuna baadhi ya watu wanapenda kuoa wamama wa nyumbani. Hapo utakuta ana kazi kurudi saa mbili usiku kutoka saa kumi na mbili asubuhi, akiguswa usiku anasema amechoka, hela yake haionekani.

Ndoa inataka udikteta kidogo

Kama mke anafanya kazi ajue kabisa hicho kipato ni cha familia kwahiyo kitapigiwa hesabu kwenye mipango ya familia.

Hataki aache kazi au ndo ife. Mtu hawezi kutumia muda wa famili kwa mambo yake binafsi never.

Tatizo letu wengi tumeingia kwenye demokrasia ya kijinga ndio maana tunapata tabu sana
 
Imagine mtu mzima mwenye meno 32 kama wewe, Mwenye elimu kama wewe au pengine kakuzidi, Mwenye kazi na analipwa mshahara vizuri tu kama wewe... Tena ukiangalia waweza kukuta wote mmetokea familia masikini kweli hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuikwamua ya kwakwe na ndo sababu wazazi wenu kila mmoja akawa akimpambania mwanae afike mahali fulani ili aje ajikomboe na maisha yake na hakuna mzazi wa mtoto wa kike alietokea kusema hela ya kumpeleka mwanangu shule apewe mtoto wa kiume wa fulani ili baadae aje kumuhudumia huyu wakike, Wote walikuwa treated the same na wazazi wote wakiwa na matarajio makubwa kwa wote (wakiume kwa wakike).... Then leo ndo huyu mmoja eti kwa kuwa yeye ana papuchi anataka kuitumia kumrubuni mwenzake aanze kumuhudumia yeye huku analalamika kabisa as if ni haki yake.

Dear men this world usipotumia akili kuishi na hawa watu utateseka sana.... Acheni kupoteza muda na watu ambao wanajijaliwa wao kuliko ninyi mtaendelea kufa mapema mpaka mnyooke

Mwanamke wa sasa sio kiumbe dhaifu kiasi cha kumfanyia majukumu yake, Mwanamke wa sasa anajimudu na anaweza hata ku-replace nafasi yako ukikaa kiduwanzi hivyo hupaswi kuishi kwa kumuonea huruma na kuhisi kwamba yeye ni wa kuhitaji msaada wako kila wakati.

Ukiishi ninavyokuelekeza uta-save mambo mengi mno kwenye maisha ikiwemo Depression na Hasira za kufanya maamuzi ya ajabu pindi ikitokea usaliti kwenye mahusiano yenu maana watu wengi hufikia kutokuwa na maamuzi ya busara kwa kuwa walipoteza Gharama kubwa kwa hawa watu ndo maana haiwezi kuwa rahisi kuachia bila tough decision.
 
Back
Top Bottom