Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,617
- 34,062
DISCLAIMER: Huu ni mtazamo wangu tu kuhusu hili suala kwa jinsi nilivyoliona na kulishuhudia. Sina maslahi yoyote na suala hili.
=========
Ni maajabu juu ya maajabu. Nchi ina maajabu sana hii.
Iko hivi:
Hivi karibuni bungeni, Mb. Shabiby na Tabasamu waliibua hoja kwamba serikali imepigwa sana pesa (Tsh 3B kila mwezi) na kampuni iliyokuwa inatumika kuweka vinasaba (marking) kwenye mafuta. Ifahamike kuwa hili siyo suala la kuweka kama walivyojaribu kupotosha wabunge pamoja na Speaker Ndugai, bali huhuhisha vipimo na utaalamu.
1- Kumbuka Uwekaji wa vinasaba (marking) hurahisisha ufuatiliaji wa mafuta yanayouzwa kwa siku ili kuweka kumbukumbu sawa za ulipaji kodi.
Na ili kurahisisha hili ndio maana serikali kupitia EWURA ikatangaza tender ya kuipata kampuni husika kwaajili ya kazi hiyo. Malipo ya kampuni hiyo yalitokana na tozo ya Tsh 17 kwa kila litre moja ya mafuta na ilipaswa kulipwa na wamiliki wa depots.
Mkanganyiko,
1: Mhe. Shabiby, Speaker Ndugai na Waziri Kalemani wanasemaje eti pesa ya serikali ilikuwa inapigwa wakati pesa inalipwa na wamiliki wa depots?
2: Hivi inakuwaje bunge lenye kamati ya kudumu ya nishati inashindwa kutembelea kampuni husika pamoja na depots na badala yake wanafanya maamuzi kwa kujishuku shuku tu?
3: Ieleweke kuwa kampuni husika iliyokuwa inafanya kazi ya vinasaba imekuwa ikipewa tender kila baada ya miaka 3. Na baada ya mkataba wao kyisha, EWURA walitangaza tender, ambayo inavyoonekana ilishinda kampuni ya Intertek.
Sasa ilikuwaje badala ya kupewa wao kazi, imepigwa U-turn wanapewa TBS?
Haya mambo ya serikali kufanya biashara yenyewe kwa yenyewe yataisha lini?
4: Unaposema ile pesa waliokuwa wanalipwa waweka vinasaba ipelekwe RUWASA na TARURA inakuwa vipi tena kuchota pesa kwa kumiliki wa mafuta na kuzipelekwa kwenye Maji na Barabara?
Je, wamiliki wa depots wakianza kuikataa hiyo tozo ya Tsh 17 itakuwaje?
Na, Je kama TBS wakiwa ndio wanafanya kazi maana watahitaji kuwa na staff wa kufanya kazi hiyo
Je, watawalipaje ikiwa pesa mnataka kupeleka RUWASA na TARURA?
5: Inakuwaje Waziri Kalemani anaongea tu kwente vyombo vya habari kwamba mafuta yote yawekewe vinasaba wakati TBS wenyewe hawana ujuzi wala hawajui kazi inafanyikaje mpaka sasa wala hawana staff wa kufanya kazi hiyo?
6: Hii kampuni iliyokuwa inafanya kazi mbona mpaka sasa bado inaendekea kufanya kazi Zanzibar kama ni ya kifisadi kama mlivyosema?